Utapeli wa mabati Buguruni

Utapeli wa mabati Buguruni

Eustadius

Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
10
Reaction score
21
Habarini za leo wadau,

Eneo la Buguruni Chama ni eneo ambalo lililozoeleka na umaarufu sana kwa biashara ya mbao pamoja na utapeli kwa wateja wanaofanyiwa katika kununua mbao kwa kutumia ule mchezo wa kupunguza zile futi kamba wakati wa upimaji wa mbao (waliowahi fanyiwa huu mchezo wanajua).

Zaidi ya hapo, kwa sasa kuna makampuni yanayojifanya ni mawakala wa kampuni ya ALAF Tanzania kumbe ni matapeli tu wanaoishia kuchukua hela za watu kwamba watawapatia mabati toka ALAF na mwishowe kuishia kuwazungusha wananchi hao.

Mimi mwenyewe imenitokea kusumbuliwa na hao matapeli wanaojiita dealers wa ALAF kumbe sio na kibaya zaidi nilielekezwa kwa huyo anayejiita wakala wa ALAF na mtu ambaye tunaheshimiana SANA. Kumbe uwakala wake umeishasimamishwa na amebaki mjini kusumbua na kutapeli watu. Hivi ninavyo andika ujumbe huu tapeli huyo yupo ndani katika Kituo cha Polisi Buguruni na maneno anayoongea muda huu hayaeleweki kabisa kuhusiana na mzigo wangu.

#mytake
1.Nawashauri endapo unahitaji bati kutoka ALAF ni bora kwenda kiwandani moja kwa moja maana haizuiliwi kabisa unakwenda unatoa order yako na kupatiwa bidhaa yako ndani ya muda mfupi sana kuliko kuendelea kusumbuka na hawa matapeli.
Hili nimeligundua baada ya kwenda kulalamika na kuwaeleza kuhusiana na maneno aliyokuwa ananiambia huyo aliyekuwa anajiita wakala kumbe sio.
Tuchukue tahadhari katika hili.

2. Kampuni ya ALAF ifanye chapisho kuwabainisha mawakala wao wote na kuwabainisha wote ambao ni matapeli wanaotumia jina lao kwani wanawajua na hizo kesi zinakwenda kwao kila leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njoooni ALAF maitishwe kwamba bei ni kubwa waongo bei niza kawaida kabisa halafu unapata bati nzuri zisizokuwa na mashaka yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbao unaibiwaje wakati mbao urefu wake unajulikana? Kuanzia huko zitokapo mbao huwezi ipunguza sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu ukiataka kujua mbao unaibiwaje wewe nenda kanunue mbao pale kwa urefu unaoujua alafu fika nyumbani uzipime tena kama zitakuwa na urefu ule ule.
Kuna mchezo wa kuchezea zile futi kamba wanazotumia kupimia, labda uende na futi kamba yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njoooni ALAF maitishwe kwamba bei ni kubwa waongo bei niza kawaida kabisa halafu unapata bati nzuri zisizokuwa na mashaka yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli, hata hao mawakala wa ALAF wanajifanya mkinunia kwao ndio kuna discount lakini sio kweli. Hiyo. Ni lugha ya biashara tu.., unakuta kule wakala anapewa discount ya 15% ila yeye anakupa discount ya 5% pekee. Ni bora kwenda kiwandani moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za leo wadau,

Eneo la Buguruni Chama ni eneo ambalo lililozoeleka na umaarufu sana kwa biashara ya mbao pamoja na utapeli kwa wateja wanaofanyiwa katika kununua mbao kwa kutumia ule mchezo wa kupunguza zile futi kamba wakati wa upimaji wa mbao (waliowahi fanyiwa huu mchezo wanajua).

Zaidi ya hapo, kwa sasa kuna makampuni yanayojifanya ni mawakala wa kampuni ya ALAF Tanzania kumbe ni matapeli tu wanaoishia kuchukua hela za watu kwamba watawapatia mabati toka ALAF na mwishowe kuishia kuwazungusha wananchi hao.

Mimi mwenyewe imenitokea kusumbuliwa na hao matapeli wanaojiita dealers wa ALAF kumbe sio na kibaya zaidi nilielekezwa kwa huyo anayejiita wakala wa ALAF na mtu ambaye tunaheshimiana SANA. Kumbe uwakala wake umeishasimamishwa na amebaki mjini kusumbua na kutapeli watu. Hivi ninavyo andika ujumbe huu tapeli huyo yupo ndani katika Kituo cha Polisi Buguruni na maneno anayoongea muda huu hayaeleweki kabisa kuhusiana na mzigo wangu.

#mytake
1.Nawashauri endapo unahitaji bati kutoka ALAF ni bora kwenda kiwandani moja kwa moja maana haizuiliwi kabisa unakwenda unatoa order yako na kupatiwa bidhaa yako ndani ya muda mfupi sana kuliko kuendelea kusumbuka na hawa matapeli.
Hili nimeligundua baada ya kwenda kulalamika na kuwaeleza kuhusiana na maneno aliyokuwa ananiambia huyo aliyekuwa anajiita wakala kumbe sio.
Tuchukue tahadhari katika hili.

2. Kampuni ya ALAF ifanye chapisho kuwabainisha mawakala wao wote na kuwabainisha wote ambao ni matapeli wanaotumia jina lao kwani wanawajua na hizo kesi zinakwenda kwao kila leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu, hawa mawakala siyo wa kuwaamini maana mwisho wa siku lazima akufaidi wewe, hakuna msaada wa bure! alafu mbona huo wizi wa kizamani sana bado wanauendeleza..
 
Mbao unaibiwaje wakati mbao urefu wake unajulikana? Kuanzia huko zitokapo mbao huwezi ipunguza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanachofanya mfano mbao ni futi 10 , wao wanakata futi yao katikati wanaondoa kipande kama futi 2 au 2.5 alafu wanaiunganisha tena ile futi, kwa hiyo mwisho wa siku wakikupimia kweli futi itasoma futi kumi lakini uhalisia mbao yako ni futi 8 au 7.5 .

Cha kufanya usiamini vipimio vya madukani au kwenye hardware badala yake fika na futi yako waambie unataka uitumie yako, ukiona wanaleta ubishani jua futi zao zina walakini
 
ALAF wenyewe ni sehemu ya kulaumiwa kwa sababu nao wanawalea sana hao madalali pengine kutokana na maslahi fulani wanayopata baadhi ya management staff wa pale. Ukifika pale kiwandani ALAF utashangaa kuwaona madalali wamejazana getini na pia pale ndani mapokezi ili kuwarubuni wateja wageni wanunue mabati kupitia kwao kwa kisingizio kuwa wao wanaponunua wanapata discount. Serikali inapaswa kukomesha utapeli huu kwa kuzingatia kwamba nayo ina hisa kubwa katika kampuni hiyo.
 
Mbao zinauzwa kwa ft. Sasa mijamaa unakuta inafuti za kamba zilizopunguzwa huko kwenye shina letsay cm30!

Wewe pale unafika na haraka zako na macho yako maoga.

Ubao wa ft 11 unauziwa thamani ya ubao wenye ft12.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbao zilizowekwa dawa zinauzwa kwa futi hivyo wanachofanya wanakata ile futi kamba katikati alafu wanaunga na gundi hivyo badala ya futi 12 unakuta ni futi 8 hivyo kama umenunua mbao 100 tayari umepigwa ft 400 na kama futi moja ni elf moja tayari umeliwa laki nne.
Kama mjanja ukakagua ile futi kamba yao basi watakuletea nyingine ambayo ipo sahihi lakini watakupiga kwenye kuandika vipimo
Mbao unaibiwaje wakati mbao urefu wake unajulikana? Kuanzia huko zitokapo mbao huwezi ipunguza sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbao unaibiwaje wakati mbao urefu wake unajulikana? Kuanzia huko zitokapo mbao huwezi ipunguza sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanafanya wizi kwa njia kama 4. 1)wametengeneza futi kamba zao ambazo ni fupi kuliko kawaida na ndo wanatumia. Ukipima ubao unapata 14ft kumbe ni 12ft. 2)wanapima ubao mmoja mmoja na wakati wa kujumlisha wanafanya figisu figisu, ukiwamini inakula kwako. 3) wakati wa kuhesabu zile mbao zenyewe wanakupiga pia. 4)wakati wa kipakia wanakupiga ukizubaha. Yaani pale ni majanga tupu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
ALAF wenyewe ni sehemu ya kulaumiwa kwa sababu nao wanawalea sana hao madalali pengine kutokana na maslahi fulani wanayopata baadhi ya management staff wa pale. Ukifika pale kiwandani ALAF utashangaa kuwaona madalali wamejazana getini na pia pale ndani mapokezi ili kuwarubuni wateja wageni wanunue mabati kupitia kwao kwa kisingizio kuwa wao wanaponunua wanapata discount. Serikali inapaswa kukomesha utapeli huu kwa kuzingatia kwamba nayo ina hisa kubwa katika kampuni hiyo.

Unalosema ni kweli kabisa. Ukifika pale ndani unawakuta hao madalali na reflector zao nyekundu.., inakera sana. Ila ndio tunajifunza kutokana na makosa. Next time ni straight kiwandani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafanya wizi kwa njia kama 4. 1)wametengeneza futi kamba zao ambazo ni fupi kuliko kawaida na ndo wanatumia. Ukipima ubao unapata 14ft kumbe ni 12ft. 2)wanapima ubao mmoja mmoja na wakati wa kujumlisha wanafanya figisu figisu, ukiwamini inakula kwako. 3) wakati wa kuhesabu zile mbao zenyewe wanakupiga pia. 4)wakati wa kipakia wanakupiga ukizubaha. Yaani pale ni majanga tupu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Njia nyingine ambayo sijawahi kuielewa mpaka leo ni matumizi ya calculator zao. Kuna siku nimeenda kununua mbao pale buguruni. Kwa kuwa nilikuwa najua mchezo wa futikamba niliwataka wapimie yangu na wakafanya hivyo. Issue ikawa wakati wa kujumlisha mahesabu kwa calculator. Nilishika ile calculator jamaa akawa ananisomea huku nimemweka na jamaa yangu ajiridhishe kama anasoma kilichoandikwa. Tukamaliza na nikalipa na kuondoka.
Baada ya wiki tatu nikarudi tena kununua mbao zingine kwenye duka lilelile. Tukafanya taratibu zote kama awali. This time nilikwenda na jamaa zangu watatu. Moja akawa anaangalia kama kinachosomwa ni kweli, mimi nikawa najumlisha na calculator yao. Jamaa yangu wa tatu kumbe naye akawa anajumlisha kwenye simu yake. Cha ajabu hesabu za kwenye calculator na simu zikawa tofauti. Calculator ikaleta namba kubwa kuliko simu. Ikabidi turudie kwa simu nyingine. Bado hesabu za simu zikaoana. Cha ajabu jamaa akakubali tulipie kutumia hesabu za simu. Nikajua ile calculator imechezewa na mara ya kwanza nilipigwa. Ninachojiuliza mpaka leo ni kuwa calculator inachezewaje?
 
Mbao unaibiwaje wakati mbao urefu wake unajulikana? Kuanzia huko zitokapo mbao huwezi ipunguza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbao zilizopo Buguruni note hazilingani urefu kwa 100%.Zinatofautiana cm 1 hadi 3 na nyingine ni tofauti ya nusu cm.Sasa futi wanayopimia huwa imekatwa katikati na imeungwa kwa ustadi wa hali ya juu,sio rahisi kupaona,hiyo ni moja watu wanapopigwa.
Pili pale mbao inapopima wanaandika kwenye daftari/diary kila urefu wa mbao,sasa hapo wako fasta sana na anaweza kuzidisha cm 1 au point kadhaa tu kwenye baadhi ya mbao na usishtuke.Hapo tayari umepigwa.
Njia ya tatu ni pale wanapojumlisha urefu wa jumla wa mbao unazochukua,napo wanajumlisha fasta fasta napo unaweza ongezewa point au cm kadhaa kwenye baadhi ya mbao.
Sasa kama umenunua mbao mfano 200 za kenchi au blundering unakuwa umewaachia hela ndefu bila kujua.
Na wanakuwa wengi wale vibarua hivyo kelele zinakuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za leo wadau,

Eneo la Buguruni Chama ni eneo ambalo lililozoeleka na umaarufu sana kwa biashara ya mbao pamoja na utapeli kwa wateja wanaofanyiwa katika kununua mbao kwa kutumia ule mchezo wa kupunguza zile futi kamba wakati wa upimaji wa mbao (waliowahi fanyiwa huu mchezo wanajua).

Zaidi ya hapo, kwa sasa kuna makampuni yanayojifanya ni mawakala wa kampuni ya ALAF Tanzania kumbe ni matapeli tu wanaoishia kuchukua hela za watu kwamba watawapatia mabati toka ALAF na mwishowe kuishia kuwazungusha wananchi hao.

Mimi mwenyewe imenitokea kusumbuliwa na hao matapeli wanaojiita dealers wa ALAF kumbe sio na kibaya zaidi nilielekezwa kwa huyo anayejiita wakala wa ALAF na mtu ambaye tunaheshimiana SANA. Kumbe uwakala wake umeishasimamishwa na amebaki mjini kusumbua na kutapeli watu. Hivi ninavyo andika ujumbe huu tapeli huyo yupo ndani katika Kituo cha Polisi Buguruni na maneno anayoongea muda huu hayaeleweki kabisa kuhusiana na mzigo wangu.

#mytake
1.Nawashauri endapo unahitaji bati kutoka ALAF ni bora kwenda kiwandani moja kwa moja maana haizuiliwi kabisa unakwenda unatoa order yako na kupatiwa bidhaa yako ndani ya muda mfupi sana kuliko kuendelea kusumbuka na hawa matapeli.
Hili nimeligundua baada ya kwenda kulalamika na kuwaeleza kuhusiana na maneno aliyokuwa ananiambia huyo aliyekuwa anajiita wakala kumbe sio.
Tuchukue tahadhari katika hili.

2. Kampuni ya ALAF ifanye chapisho kuwabainisha mawakala wao wote na kuwabainisha wote ambao ni matapeli wanaotumia jina lao kwani wanawajua na hizo kesi zinakwenda kwao kila leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo dar kuna ALAF roof Galleries nyingi tu. Zote zinamilikiwa na kiwanda. Mfano: Mwenge pale JOSAM house.

Hao makanjanja wa buguruni & co achaneni nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakikukosa kwenye futi, unapigwa kwenye calculator, kuna mbinu nyingi sana pale

Back
Top Bottom