Utapeli wa mabati Buguruni

Utapeli wa mabati Buguruni

ALAF wawe wanatoa matangazo ya maagent wao mara kwa mara ili wale waliowafukuza wasiwe wanatapeli watu. Na hilo la maagent kujazana hapo makao makuu na kusumbua wateja litafutiwe dawa maana mpaka baadhi ya wafanyakazi wanakujengea mazingira magumu huku wanakushawishi wakuunganishe na hao maagent waliopo pale ili mzigo utoke mapema. Lakini kuna haja gani ya kuwa na agent wakati wanaweza kuwa na ofisi ndogo ndogo pamoja na godown dogo kila wilaya kwa ajili ya kupokea oda. Mbona ofisi yao iliyopo JOSAM HOUSE Mwenge ipo vizuri tu japo haina godown. Kwa unayeenda kununua bati pale ofisini ALAF wewe usiwape nafasi maagent wewe komaa kila kitu kiende kiofisi kwa sababu hata ukichelewa bati zako utazipata zikiwa na vipimo sahihi na idadi kamili uliyolipia hata kama zitzachelewa kidogo kupatikana.

Tahadhari nyingine kwa unayetaka kupaua ukiepuka mtego huo hapo juu chunga sana fundi wako anayepaua. Baada ya kupiga mbao zote akifanya mahesabu ya idadi ya bati zinazotakiwa chukua hayo mahesabu kanunue bati zote mwenyewe. Halafu hakikisha unasimamia mwenyewe (ikiwezekana kama ni mfanyakazi omba likizo kabisa) au weka mtu wako unayemwamini asimamie fundi awe anapiga bati moja moja. Kama fundi hana roho ngumu ikifika nusu lazima akimbie kazi maana huchelewi kukuta bado una mzigo wa bati za kutosha hata nyumba mbili. Ukizubaa tu hachelewi kubandika bati mbili mbili pamoja kwa sababu anajua mchezo alioucheza kwenye mahesabu ya ununuzi wa bati. Hapo ndio watu huwa wanashangaa vipi nyumba ndogo tu imepauliwa kwa gharama kubwa au sawa na nyumba nyingie kubwa. Kwa wale mnaojifanya mko bize mnamwachia fundi apime mwenyewe anunue bati mwenyewe apaue mwenyewe mkae mkijua mnapaua nyumba mbili au hata tatu kwa wakati mmoja.
 
Hao watu ni majizi sana, tahadhari kubwa inatakiwa au kwenda na watu wengine wawili wazoefu wa kubaini hiyo michezo
 
Njia nyingine ambayo sijawahi kuielewa mpaka leo ni matumizi ya calculator zao. Kuna siku nimeenda kununua mbao pale buguruni. Kwa kuwa nilikuwa najua mchezo wa futikamba niliwataka wapimie yangu na wakafanya hivyo. Issue ikawa wakati wa kujumlisha mahesabu kwa calculator. Nilishika ile calculator jamaa akawa ananisomea huku nimemweka na jamaa yangu ajiridhishe kama anasoma kilichoandikwa. Tukamaliza na nikalipa na kuondoka.
Baada ya wiki tatu nikarudi tena kununua mbao zingine kwenye duka lilelile. Tukafanya taratibu zote kama awali. This time nilikwenda na jamaa zangu watatu. Moja akawa anaangalia kama kinachosomwa ni kweli, mimi nikawa najumlisha na calculator yao. Jamaa yangu wa tatu kumbe naye akawa anajumlisha kwenye simu yake. Cha ajabu hesabu za kwenye calculator na simu zikawa tofauti. Calculator ikaleta namba kubwa kuliko simu. Ikabidi turudie kwa simu nyingine. Bado hesabu za simu zikaoana. Cha ajabu jamaa akakubali tulipie kutumia hesabu za simu. Nikajua ile calculator imechezewa na mara ya kwanza nilipigwa. Ninachojiuliza mpaka leo ni kuwa calculator inachezewaje?
Usinunue mbao kwa Wakinga ni wachawi sana. Huwezi kuamini lakini ndiyo hivyo
 
Mbao zilizopo Buguruni note hazilingani urefu kwa 100%.Zinatofautiana cm 1 hadi 3 na nyingine ni tofauti ya nusu cm.Sasa futi wanayopimia huwa imekatwa katikati na imeungwa kwa ustadi wa hali ya juu,sio rahisi kupaona,hiyo ni moja watu wanapopigwa.
Pili pale mbao inapopima wanaandika kwenye daftari/diary kila urefu wa mbao,sasa hapo wako fasta sana na anaweza kuzidisha cm 1 au point kadhaa tu kwenye baadhi ya mbao na usishtuke.Hapo tayari umepigwa.
Njia ya tatu ni pale wanapojumlisha urefu wa jumla wa mbao unazochukua,napo wanajumlisha fasta fasta napo unaweza ongezewa point au cm kadhaa kwenye baadhi ya mbao.
Sasa kama umenunua mbao mfano 200 za kenchi au blundering unakuwa umewaachia hela ndefu bila kujua.
Na wanakuwa wengi wale vibarua hivyo kelele zinakuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani kwa elimu umetutoa tongotongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atm uwa inachezewaje
Njia nyingine ambayo sijawahi kuielewa mpaka leo ni matumizi ya calculator zao. Kuna siku nimeenda kununua mbao pale buguruni. Kwa kuwa nilikuwa najua mchezo wa futikamba niliwataka wapimie yangu na wakafanya hivyo. Issue ikawa wakati wa kujumlisha mahesabu kwa calculator. Nilishika ile calculator jamaa akawa ananisomea huku nimemweka na jamaa yangu ajiridhishe kama anasoma kilichoandikwa. Tukamaliza na nikalipa na kuondoka.
Baada ya wiki tatu nikarudi tena kununua mbao zingine kwenye duka lilelile. Tukafanya taratibu zote kama awali. This time nilikwenda na jamaa zangu watatu. Moja akawa anaangalia kama kinachosomwa ni kweli, mimi nikawa najumlisha na calculator yao. Jamaa yangu wa tatu kumbe naye akawa anajumlisha kwenye simu yake. Cha ajabu hesabu za kwenye calculator na simu zikawa tofauti. Calculator ikaleta namba kubwa kuliko simu. Ikabidi turudie kwa simu nyingine. Bado hesabu za simu zikaoana. Cha ajabu jamaa akakubali tulipie kutumia hesabu za simu. Nikajua ile calculator imechezewa na mara ya kwanza nilipigwa. Ninachojiuliza mpaka leo ni kuwa calculator inachezewaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili usiibiwe mbao buguruni ni lazima na wewe uwe mwizi full stop
mimi niliacha kununua vitu vyovyote vya hela nyingi maeneo ya buguruni.Hata pale sokoni kwenye soko la vyakula ogopa sana kusindikizwa na wale vijana wanojifanyaga wanakusaidia kubeba mzigo unapozunguka kufanya shopping.Kuna upigaji wao pia wanafanya kwa ustadi.Yaani kama ulishazungushwa na kijana mle sokoni jua tu kwamba alikupiga
 
Ndugu ukiataka kujua mbao unaibiwaje wewe nenda kanunue mbao pale kwa urefu unaoujua alafu fika nyumbani uzipime tena kama zitakuwa na urefu ule ule.
Kuna mchezo wa kuchezea zile futi kamba wanazotumia kupimia, labda uende na futi kamba yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuliwahi strict mnatuita wagoloka a.k.a mporipori mm huwa simuamini mtu.
 
Mbao zilizowekwa dawa zinauzwa kwa futi hivyo wanachofanya wanakata ile futi kamba katikati alafu wanaunga na gundi hivyo badala ya futi 12 unakuta ni futi 8 hivyo kama umenunua mbao 100 tayari umepigwa ft 400 na kama futi moja ni elf moja tayari umeliwa laki nne.
Kama mjanja ukakagua ile futi kamba yao basi watakuletea nyingine ambayo ipo sahihi lakini watakupiga kwenye kuandika vipimo

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee sasa hivyo vipisi vya mbao wanavyokata wanavifanyia nini!? Au mimi sijaelewa wizi /utapeli wenyewe unavyofanyika!!? Dadavua Mkuu.
 
Back
Top Bottom