Utaratibu unaotakiwa kufuatwa kupata hatimiliki

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,830
2,417
Je hatimiliki ni nini?

Hatimiliki ni cheti maalumu kinachotolewa kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba nne ya 1999 kwa mmiliki wa ardhi kulingana na matumizi yake.

Kuna aina mbili za hatimiliki yaani kuna hatimiliki yenyewe(ambayo hii hutolewa kwenye ardhi ya mijini na mara nyingi kwa maeneo yale yamepimwa na yana ramani za upimaji na mipango miji.) Na kuna hatimiliki ya kimila(hii ni ambayo hutolewa kwenye ardhi za vijijini na mara nyingi kwenye maeneo ambayo hayajapimwa).

Hivyo utaratibu wa upatikanaji wa hatimiliki ya mjini na hatimiliki ya vijijini zinatofautiana.

UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA HATIMILIKI KWA ARDHI YA MJINI

I. FOMU YA MIPAKA.
Hii ni fomu ambazo hutolewa na Halmashauri husika, fomu hii inaonyesha majirani ambao unapakana nao kwa pande zote na wanatakiwa kusaini kwa kukubaliana na mipaka yako.

Pia katika fomu hii kunakuwa na sehemu ambazo ni lazima zisainiwe na Afisa Mtendaji wa Mtaa(jina,saini na mhuri) na Mwenyekiti wa Mtaa(jina,saini na mhuri).

II. FOMU YA MAOMBI YA HATI (Land Form Na.19).
Hii fomu kwa ajili ya maombi ya hati, Na hizi fomu inatakiwa ujaze mbili lakini zote za aina moja, katika fomu hii ndio unajaza taarifa zako muhimu kama jina lako kwa urefu,anuani yako na saini yako.

III. KITAMBULISHO CHA TAIFA(NIDA).
Katika uombaji wa hatimiliki ni vyema kuambatanisha na copy ya kitambulisho chako cha Taifa na ni vyema copy ikawa na rangi yake(coloured).

IV. HATI YA UTAMBULISHO(AFFIDAVIT).
Huu ni uthibitisho ambao ni lazima upeleke kwa wakili ili akusainie na kuweka muhuli wake,katika hati hii kunakuwa na sehemu za kujaza kama ukubwa wa kiwanja, eneo lilipo,Namba ya kiwanja na majina yako yote matatu.

V. MKATABA WA UMILIKI.
Unavyotaka kuanza kutafuta hatimiliki hakikisha una mkataba ambao unaonyesha umiliki wako wa eneo hilo,mkataba ambao utaonyesha kama ulinunua eneo,ulirithishwa hilo eneo au namna yoyote ile ambayo haitaleta usumbufu katika mamlaka za ardhi katika kujua umiliki wako.
Pia hakikisha mkataba huo una saini za wakili na mhuri wake ili kuuthibitisha kisheria.

VI. PICHA(PASSPORT SIZE).
Hizi picha zinabandikwa kwenye fomu ya maombi ya hati,kwahiyo ni vizuri ukawa nazo zisizopunguambili pindi uendapo kwenye mamlaka ya ardhi.

VII. RAMANI YA MIPANGO MIJI(URBAN PLANNING DRAWING).
Katika utafutaji wa hati lazima uambatanisho na ramani ya mipango miji ambayo ndio inaonyesha sehemu unayotafutia hati ina matumizi gani, Na ramani ya mipango miji inayotakiwa ni ile ambayo inakuwa imeidhinishwa na wizara na mhuri na sahihi ya Mkurugenzi wa mipango miji.

VIII. RAMANI YA UPIMAJI(SURVEY PLAN DRAWING).
Hii ndio ramani haswa huhitajika katika mammlaka za ardhi ambazo zitakusaidia kupata hatimiliki, ramani hii nilazima iwe ile iliyoidhinishwa na Mkurugenzi wa Upimaji na inatambulika na Wizara.
●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●●

UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA HATIMILIKI KWA ARDHI YA VIJIJINI
(HATI YA KIMILA)

I. Mwananchi yeyote anaetaka kumiliki ardhi atatakiwa kuandika barua ya maombi na kuipeleka kwa Mtendaji wa serikali ya Kijiji ambaye yupo katika eneo la Kijiji.

II. Halmashauri ya Kijiji itafanya uamuzi juu ya maombi hayo kukubali au kukataa na ikikataa lazima ieleze sababu za msingi kwanini imekataa.

III. Halmashauri ya Kijiji ya baada kujadili maombi hayo itayapeleka mkutano mkuu kwa ajili ya kuridhiwa na wananchi.

IV. Muhtasari wa mkutano mkuu ukiwa na majina ya waombaji wote na idadi ya ekari wanazoomba kumiliki kila mwananchi utawasilishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji.

V. Baada ya hapo waombaji watapewa wataalamu wa upimaji na uchoraji kwa ajiri ya ramani za maeneo hayo na kuandaa rasimu ya hatimiliki.

VI. Baada ya hapo hati itaandaliwa na kusainiwa na Mmiliki,Mtendaji wa Kijiji husika na Mwenyekiti.

VII. Baada yah apo mmiliki anakuwa amepewa mammlaka kamili ya kumiliki eneo hilo.

NB: Hatimiliki ya kimila huwa inafutika na kukoma kutumika endapo ardhi ya Kijiji hicho itatangazwa kuwa mji na kuidhinishwa kama eneo la mpango.

Imeandaliwa na ;
UTUKUFU CLEMENT MWANJISI
Whatsapp No; +255 713132109
Telegram No; +255 713132109
Email ; mwanjisiutukufu@gmail.com
Signature;View attachment 2488498View attachment 2488499
IMG_20230120_054651_266.jpg
 
Tunashukuru kwa kutukumbusha mambo muhimu..
Ila kama wakuu hapo juu inachukua muda gan mpk upate?? Naona mpk leo mwaka unaisha hizo simu hatuzioni tulizoambiwa tutaitwa...alipokuwepo waziri wa ujenzi yule nani sijui kanitoka mambo yalikua kidogo yanaenda chapchap..hata vibali vya ujenzi havikua vinachukua muda kutoka..
 
Back
Top Bottom