Utapeli wa chuo kikuu cha dar -es salaam {udsm}

kibwengomwitu

Member
Dec 19, 2011
6
0
Habari wana JF UDSM kumekua na utapeli ambao unaendelea, miaka miwili iliyopita UDSM kupitia tawi lake la COET limetangaza kuanzisha kozi ya Record and Archives Management chini ya tapeli mkuu Mr Fredi Kabori ambae ndio cordinator mwenye shahada ya uhandisi,wanafunzi wengi sana walijiunga kutoka Magogoni Chuo cha utumishi kwa kufuata jina la chuo kikuu cha Dar es Salaam na kutambulika kwake na wengine wale waliomaliza IV, wakiamini wakimaliza wakimaliza chuoni hapo itakua ni rahisi kupata kazi,maskini kumbe sio hivyo,Mr Fred kabori alipanga utapeli wake vizuri sana kwa kuweka nembo ya UDSM juu ya fomu za maombi kwa kuwahadaa watu.Ukweli uliopo ni huu Mr kabori ameanzisha ile kozi yeye mwenyewe tena hajaisajili popote anawaibia watu hivi hivi waliomaliza mwaka jana mpaka sasa hawajapata vyeti vyao wachache waliopata wamepewa havina nembo ya UDSM lakini bado anaendelea kuwatapeli watu maana bado wanafunzi wanajiunga kwa kutokujua madarasa yenyewe ya kusomea wamefukuzwa pale COET Fred kawapeleka Sinza kawakodia jengo kafanya madarasa nawasikitikia wazazi waliolipa ada zao kumbe wanamtajirisha mtu burebure pia nawashauri kwa wale wenye malengo ya kwenda kujiunga wasiende ukitaka ukweli nenda kafuatilie hatua kwa hatua utajua.Lakini naulaumu sana uongozi wa UDSM kwa kuliona hili na kulifumbia macho na kuwaacha wananchi wakiibiwa tena kupitia jina la chuo hicho,pia nailaumu serikali kwa kuzifumbia macho kesi hizi za vyuo kutosajiliwa na kutoa huduma kwa udanganyifu sio mpaka kila kitu wanafunzi waandamane au kama mmezoea hivyo sawa lakini kama chuo kikuu kinafanya utapeli wa elimu tukimbilie wapi sasa na siamini hata kidogo kama eti hakuna mkono wa kigogo kwenye hili jamani waandishi wa habari tusaidieni wa TZ tunaibiwa hukutunaona naomba mwende kwa uongozi wa chuo mukalifuatilie hili.kwa upande wa serikali sijui muhusika wa kulichukulia hatua ni nani Wizara ya elimu au sijui nani hata Takukuru pia kama mnahusika basi kamchukulieni hatua huyu mtu keshakula pesa nyingi na bado anaendelea kula mwanafunzi mmoja certificate ni laki tisa na diploma millioni moja laki tano anawanafunzi zaidi ya mia nane sasa na wanazidi kwennda inaniuma sana mtu msomi aliyesomeshwa na kodi ya serikali badala ya kusaidia jamii upande wa elimu anakua tapeli upande wa elimu na chuo kikuu kinamtizama tu na kinamlipa mshahara kodi za wanachi hii hapana wana JF kama yupo anaeweza kukemea hili mchango wako unahitajika please.
 
Keli hili si la kufumbia macho, ikizingatia wazazi wengi wanapopeleka watoto wao huenda kutokana na hadhi ua UDSM.
Nakumbuka kuna jamaa flani walikuwa pia wanafanya workshop flan za mambo ya Research then ukitaka cheti unalipa, so watu wengi walilipa hata bila kuhudhuria na kupata vyeti hivyo japo siamini kama vinawasaidia sana maana kama kozi hukuisoma then unacheti ni tatizo
 
Kwahiyo mnataka cheti cha Mlimani sio!. Poleni sana.
 
Inabidi u-edit heading yako isomeke 'Utapeli wa Mr. Fred Kabori'..

Mmedandia treni kwa mbele nyie wenyewe (based on your own description).
 
kazi ipo, hii nchi inakosa ungalizi kkisi kwamba mtu unajiamulia kufanya maamuzi ambayo yanaathiri maisha ya mtu moja kwa moja na hakuna anasema kitu?
nafikiri kuna haja ya haya mambo kuangaliwa vema na vyombo husika..
 
Inabidi u-edit heading yako isomeke 'Utapeli wa Mr. Fred Kabori'..

Mmedandia treni kwa mbele nyie wenyewe (based on your own description).

Muanzisha thread naye ni sawa na Fred Kabori katutapeli wasomaji thread kwa kuipa wrong title makusudi mazima ili atuvute kuisoma.
 
Habari wana JF UDSM kumekua na utapeli ambao unaendelea, miaka miwili iliyopita UDSM kupitia tawi lake la COET limetangaza kuanzisha kozi ya Record and Archives Management chini ya tapeli mkuu Mr Fredi Kabori ambae ndio cordinator mwenye shahada ya uhandisi,wanafunzi wengi sana walijiunga kutoka Magogoni Chuo cha utumishi kwa kufuata jina la chuo kikuu cha Dar es Salaam na kutambulika kwake na wengine wale waliomaliza IV, wakiamini wakimaliza wakimaliza chuoni hapo itakua ni rahisi kupata kazi,maskini kumbe sio hivyo,

Mr Fred kabori alipanga utapeli wake vizuri sana kwa kuweka nembo ya UDSM juu ya fomu za maombi kwa kuwahadaa watu.Ukweli uliopo ni huu Mr kabori ameanzisha ile kozi yeye mwenyewe tena hajaisajili popote anawaibia watu hivi hivi waliomaliza mwaka jana mpaka sasa hawajapata vyeti vyao wachache waliopata wamepewa havina nembo ya UDSM lakini bado anaendelea kuwatapeli watu maana bado wanafunzi wanajiunga kwa kutokujua madarasa yenyewe ya kusomea wamefukuzwa pale COET Fred kawapeleka Sinza kawakodia jengo kafanya madarasa

nawasikitikia wazazi waliolipa ada zao kumbe wanamtajirisha mtu burebure pia nawashauri kwa wale wenye malengo ya kwenda kujiunga wasiende ukitaka ukweli nenda kafuatilie hatua kwa hatua utajua.Lakini naulaumu sana uongozi wa UDSM kwa kuliona hili na kulifumbia macho na kuwaacha wananchi wakiibiwa tena kupitia jina la chuo hicho,pia nailaumu serikali kwa kuzifumbia macho kesi hizi za vyuo kutosajiliwa na kutoa huduma kwa udanganyifu sio mpaka kila kitu wanafunzi waandamane au kama mmezoea hivyo sawa lakini kama chuo kikuu kinafanya utapeli wa elimu tukimbilie wapi sasa na siamini hata kidogo kama eti hakuna mkono wa kigogo kwenye hili jamani

waandishi wa habari tusaidieni wa TZ tunaibiwa hukutunaona naomba mwende kwa uongozi wa chuo mukalifuatilie hili.kwa upande wa serikali sijui muhusika wa kulichukulia hatua ni nani Wizara ya elimu au sijui nani hata Takukuru pia kama mnahusika basi kamchukulieni hatua huyu mtu keshakula pesa nyingi na bado anaendelea kula mwanafunzi mmoja certificate ni laki tisa na diploma millioni moja laki tano anawanafunzi zaidi ya mia nane sasa na wanazidi kwennda inaniuma sana mtu msomi aliyesomeshwa na kodi ya serikali badala ya kusaidia jamii upande wa elimu anakua tapeli upande wa elimu na chuo kikuu kinamtizama tu na kinamlipa mshahara kodi za wanachi hii hapana wana JF kama yupo anaeweza kukemea hili mchango wako unahitajika please.

ngoja nijaribu tena kusoma labda nitaelewa
 
Unamshutumu huyo Fred kwa kutumia jina la UDSM kuvuta watu, lakini pia na wewe unaandika title ya thread hii ukitumia jina la UDSM kuvuta wachangiaji. Wewe na Fred wote wawili ni matapeli.
 
Inabidi u-edit heading yako isomeke 'Utapeli wa Mr. Fred Kabori'..

Mmedandia treni kwa mbele nyie wenyewe (based on your own description).

Mkuu kama UDSM siyo sehem ya utapeli huo wasingelifumbia macho bali wangepingana nalo kwa kila njia
 
kazi ipo, hii nchi inakosa ungalizi kkisi kwamba mtu unajiamulia kufanya maamuzi ambayo yanaathiri maisha ya mtu moja kwa moja na hakuna anasema kitu?
nafikiri kuna haja ya haya mambo kuangaliwa vema na vyombo husika..

Serikali yetu ya chochotd kitu inajua kuangalia baada ya chochote kitu? Mungu ndiye atakaetunusuru waTz tusiojua kupigania haki zetu
 
Muanzisha thread naye ni sawa na Fred Kabori katutapeli wasomaji thread kwa kuipa wrong title makusudi mazima ili atuvute kuisoma.

Acha ubogiaz wewe unafikiri mtu utakamilika kwote, ushamwonyesha alipokosea atajirekebisha next time sio kufananisha mbwa na mbuzi ukiwa umemshikilia mbuzi pembe
 
Unamshutumu huyo Fred kwa kutumia jina la UDSM kuvuta watu, lakini pia na wewe unaandika title ya thread hii ukitumia jina la UDSM kuvuta wachangiaji. Wewe na Fred wote wawili ni matapeli.

Kumwelimisha mpumbavu ni kazi kweli! Labda ungekuwa mjinga tungejaribu na tungeweza pole sana
 
Sasa watz watakimbilia wapi? Kama kwenye elimu serikali imewekeza matapeli mikataba ya madini na rasilimali zetu wamewawekezea mafisadi, wamewafanya wenye shell za mafuta kuwa juu ya serikali mwisho wake tutajakuwa watumwa kwenye nchi yetu tuliyozaliwa
 
Mr nawe ni mmoja wao nini au ndugu yako maana sikuelewi Fred kaajiriwa na nani COET ipo chini ya UDSM nae ndipo anapofanyia kazi pia fomu za kujiunga zina title ya UDSM na nembo yao kama sio utapeli wa Udsm kwanini wasimkataze kutumia ofisi na jina la Udsm kwa utapeli huu.acha mambo yako kua mzalendo.
 
We kweli ni kipofu aliyetapeli kuvutia wasomaji na wachangiaji ili aokoe pesa za watanzania wengine na aliyevutia wanafunzi ili wakose elimu na yeye apate pesa kwa utapeli bora yeye kweli sisi wa tz tumerogwa.
 
kazi ipo, hii nchi inakosa ungalizi kkisi kwamba mtu unajiamulia kufanya maamuzi ambayo yanaathiri maisha ya mtu moja kwa moja na hakuna anasema kitu?
nafikiri kuna haja ya haya mambo kuangaliwa vema na vyombo husika..

hii sio TZ tu mkuu, wale mafisadi wa elimu akina Lukuvi si wamesoma kwenye vyuo ambavyo havitambuliwi huko Ughaibuni? Na bado vinatoa huduma. Tatizo letu wtz tunapenda lawama! Wewe angalia tunavyotupa taka taka zinazoziba mifereji ya maji, leo tunapatwa na mafuriko kwa mifereji kuziba kwa taka ngumu tulizozitupa kwa mikono yetu, tunailaumu serikali!
 
Back
Top Bottom