Wadau,
Kuna utapeli wa aina yake unaendelea kuwatafuta mamia kama sio maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza na mingine ya jirani, kwa kisingizo cha Ajira.
Nyuma ya shule ya msingi Nyanza, jirani na Ofisi za AMREF kuna jengo linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambako kuna taasisi uchwara inayodai kushughulika na masuala ya utamaduni.
ukifika katika Ofisi hizo ambazo ziko jirani na duka maarufu la U-turn, kwanza utavutiwa na mamia ya watu walioko katika eneo hilo wakiwa katika makundi makundi huku wengi wakiwa wamevaa vitambulisho lakini wakiwa nje ya hiyo ofisi. Ndani kuna ofisi yenye vyumba viwili, hapo "Sebuleni"kuna meza mbili ilyoko upande wa kushoto kuna kitabu cha mahudhurio ya "wafanyakazi" na meza ya pili kuna wanawake wasiopungua wattatu wakipitia mafaili.
kwneye mlango wa kuingia kwa "Bosi" kuna mtu ameweka kiti kuratibu wanaoingia na kuangalia kama wamekidhi "vigezo". huko ndani kuna bosi na mtu mwingine wanatumia Laptop, (ndio pekee katika taasisi hii). anaonekana yuko busy kupitia barua nyingi za mambo ya kazi lakini zinazopewa kipaumbele ni zile ambazo waombaji wamelipa ada ya usaili.
Mara anaingia "mtumishi" akiwa na shida. amefiwa na mama mzazi. anaomba ruhusa. Bosi anamwambia sasa inatulazimu kufuata utaratibu, "mtumishi" mwenye tatizo anapaswa kuandika barua ya ruhusa na huyu Bwana mwneye shida anaruhusiwa kwenda kwenye msiba kwani pamoja na mabo mengine anapaswa kwenda kutafuta fedha za shughuli hiyo!
Ili kuweza fanya usaili unapaswa kulipa ada ya shilingi 30,000 na kupewa mtihai huo ambao hufanywa na waombaji wote bila kujali aina ya kazi ya mwombaji. Taasisi hii inadai kuajiri watu kwa niaba ya shirika la Kimarekani ( halitajiwi) ambalo litaendesha harakati za kupambana na ukimwi kwa njia ya sanaa. inaelezwa shughuli zake zitafanyika Tanzania na DRC. Malipo yake, watu wanaambiwa kuwa ni Dola 900 kwa mwezi kwa dereva, pesa ya pango la nyumba dola 3000, malipo ya safari ni dola 100 kwa siku ukiacha mbali fedha za matibabu!
Nje nakutana na Dada moja ambaye amekuja kuomba kazi, katika mazunguzo anasema lazima atafute fedha za usaili mapema kwani shughuli katika shirika hilo la AMREF zimeanza huko tanga kwani ameona kwenye Tv. Lakini namwambia hapo sio AMREF anasema mbona kuna kibao hapo kwneye kona kinaonyesha hapo ni AMREF!
mwingine anasema amekuwa akifika hapo kwa zaidi ya miezi sita sasa na kusaini kitabu cha maudhurio baada ya kupatiwa kitambulisho cha kazi ambacho mwajiriwa hulipia shiilingi 5500. baada ya kusaini kitabu hicho wafanyakazi hawa hukusanyika nje ya ofisi hiyo kupiga soga. wameambiwa wazungu watafika hivi "karibuni" huku ofisi zao zikiwa zinamalizia kukarabatiwa eneo la Nyakato. Utapeli huu umeanza tangu mwezi February mwaka jana na kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa zaidi ya watu 900 wameajiriwa.
Wanahitajika watu wa fani zote unazozifahamu na elimu yoyote kwani kuna nafasi zote hata wafagiaji na wengine watapelekwa DRC!