Utaratibu wa kubeba maiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu wa kubeba maiti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibunango, Apr 7, 2012.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Iwapo mtu amefia nyumbani kwake na mwili wake ukabidi kwenda kuhifadhiwa hospitalini, kwa nini haubebwi na ambulance?

  Na iwapo utabebwa na kwa njia nyingine yoyote, kwa nini mwili hawaufuniki?

  Na wanapofika hospitalini, kwa nini sio wahudumu wa hospitali wanaowajibika kuutoa mwili huo badala ya walioupeleka hapo?

  Nini nafasi ya polisi katika uchunguzi wa kesi kama hii? Baada ya kila hatua ya awali kuchukuliwa na ndugu na majirani?

  Refer kifo cha S. Kanumba.
   
 2. pepim

  pepim JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  No research, no right to say.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  research ya kitu gani?
   
 4. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  An ambulance is a vehicle for transportation of sick or injured people to, from or between places of treatment for an illness or injury,
   
 5. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu heshima mbele.

  Umeleta swali ambalo mimi mwenyewe nimekuwa nikifikiria kila siku kwamba kwanini sisi watu tunafanya mambo kienyeji mno.

  Utaratibu ambao ungefanyika ambao duniani kote wanafanya ni kwamba.

  1. Ndugu wa marehemu alipogundua kwamba marehemu amefariki alipaswa kupiga simu polisi na kutoa taarifa ya kifo na polisi wangefika eneo la tukio mara moja.

  2. Polisi kama wangefika nyumbani kwa marehemu wangezungusha uzio eneo lote linalozunguka nyumba ya marehemu na lingejulikana kwamba ni "murder scene" na mtu yoyote haruhusiwi kuingia kwenye eneo hilo.

  3. Polisi wangeita watu wa ambulance ambao wangefika mahala hapo na baada ya kuridhika kwamba marehemu amekwishafariki wangeutia mwili wa marehemu kwenye fuko la kubebea maiti na kuupeleka chumba cha maiti Muhimbili ambako ungehifadhiwa na pathologist angesubiriwa kufanya uchunguzi zaidi au "post moterm".

  4. Polisi wangeweka doria kwenye eneo hilo na mtu yoyote kutoruhusiwa kuingia humo.

  5. Polisi wangemkamata ndugu wa marehemu na huyo msichana ili kuchukua maelezo na baada ya hapo polisi wangetoa taarifa kwamba kuna mtu amefariki (merehemu Kanumba) nyumbani kwake katika mazingira yasoeleweka na watu wawili wanashikiliwa na maelezo mengine yatatolewa baadae.

  Sasa labda jumanne au katikati ya wiki ijayo polisi wangetarajiwa kutoa taarifa kwamba kutokana na ushahidi ambao wameukusanya wanamfungulia mashtaka yoyote ambae walikuwa wakimfanyia mahojiano na ambe wamemtia ndani.

  Kwa sasa kila sehemu ya eneo hilo limetapakaa vidole na ushahidi wote umekwishavurugwa au "contaminated" ingawa wananchi wamejitahidi kadri ya uwezo wao kufanya kazi zote za polisi jambo ambalo si jukumu lao.

  Huu ndio utaratibu ambao unatoa haki kwa kila mtu yule alekufa na wale wanaobakia hapa duniani.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ukikumbuka tukio la Fabrice Muamba
  napata wasiwasi tunazika wengi wakiwa hai still...
  hii nchi utasema tuko miaka ya sitini bado
  ajabu mno.....
   
 7. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  For forensic reasons ni kosa, hii inaweza kumsevu lulu, finger prints, marks of violence disgused.
   
 8. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inawezekana kanumba alikuwa hajafa .uzembe wetu na vitendea kazi na madaktari wetu
   
 9. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna magonjwa mengine hata ukifanya CPR (Cardiopulmonary Resuscitation) haisaidiii. Bila kujali marehemu alikuwa anaumwa nini, nadhani kuna makampuni binafsi hapa bongo kama Ultimate Security ambayo huwa na paramedics, kwa hiyo ukishapata tatizo la style hii wakija kwako kitu cha kwanza wanachofanya ni CPR. Sio CPR wafanya zaidi ya nusu saa baada ya kufa (unapofikishwa hospitalini). Na kwa kesi ya Muamba, kila daktari anaamini ile ni miraculous healing na si ubora wa vifaa au utoaji huduma.
   
 10. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nimeshangaa ndugu kupeleka mwili mortuary, Polisi ndio walipaswa kama alikuwa amefia nyumbani. Kisheria hawawezi kuuzika bila ruksa ya polisi. Eneo lilipaswa kuwa chini ya uangalizi wa polisi wakati wakichukua picha na ushahidi. Ila kama alipelekwa bado mzima ni sawa huduma za ambulance wakati mwingine huchelewa mara nyingi kesi kama hizi mgonjwa anatakiwa awe stabilized kabla ya kumchukua kama wanavyofanya kwa wachezaji. Still long way to go ila tutafika
   
 11. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ilitakiwa iwe hivyo lkn basi tu.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Hatuna jeshi la polisi nchi hii. Labda wafyatua mabomu na risasi kwa waandamanaji.
  Nimekuwa najiuliza kwa issue kama ya Steven Manumba polisi wana ushahidi gani hadi sasa hivi au ni masimulizi tu? Wametembelea hata sehemu inayosemekana kuwa ndio eneo la tukio? Au wanakula maandazi na kusikiliza story za mimi nikafunga mlango na mara nikasikia kitu kizito kimedondoka?
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  kwani wewe umeongea nini?
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Mnawaza mbali sana.

  Hivi hata basic needs zimetushinda, sembuse ya uchunguzi wa kipolisi??

  Kwa elimu zetu za kata sipiyu inachorwa ubaoni?

  Bado tuna hatua ndefu sana.
   
 15. u

  utantambua JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii itawezekana tu pale tutakapoweza kujenga mabarabara ya juu, daraja la Kigamboni kuwa na umeme wa kutosha, kima cha chini cha mshahara cha shilingi milioni moja, na kuwa na wastaani wa kuishi wa miaka 65. Hii itakuwa mwaka 3012 yaani milenia ijayo.

  Hata hivyo namba 5 hapo umedanganya, polisi wa nchi zilizoendelea hawakamati tu mtu kwa kuwa amekutwa eneo la tukio bali ni baada ya kureview evidence na kujiridhisha kuwa mtu husika anafaa kuitwa mtuhumiwa.
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Madaktari walipogoma kwa vifaa duni watanzania tukawadharau na kuwaona wasaliti wanadai posho. Ila this is the price we pay. Watu kuwa declared dead 1 hour before they are dead (ie kama kuna vifaa wangeokolewa), Moyo kusimama si sababu ya kutamka mtu kafariki. Inatakiwa tamko hilo lifanyike baada ya huduma zote za dharura kufanyika na kushindikana hasa kwenye issue za dharura kama Kanumba.

  Tunahitaji mabadiliko katika huduma za afya kwa kweli. Polisi nao wanafanya kizamani. Ukisema wanakwambia kuwa nchi yetu masikini na wanatumia udhaifu huu kuombea misaada na kuielekeza kwenye private accounts zao.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Polisi wa sasa wanakuwa trained kupambana na waandamanaji zaidi na kupiga mabomu wapinzani. Kesi kama hizi wao huziona ni kama something else. Saa ngapi mtu afuate utaratibu huo?, Kwanza Tanzania hakuna numba za dharura zinazofanya kazi 'Hatuna first responders' Yaani tunaisha kwa kudra ya mwenyezimungu na ukiwa na bahati mbaya kama ya Kanumba ukapata dharura basi tena utakufa huku unajiona. Tunahitaji kujenga people centred country sio leader centered country. Kama kale ka ambulance anakotembea nako JK kangekuwa available kwa kila mtanzania basi leo hii huenda tungekuwa tunaongea kuwa Kanumba anaendelea vizuri hospitali.
   
 18. O

  Omtata Member

  #18
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kwani tz kuna polisi?
  Naipenda chadema
   
 19. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ....komentini bila ku Quote.... Mnatupotezea muda wa ku scroll down.... Alaaaa!!
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Polisi wakipeleka maiti wao ni more worse manake wao wataweka nyuma ya defenda na defender zinakuwa na strecther only wakati wa maandamano. wanao funika ni wasamalia wema ndio wanao jitolea kanga, shuka au mikeka.

  Na wasanii wapunguze kuuza nyago mengine ni hatari kwao, wengine walikuwa na kufuru kwa kudhani montuary ni kwa ajili ya watu flani tu na wao hawausiki. Wakati wa msiba ni vyema tukakumbuka kila mtu atakufa siku moja.

  Elimu ya first aid bado kueleweka kabisa manake hata wengine walipata kuzimia na huduma za kwanza ndio zile zile tulizoea sio kama muamba alivyohudumiwa.
   
Loading...