Iwapo mtu amefia nyumbani kwake na mwili wake ukabidi kwenda kuhifadhiwa hospitalini, kwa nini haubebwi na ambulance?
Na iwapo utabebwa na kwa njia nyingine yoyote, kwa nini mwili hawaufuniki?
Na wanapofika hospitalini, kwa nini sio wahudumu wa hospitali wanaowajibika kuutoa mwili huo badala ya walioupeleka hapo?
Nini nafasi ya polisi katika uchunguzi wa kesi kama hii? Baada ya kila hatua ya awali kuchukuliwa na ndugu na majirani?
Refer kifo cha S. Kanumba.
Mkuu heshima mbele.
Umeleta swali ambalo mimi mwenyewe nimekuwa nikifikiria kila siku kwamba kwanini sisi watu tunafanya mambo kienyeji mno.
Utaratibu ambao ungefanyika ambao duniani kote wanafanya ni kwamba.
1. Ndugu wa marehemu alipogundua kwamba marehemu amefariki alipaswa kupiga simu polisi na kutoa taarifa ya kifo na polisi wangefika eneo la tukio mara moja.
2. Polisi kama wangefika nyumbani kwa marehemu wangezungusha uzio eneo lote linalozunguka nyumba ya marehemu na lingejulikana kwamba ni "murder scene" na mtu yoyote haruhusiwi kuingia kwenye eneo hilo.
3. Polisi wangeita watu wa ambulance ambao wangefika mahala hapo na baada ya kuridhika kwamba marehemu amekwishafariki wangeutia mwili wa marehemu kwenye fuko la kubebea maiti na kuupeleka chumba cha maiti Muhimbili ambako ungehifadhiwa na pathologist angesubiriwa kufanya uchunguzi zaidi au "post moterm".
4. Polisi wangeweka doria kwenye eneo hilo na mtu yoyote kutoruhusiwa kuingia humo.
5. Polisi wangemkamata ndugu wa marehemu na huyo msichana ili kuchukua maelezo na baada ya hapo polisi wangetoa taarifa kwamba kuna mtu amefariki (merehemu Kanumba) nyumbani kwake katika mazingira yasoeleweka na watu wawili wanashikiliwa na maelezo mengine yatatolewa baadae.
Sasa labda jumanne au katikati ya wiki ijayo polisi wangetarajiwa kutoa taarifa kwamba kutokana na ushahidi ambao wameukusanya wanamfungulia mashtaka yoyote ambae walikuwa wakimfanyia mahojiano na ambe wamemtia ndani.
Kwa sasa kila sehemu ya eneo hilo limetapakaa vidole na ushahidi wote umekwishavurugwa au "contaminated" ingawa wananchi wamejitahidi kadri ya uwezo wao kufanya kazi zote za polisi jambo ambalo si jukumu lao.
Huu ndio utaratibu ambao unatoa haki kwa kila mtu yule alekufa na wale wanaobakia hapa duniani.