Wizara ya Ardhi iweke mfumo wa online wa Ramani za Mipango miji

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Kutokana na ukuaji wa maeneo mbalimbali, kumekuwa na ujengaji holela kwenye maeneo ambayo hayakupaswa kujengwa, mfano maeneo ya kingo za mito, maeneo ya barabara za mitaa, na barabara kuu na kadharika.

Kutokana na ukuaji wa Teknolojia na utandawazi, vitu vingi siku hizi ufanyika online kuepusha msongamano na rushwa katika ofisi za Serikali.

Wizara ya Ardhi kuendana na kasi ya Teknolojia inatakiwa kuja na ramani rasmi za maeneo yaliyoko kwenye mipango miji, ili kila raia awe na access ya kuona na kujua eneo lake liko katika mipango hipi.

Hii itaepusha hata watu walioko mbali na ofisi za ardhi kuweza kupata huduma online. Ramani zichorwe katika mfumo wa Google map au online map yoyote na ziwekwe online hili kila raia haweze kujua kuwa eneo lake liko katika eneo hupi hili kuepusha watu kujenga kiholela na mwishowe kukumbana na janga la kuambiwa umejenga eneo la barabara au eneo lisilo sahihi.

Hii itaepusha watu pia kujenga maeneo hatari kama yenye ramani za mito ambayo yako katika hatari ya kukumbwa na natural calamities kama mafuriko na kadharika.

Vilevile huduma nyingine za ardhi ziwekwe katika mfumo wa online ili mtu ajihudumie mwenyewe akiwa mahali halipo kuliko kufunga safari kuja ofisini kwenu.
 
Watu wanajenga kwenye maeneo ya wazi na watu wa mipango wapo tu wanatoa macho kodo

Ova
 
Tatizo ni siasa, tukiweka siasa kando nyumba za wengi zitavunjwa na tutapata maeneo huru mengi
 
Unahoja kubwa sana, usikilizwe. Hii wizara ina migogoro mingi sana miaka nenda miaka rudi kero ni zile zile.

Ukiacha miji iliyoanzishwa na mkoloni ni miji michache sana yenye miundombinu na hadhi ya kuwa sawa na Masaki na Oysterbay. Asilimia kubwa ni ile unakata kiwanja unajijengea halafu ndio unakujq kurasimisha hapo baadae.

Kusolve hili tatizo ni lazima hii wizara ipewe fedha ya kupimq nchi nzima na teknolojia ilivyokuwa kubwa kwa sasa wanaweza kutumia hata drones wakaset mipango inayoweza kuipata online.
 
Back
Top Bottom