Utapeli, utapeli AIRTEL TL,

laurent Msembeyu

Senior Member
Oct 5, 2015
121
101
Nimepata ujumbe mfupi toka no 0786963511 ukiniarifu kwa Kiswahili kibovu " Imethibitishwa umepokeaTsh 5,000,000 kutoka kwa ofa ya YATOSHA kwa maelezo zaidi mpigie Mr. Juma kwa kutumia no hii, karibu.

Nikampigia huyo Mr. Juma akaniongelesha maneno mengi mojawapo nimeshinda kwa kadi mbili na zote zina shs 2.500.000 kila moja itabidi niilipie shs 25.000/- kwa kila kadi kwa hiyo niende kwa wakala wa airtel nilipe salio kisha nimtumie halafu nitapata sh 4,495.000/= na nisimwambie mtu yoyote akiwemo yule wakala ambae nitamtumia kutuma pesa.

Nikakaa dakika 5 nikampigia kumjulisha kwamba salio teyari nimeweka. Akanijibu huyo Juma nimtumie haraka hilo salio ana wateja wengi akanipa dakika mbili tu.

Nikanyamaza, baada ya dakika mbili akanipigia na kuuliza vipi tena mbana sijamtumia hela? Nikamjibu kwamba kwa nini anataka kumtapeli tapeli?, Akakata simu haraka sana.

AIRTEL wawe waangalifu na matapeli hao na hebu wafuatilie hiyo no ni ya nani? ILI wampe kibano. Ina maana kama akili yangu isingejumlisha ningeisha liwa sh 50.000/-
 
Jamaa hao ni wezi sugu sijuwi kwa nn hii sheria ya mtandao ime lala kwa hawa jamaa
 
Mkuu, mie nasumbuliwa na Voda katika huduma yao ya Nipige Tafu. Nimeambiwa huwezi pata huduma hii mpaka uiombe lakini mie kwangu ni tofauti, wakiona sina salio tu wananitumia jero.
 
Back
Top Bottom