MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,768
Serikali kupitia waziri wake anayehusika na masula ya afya Dr ndugulile imewafumbua macho watanzania tanzania wengi wanaokwenda kwenye mahospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya U.T.I na homa za matumbo (typhod)
Inaelezwa kitaalam kwamba vipimo vya magonjwa haya huchukua muda wa masaa mawili (2) hadi sabini na mbili (72) ili kupata majibu yaliyo sahihi na sio vinginevyo
Taarifa hii imekuja kuwafumbua macho wananchi ambao kwa kiasi kikubwa tumekua "tunapigwa" kwa kupatiwa majibu ya maradhi haya sugu na hatari kwa muda usiozidi hata nusu saa!
Hali hii ikiachwa iendelee hivyo itapelekea watu wasio na maradhi kutumia dawa wakidhani wana maradhi (medicalization)
Au itawezakufanya watu walio na maradhi haya kutokupewa dawa zozote kwani huenda kwa muda huo mfupi maradhi hayataweza kudhihirika
Kwa maoni yangu serikali itupie macho pia mahospitali ya binafsi ambayo mengi yao si waaminifu kwani wengi hujisahau na kujikita zaidi kwenye biashara na si kutoa huduma
Imekua ni kawaida kila ukienda baadhi ya mahospitali haya ya binafsi ni lazima ukutwe na ugonjwa flani hasa U.T.I na malaria ili waweze kuuza na kumaliza stock zao za dawa walizojaza kwenye pharmacy zao
Pengine watakuambia macho yako yameharibika kabisa ili wakuuzie miwani kwa 150000/- , huu ni upigaji
Chanzo: gazeti la mtanzania
tar 19/5/2019