kibwengomwitu
Member
- Dec 19, 2011
- 6
- 0
Habari wana JF UDSM kumekua na utapeli ambao unaendelea, miaka miwili iliyopita UDSM kupitia tawi lake la COET limetangaza kuanzisha kozi ya Record and Archives Management chini ya tapeli mkuu Mr Fredi Kabori ambae ndio cordinator mwenye shahada ya uhandisi,wanafunzi wengi sana walijiunga kutoka Magogoni Chuo cha utumishi kwa kufuata jina la chuo kikuu cha Dar es Salaam na kutambulika kwake na wengine wale waliomaliza IV, wakiamini wakimaliza wakimaliza chuoni hapo itakua ni rahisi kupata kazi,maskini kumbe sio hivyo,Mr Fred kabori alipanga utapeli wake vizuri sana kwa kuweka nembo ya UDSM juu ya fomu za maombi kwa kuwahadaa watu.Ukweli uliopo ni huu Mr kabori ameanzisha ile kozi yeye mwenyewe tena hajaisajili popote anawaibia watu hivi hivi waliomaliza mwaka jana mpaka sasa hawajapata vyeti vyao wachache waliopata wamepewa havina nembo ya UDSM lakini bado anaendelea kuwatapeli watu maana bado wanafunzi wanajiunga kwa kutokujua madarasa yenyewe ya kusomea wamefukuzwa pale COET Fred kawapeleka Sinza kawakodia jengo kafanya madarasa nawasikitikia wazazi waliolipa ada zao kumbe wanamtajirisha mtu burebure pia nawashauri kwa wale wenye malengo ya kwenda kujiunga wasiende ukitaka ukweli nenda kafuatilie hatua kwa hatua utajua.Lakini naulaumu sana uongozi wa UDSM kwa kuliona hili na kulifumbia macho na kuwaacha wananchi wakiibiwa tena kupitia jina la chuo hicho,pia nailaumu serikali kwa kuzifumbia macho kesi hizi za vyuo kutosajiliwa na kutoa huduma kwa udanganyifu sio mpaka kila kitu wanafunzi waandamane au kama mmezoea hivyo sawa lakini kama chuo kikuu kinafanya utapeli wa elimu tukimbilie wapi sasa na siamini hata kidogo kama eti hakuna mkono wa kigogo kwenye hili jamani waandishi wa habari tusaidieni wa TZ tunaibiwa hukutunaona naomba mwende kwa uongozi wa chuo mukalifuatilie hili.kwa upande wa serikali sijui muhusika wa kulichukulia hatua ni nani Wizara ya elimu au sijui nani hata Takukuru pia kama mnahusika basi kamchukulieni hatua huyu mtu keshakula pesa nyingi na bado anaendelea kula mwanafunzi mmoja certificate ni laki tisa na diploma millioni moja laki tano anawanafunzi zaidi ya mia nane sasa na wanazidi kwennda inaniuma sana mtu msomi aliyesomeshwa na kodi ya serikali badala ya kusaidia jamii upande wa elimu anakua tapeli upande wa elimu na chuo kikuu kinamtizama tu na kinamlipa mshahara kodi za wanachi hii hapana wana JF kama yupo anaeweza kukemea hili mchango wako unahitajika please.