LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,349
- 36,301
Hii imemtokea ndugu yangu mmoja. Ni hivi mnamo mwezi Machi 2013, zilitangazwa nafasi za kazi kupitia gazeti moja la udaku. Mtangaza nafasi alijitaja kama kampuni inayo jihusisha na INVESTIGATIVE JOURNALISM . Mwombaji nafasi alitakiwa kuwa na shahada ya Journalism/ aliyebobea kwenye mambo ya Investigative Journalism angepewa kipaumbele/ kwa ambao hawajasoma masuala ya journalism lakini wapo interested na nafasi, maombi yao yanakaribishwa, watapewa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwenye hiyo program, ilimradi tu wawe na walau shahada moja... Jamaa akatuma maombi yake, akaitwa kwenye interview, ,walikuwa kama kumi na mbili na waliambiwa wanawagombania nafasi 3 kwa watu wanne. Wiki mbili baadaye alipigiwa simu na kuambiwa ameshinda usaili, so aende ofisini akapewe mkataba wa kazi. Kweli alivyo enda akapewa mkataba, ukasainiwa mbele ya "mwanasheria" feki kwenye ofisi za kampuni hiyo ya kitapeli iliyokuwa maeneo ya Upanga, DSM. Mkataba unaonyesha mshahara utakuwa Milioni 3.8, pamoja na makato mengine, atarudi na take home ya 2.7, vilevile kutakuwa na malipo ya ziada, malipo ya kazi za nje ya Dsm, plus maruurupu and all that.
ALIPIGWAJE HELA?
Alipigwa hela kwenye ishu ya vitendea kazi. Jamaa walimwambia, tunakupa sound recorder yetu ambayo itabidi uinunue kabisa, kwa sababu jinsi ilivyo kuwa designed haitakuwezekana kwa mtu mwingine yoyote yule kuitumia pindi inapokuwa imetumiwa na mtu mwingine tayari. Bei ya SOUND RECORDER ni shilingi Milioni Moja na Laki Tano. Ila ofisi itakudhamini nusu ya gharama. Itakulipia shilingi laki saba na nusu, ambayo utailipa ndani ya miezi mitatu kupitia makato ya kila mwisho wa mwezi kwenye mshahara wako. Wewe utatakiwa kulipa shilingi LAKI SABA NA NUSU. Baada ya kumaliza mkataba wetu wa miaka mitatu, basi utabaki na hiyo PROFFESSIONAL SOUNDRECORDER....
Jamaa akajaa upepo, akatafuta hiyo shilingi LAKI SABA NA NUSU akawapeleke jamaa. Wakampa assignment ya kwenda kufanya upelelezi uchwara, wakamwambia arejeshe ofisini hapo, taarifa za kazi yake baada ya wiki tatu.....
BAADA YA WIKI TATU: Akakuta ofisi zimefungwa, namba zao hazipatakini, kuwauliza majirani wnasema hatuwajui hawa jamaa ila tangu wahamie hapa wana kama mwezi mmoja tu. Alipowapa stori yake, wakamwambia hi ni wiki ya tatu sasa kila siku wanakuja zaidi ya watu kumi hapa kuwaulizia hawa jamaa, sisi tunahisi watakuwa matapeli. Akiwa bado anaongea na wale jamaa, wakajitokeza tena watu wengine wawili ambao nao wamekuwa wahanga wa hao matapeli. Jamaa alichanganyikiwa kabisa, ubishi na ujanja wote kwisha! Baada ya kugundua amepigwa nakumbuka alikuja kunifuata kuniuliza kama najua sehemu anapoweza kukiuza hicho kisound recorder, ( INGAWA HAKUNIAMBIA KAMA AMEPIGWA ) nikamwambia ajaribu kuwapelekea SAPNA wanaweza kuinunua.Yeye alijua labda anaweza kupewa walau laki 4 au tano hivi, jamaa wakamwambia hivyo huwa vinauzwa eLFU SITINI NA TANO! Alichanganyikiwa. Alivyoambiwa amepata kazi alifanya sherehe na kualika ndugu jamaa na marafiki kitaani.. Tukio hilo limemuathiri sana jamaa na limemrudisha nyuma sana.. Anasema kwa alivyo kadiria anadhani wale jamaa watakuwa wamewaliza zaidi ya watu mia tatu.
MY TAKE: UKIKUTANA NA JAMBO KAMA HILI NI VYEMA KUOMBA USHAURI KWA WATU KWANZA KABLA YA KUINGIA KICHWA KICHWA. INAVYO ONEKANA HAO JAMAA NI WAFANYA BIASHARA WA SOUND RECORDERS, PENGINE WALILETA MZIGO UKAWABUMIA WAKAAMUA KUUUZA KWA DESIGN HIYO.