Utaratibu mpya wa mahari uboreshwe kuwa hivi

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
9,504
12,176
Mahari imekuwa changamoto kubwa hapa mjini.
Kawaida mahari inatolewa na mume kama shukrani kwa wazazi wa mke kwa kumtunza binti yao hadi kuwa mkeo.
Kipindi hiko unapewa mtoto mbichiii na bikra yake au kama sio bikra basi binti mwenyewe hajachakaa sana.

Ila kwa hali iliyopo sasa vijana wengi tunahisi tunakomolewa, watu tunalipishwa milioni 3, 4, 5 hadi 8, sawa mshahara wa miezi 3 hadi 12 (kutoka a kazi yako) lakini unayemwoa anaweza kuwa na msululu wa ma ex boyfriends wanajaza DCM.
Ukijiangalia wewe ma ex girlfriends zako hata bajaj hawajazi.

Vijana wa sasa wanalipa mahari tu kwa sababu ndio utaratibu tulioukuta na utahitaji kuanzisha familia ila ukweli malalamiko ni mengi.
Huwa tunajiuliza kwanini nilipe mahari ilihali kuna mtu kapita kapewa vyote tena bure na zawadi ya mtoto bure tu, na mtoto analelewa na wazazi wa mwanamke.

Sasa wewe umtokea wapi sijui ukijipeleka kwenda kutoa posa kwa huyo dada unakutana na wajomba wana hasira hao, adhabu za masela wote unapewa wewe utasikia "khanga ya shangazi, blanketi la bibi, jembe la babu, ng'ombe 10, Mbuzi 5, mbege debe 5 n.k, ukipigiwa hesabu milioni 6 hadi 7 huko.

Kwa hali halisi ilivyo sasa ukweli ni kwamba wanaume ndio wanajitunza kuliko wanawake.
Kama bwana harusi ana ma ex girlfriends 5 na bibi harusi ana ma ex boyfriends 10, wanaostahili kupewa shukrani ni wazazi wa mume kwa kumtunza kijana wao.

Kwa maana sasa kuna kampeni ya haki sawa kwa wote utaratibu mpya uwe hivi.

Kati yenu wawili yule mwenye ma ex wengi ndio amlipie mwenzake mahari.

Utaratibu huu ukitumika nadhani wanaume kibao watalipiwa mahari hapa mjini kama wahindi vile wanavyolipiwa mahari na wake zao.

Faida nyingine itapunguza kasi ya kina dada kuachia utamu kirahisi rahisi kwa mtu yeyote yule.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom