Utaratibu ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya sita wa kugawa fedha za miradi ya maendeleo kupitia majimbo ufutwe mara moja

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
16,029
Reaction score
26,231
Kuna utaratibu uliletwa huko Tanzania fedha za miradi ya maendeleo kugawanywa na serikali kupitia majimbo mfano fedha za IMF 1.3 trilion, fedha za Tarura.

Majimbo mengine yanabidadi ndogo ya wakazi, majimbo mengine yako mbele kimaendeleo kuliko mengine, na kutumia mfumu huu usimamizi wa fedha za miradi inasimamiwa kisiasa na wabunge wa majimbo.

Ambapo wizara husika inakuwa observer wa miradi. Mfano Fedha zilizotolewa Tarura kujenga barabara za vijijini, wabunge wamekwenda kwa mameneja wa Tarura na Confidential letter za kuwataka wajenge barabara moja tu kwa kiwango cha lami ili kuja kuonyesha wananchi wakati wa uchaguzi. Mfumo huu ni mfumo usiofaa.

Ninaishauri serikali ya Tanzania kuupokea ushauri alioutoa Spika wa Bunge kuhusu ugawaji wa fedha za miradi ya maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…