Utapeli wa Mwendokasi

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
21,495
41,919
Hakuna kitu kinakera kwenye Maisha kama Kijana kutumia ujuzi mdogo ulionao kwenye Jambo fulani KUTAPELIII vijana wenzako wanaotafuta pesa zao kwa jasho au pengine kupewa na familia zao..!! Kuna kijana ameweka tangazo kuwa anatoa elimu ya Kuweza kukuza 120000 kwa mwezi izae Mil 100, alafu vijana wachache wasiojielewa wanamsupport utapeli anaofanyaa...!!

Huyu ONTARIO utapeli wa forex haukutosha sasa ameamua aje kutapeli vijana live bila chenga.. Kama una huo ujuzi kwa nini wewe usikuze hiyo 120000 ikazaa mil 100 kuliko kuanza kupambana kushika chaki kufundisha utumbo vijana wa watu??? Kuwa na huruma japo kidogo usitumia kielimu kidogo ulichonacho kuumiza vijana wenzio.

Hakuna mtu with Great Mind na Smart ambae anaishi kwa Utapeli na kuibia watu kisa tu hawana elimu juu ya utapeli wa ainaa hii.

Povu Ruksa.
tapatalk_1572506415550.jpeg
 
Nilivyowahi wahi kusoma nikajua unaongelea kero ya mabasi ya mwendokasi,,, kumbe ONTARIO acha awashikishe adabu sasa tufanyeje
 
Oohhh let me disguise myself so they won't recognize me.

Mmhh beard will do. Definitely will do.

Should I change my name? Of course yes, but I have ego to feed so my real name should be somewhere around... No fvck dat just put it at the top.
 
Sioni tatizo wazee pia sioni kama ni utapeli kulipia 40k kupata mentorship ambayo inaweza ku transform ur mindset katika jambo flan ako jamaa apart from hayo mengine kanayolalamikiwa nayo kana kitu kikubwa sana kana jaribu ku impart kwa jamii yake kana insipire vijana waache ufala wajiamini kwamba wanaweza hio peke yake inatosha sana tatizo la jamii yetu uvumilivu ndio changamoto, hayati Mengi mwenyewe aliandika "i can i must i will" na hakugawa bure
 
Utapeli kamwe hauwezi kuisha...ila kilichobaki unabadilika tu mode za upigaji....
Majuzi tu ..hata mwezi haujapita kuna mpuuzi akaanza kuniambia mambo ya Qnet...nikamuangaliaa alafu nikamuacha kama alivyo...alafu ni bro namweshimu sana..yeye anasema baada ya miezi 6 anaagiza kontena kama 200 kutoka China
 
Mwenye tangazo yuko Sawa unaweza kutoka 120000 kwenda mill 100 Sawa .Gharama ya kozi ni 40000 .Nilianza biashara Kwa 68000 nikaipeleka 950mill .Kwa hiyo sioni cha ajabu hapo
 
Sasa si ufungue darasa... Kama.unapiga mil 950 kwa mwezi hama nchi kabisaa
Hajasema kwa mwezi. We nae umesomea wapi?

Na hata kama atafungua darasa atatofautiana nini na Ontario?? Si ndo watu watakuwa hapa wanasema ni utapeli tu??
 
Wewe nenda sijakukatazaa nawataadharishaa wale wageni ili isije kutokea wameenda wakarudi na Kufungua nyuzi za vilio humuu... Fursa kama wewe nenda tu ukapigwe pesa.
Pamoja Boss Tutaleta Mrejesho Kama Tulivyoleta FX
 
Back
Top Bottom