Utapeli!utapeli!

Utapeli!utapeli!

Pole sana mkuu mwambie dogo awe kama mimi nisiye mwamini mtu yeyote zaidi ya M ungu.... kwa hiyo dogo ukqmfanyaje?

Nimeshapoa kiongozi;ss ningemfanyaje wkt watu wameshashukua mzigo?nilimpa tu warning na kuwa muangalifu zaidi
 
Kwa kisa hiki aliyelizwa ni wewe haswa. Tena aliyekuliza ni huyo dogo unayemuamini hapo dukani kwako. Hebu mbane vizuri atakueleza nini amafanya!!!

Nina hakika walimtapeli baada ya kujiridhisha na uchunguzi
 
Ndugu wana Jf,
Wasalaam!
Wiki mbili zilizopita kuna wateja wawili (mbongo na mzungu) walikuja dukani kwangu mda wa saa mbili na nusu usiku.Wakiwa ndani walivutiwa na microwave na Oven zilizokuwepo dukani.Wakakubaliana bei na dogo aliyekuwepo dukani siku hiyo zote kwa pamoja Tsh 560,000.
Wkt wote wa majadiliano kati ya dogo na mbongo yule mzungu alikuwa anajifanya ana haraka sna na alimtaka jamaa yke aliyefuatana nae amalizane na dogo yy alipe waondoke.
Mbongo akamwambia dogo bei waliyokubaliana afanye Tsh 600,000 kisha amtumie pesa iliyozidi kwa mpesa.
Baada ya mzungu kuambiwa bei akasema atalipa kwa foreign currency [€] coz hakuwa na Tsh.
Baada ya dogo kucheck ex rate akalipwa €300 jamaa wakachukua mzigo wao wakasepa hata risiti walikataa.
Dogo aliponiletea hesabu ya siku na kushika zile foregn currency mara moja nilitambua ni FEKI,hata baada ya kuzihakiki tena kwenye machine kesho yke zilitemwa nikajua tayari nimeshapigwa.

Angalizo:
Sio kila mtu anayekuja dukani/kwenye biashara yko ni raia mwema.Wengine ni matapeli tu haijalishi kama ni mzungu,mchina,mbongo e.t.c.nawasihi muwe waangalifu msije pigwa kama mm.

Mkuu, haujafunga cctv dukani kwako, angalau tungewaona sura huenda tunawafahamu!
Inabidi tuongee nije nikufungie mkuu, dunia ya sasa haiko salama kabisaa, unajua mtu akiingia kwako akaona camera kwenye corner kidogo anajistukia!
 
Kwa kisa hiki aliyelizwa ni wewe haswa. Tena aliyekuliza ni huyo dogo unayemuamini hapo dukani kwako. Hebu mbane vizuri atakueleza nini amafanya!!!

Hahaha, usimchongee dogo bana, ametapeliwa ametapeliwa tu kaka, wala tusimlaum dogo! Kwa akili ya harakaharaka dogo aliona amepiga biashara, na alijua brother akija atafurahi tu kuwa amejiongeza hakukataa pesa ya kigeni, tena kakokotoa vizuri kabisa na exchange rate, ndiyo kujifunza kwenyewe huko, hapo inabidi jamaa amfundishe dogo jinsi ya kutambua noti fake, dola, yuro, na pesa zingine maarufu, tofauti na hapo awaambie wakabadilishe wamletee madafu!
 
hata hizo dola zingekuwa si feki,bado ulishapata hasara,cause dola 300 ni tsh 480,000.
 
Mkuu, haujafunga cctv dukani kwako, angalau tungewaona sura huenda tunawafahamu!
Inabidi tuongee nije nikufungie mkuu, dunia ya sasa haiko salama kabisaa, unajua mtu akiingia kwako akaona camera kwenye corner kidogo anajistukia!

Sijafunga mkuu,inabidi nifanye hivyo nitakutafuta ni pm mobile no yko
 
sorry nimejichanganya,ni ya Usa.

Acha Porojo za NDEZI, Mwenzako amesema Euro. Tokea lini $300 ikawa equivalent na laki6!?

Ila tunashukuru kwa Taarifa Mkuu, Umetuweka Makini sana. Ila mtiririko wa hadith yako inatia wasiwasi,kwani hao matapeli hasa huyo Mbongo,aliweka wazi kuwa apandishe bei ili kuwa Kilo6 ili nyongeza amtumie. Mbona dogo hakuulizia chanzo/njia ya yy kumtumia chake cha juu!? Au naye dogo alipagawa hakuwahi kuuza hesabu kubwa namna hiyo!? Sababu hilo tapeli la kibongo liliweka wazi kuwa wamuumize hilo njemba la kidhungu then kile cha juu atumiwe. Angemtumia kwa njia gani kama sio Simu!????
 
Kwanza kabisa mbongo alijifanya kama vile ni dereva taxi wa huyo mzungu kumbe lao moja.Alimpatia Dogo mobile number zke wakati anaondoka waweze kuwasiliana amtumie chake lkn baadae akawa hapatikani.
 
hizi story za wazungu kutapeli watu kwa noti feki naona zipo nyingi.na wengi wao husema hivyo hivyo hawana tz money,muwe makini kuwaelimisha wafanyakazi wenu.kuna mmoja alihojiwa alisema yeye alitapeliwa baa,na mara nyingi huwa wanajifanya wana haraka,na hutoa noti ya mfano dollar mia au euro 50 ili wapate change hata ya tz money.kuna mwengine alitapeli dukani alienda kununua kitu,kwa maneno hayohayo ya kuwa hana tz money.
 
Mkuu, haujafunga cctv dukani kwako, angalau tungewaona sura huenda tunawafahamu!
Inabidi tuongee nije nikufungie mkuu, dunia ya sasa haiko salama kabisaa, unajua mtu akiingia kwako akaona camera kwenye corner kidogo anajistukia!

Dah umeona gap ha ha haaa huo ndio ujasiliamali bana
 
da hizo euro ziko za kumwaga mpaka zikija kwisha watalia wengi,kuweni makini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom