CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 686
Kijana mmoja anayesoma katika chuo cha kimoja kilichopo huko maeneo ya Uwanja wa ndege alipata dhahama inayotia uchungu sana maeneo ya Posta.
Mkasa wenyewe ulianza hivi:
Kijana huyo alikuwa anasubiri daladala ili awahi kurudi chuoni maeneo ya posta mpya. Mara akatokea mama mwenye heshima hivi ana mtoto ambaye ana dalili za kuumwa. Akamwomba kijana simu yake ili ampigie mumewe pengine kumweleza mtoto mgonjwa. kijana akasema simu ina shilingi 600, mama akamsisitizia kuwa haitotatosha ila anaomba aweke laini yake ya simu na kijana akakubali. Mama akapokea simu akatoa laini ya kijana akaweka laini yake na kupiga na kisha kumrudishia simu kijana. Kijana hakuangalia kama laini iliyowekwa ni yake au la...... Kosa kubwa!
Mara usafiri wa daladala ukafika kijana akaingia na baada ya kuanza safari abiria mmoja akasikika kaibiwa simu. Kijana aliyekuwa naye, yaonekana ni mwizi mwenziwe, baada ya kutafuta chini ya kiti akashauri wajaribu kuipiga na ndipo simu ya kijana msamaria huyu ikatoa mlio. Wale vijana wakaanza kumpiga kipigo cha mbwa mwizi wakidai kaiba simu na kulazimisha kuichukua kutoka kwa kijana kwa nguvu. Kwa busara za mzee mmoja aliyekuwa ndani ya gari lile walifanikiwa kufika kituo cha polisi na polisi bila kuuliza wala kupokea maelezo ya kijana wakamnyan'ganya kijana simu na kuwapa wale vijana waliodai simu imeibiwa na wakaondoka. Vijana wale walikuwa wakifanya kila wanaloweza kijana yule asijieleze.
Baadaye, ndipo maskini kijana wa watu akaanza kuwaeleza Polisi kilichotokea. Polisi wakabaki mdomo wazi, na kujaribu kutoa maneno ya kuashiria samahani. Lakini tayari alikuwa na majeraha kichwani na simu yake halali kabisa ikiwa imeibwa . . . .