Utapeli unawatafuna mamia ya wakazi wa Mwanza

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,248
Reaction score
1,740
Wadau,

Kuna utapeli wa aina yake unaendelea kuwatafuta mamia kama sio maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza na mingine ya jirani, kwa kisingizo cha Ajira.

Nyuma ya shule ya msingi Nyanza, jirani na Ofisi za AMREF kuna jengo linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambako kuna taasisi uchwara inayodai kushughulika na masuala ya utamaduni.

ukifika katika Ofisi hizo ambazo ziko jirani na duka maarufu la U-turn, kwanza utavutiwa na mamia ya watu walioko katika eneo hilo wakiwa katika makundi makundi huku wengi wakiwa wamevaa vitambulisho lakini wakiwa nje ya hiyo ofisi. Ndani kuna ofisi yenye vyumba viwili, hapo "Sebuleni"kuna meza mbili ilyoko upande wa kushoto kuna kitabu cha mahudhurio ya "wafanyakazi" na meza ya pili kuna wanawake wasiopungua wattatu wakipitia mafaili.

kwneye mlango wa kuingia kwa "Bosi" kuna mtu ameweka kiti kuratibu wanaoingia na kuangalia kama wamekidhi "vigezo". huko ndani kuna bosi na mtu mwingine wanatumia Laptop, (ndio pekee katika taasisi hii). anaonekana yuko busy kupitia barua nyingi za mambo ya kazi lakini zinazopewa kipaumbele ni zile ambazo waombaji wamelipa ada ya usaili.

Mara anaingia "mtumishi" akiwa na shida. amefiwa na mama mzazi. anaomba ruhusa. Bosi anamwambia sasa inatulazimu kufuata utaratibu, "mtumishi" mwenye tatizo anapaswa kuandika barua ya ruhusa na huyu Bwana mwneye shida anaruhusiwa kwenda kwenye msiba kwani pamoja na mabo mengine anapaswa kwenda kutafuta fedha za shughuli hiyo!

Ili kuweza fanya usaili unapaswa kulipa ada ya shilingi 30,000 na kupewa mtihai huo ambao hufanywa na waombaji wote bila kujali aina ya kazi ya mwombaji. Taasisi hii inadai kuajiri watu kwa niaba ya shirika la Kimarekani ( halitajiwi) ambalo litaendesha harakati za kupambana na ukimwi kwa njia ya sanaa. inaelezwa shughuli zake zitafanyika Tanzania na DRC. Malipo yake, watu wanaambiwa kuwa ni Dola 900 kwa mwezi kwa dereva, pesa ya pango la nyumba dola 3000, malipo ya safari ni dola 100 kwa siku ukiacha mbali fedha za matibabu!

Nje nakutana na Dada moja ambaye amekuja kuomba kazi, katika mazunguzo anasema lazima atafute fedha za usaili mapema kwani shughuli katika shirika hilo la AMREF zimeanza huko tanga kwani ameona kwenye Tv. Lakini namwambia hapo sio AMREF anasema mbona kuna kibao hapo kwneye kona kinaonyesha hapo ni AMREF!

mwingine anasema amekuwa akifika hapo kwa zaidi ya miezi sita sasa na kusaini kitabu cha maudhurio baada ya kupatiwa kitambulisho cha kazi ambacho mwajiriwa hulipia shiilingi 5500. baada ya kusaini kitabu hicho wafanyakazi hawa hukusanyika nje ya ofisi hiyo kupiga soga. wameambiwa wazungu watafika hivi "karibuni" huku ofisi zao zikiwa zinamalizia kukarabatiwa eneo la Nyakato. Utapeli huu umeanza tangu mwezi February mwaka jana na kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa zaidi ya watu 900 wameajiriwa.

Wanahitajika watu wa fani zote unazozifahamu na elimu yoyote kwani kuna nafasi zote hata wafagiaji na wengine watapelekwa DRC!
 
Maweeeee...! Mkuu johnmashilatu ebu saidia hao vijana hata kwa kufuatilia hilo suala hapo ofisi za AMREF penyewe au ripoti polisi mkuu,yaani unaomba kazi halafu unalipa ada ya usaili hata hawashtuki hawa watu kuwa wanaibiwa!
 
Last edited by a moderator:
Maweeeee...! Mkuu johnmashilatu ebu saidia hao vijana hata kwa kufuatilia hilo suala hapo ofisi za AMREF penyewe au ripoti polisi mkuu,yaani unaomba kazi halafu unalipa ada ya usaili hata hawashtuki hawa watu kuwa wanaibiwa!

Mkuu,

Yanayoendelea nchi hii yanashangaza sana haiwezekani suala hilo likaendelea kwa muda wote huo bila mamlaka husika kujua na kuchukua hatua.

vile vile ni bora zaidi kuweka taarifa hizi hapa badala ya Polisi au vyombo vingine huenda wanashirikiana
 
Huu ni utapeli.....ubaya wa Tanzania tuna systems nyingi hadi kila system inategea nyingine ichukue hatua hasa Polisi........Hapo ni hadi wanasiasa akina Wenje watie timu ndio utaona serikali inaibuka......
 
Mkuu,

Yanayoendelea nchi hii yanashangaza sana haiwezekani suala hilo likaendelea kwa muda wote huo bila mamlaka husika kujua na kuchukua hatua.

vile vile ni bora zaidi kuweka taarifa hizi hapa badala ya Polisi au vyombo vingine huenda wanashirikiana

Yes ndio umuhimu wa media kama hizi.....haipiti siku mbili utaona tifuatifua maana ni kama umewaamsha usingizini.....
 
Wadau,

Kuna utapeli wa aina yake unaendelea kuwatafuta mamia kama sio maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza na mingine ya jirani, kwa kisingizo cha Ajira.

Nyuma ya shule ya msingi Nyanza, jirani na Ofisi za AMREF kuna jengo linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambako kuna taasisi uchwara inayodai kushughulika na masuala ya utamaduni.

ukifika katika Ofisi hizo ambazo ziko jirani na duka maarufu la U-turn, kwanza utavutiwa na mamia ya watu walioko katika eneo hilo wakiwa katika makundi makundi huku wengi wakiwa wamevaa vitambulisho lakini wakiwa nje ya hiyo ofisi. Ndani kuna ofisi yenye vyumba viwili, hapo "Sebuleni"kuna meza mbili ilyoko upande wa kushoto kuna kitabu cha mahudhurio ya "wafanyakazi" na meza ya pili kuna wanawake wasiopungua wattatu wakipitia mafaili.

kwneye mlango wa kuingia kwa "Bosi" kuna mtu ameweka kiti kuratibu wanaoingia na kuangalia kama wamekidhi "vigezo". huko ndani kuna bosi na mtu mwingine wanatumia Laptop, (ndio pekee katika taasisi hii). anaonekana yuko busy kupitia barua nyingi za mambo ya kazi lakini zinazopewa kipaumbele ni zile ambazo waombaji wamelipa ada ya usaili.

Mara anaingia "mtumishi" akiwa na shida. amefiwa na mama mzazi. anaomba ruhusa. Bosi anamwambia sasa inatulazimu kufuata utaratibu, "mtumishi" mwenye tatizo anapaswa kuandika barua ya ruhusa na huyu Bwana mwneye shida anaruhusiwa kwenda kwenye msiba kwani pamoja na mabo mengine anapaswa kwenda kutafuta fedha za shughuli hiyo!

Ili kuweza fanya usaili unapaswa kulipa ada ya shilingi 30,000 na kupewa mtihai huo ambao hufanywa na waombaji wote bila kujali aina ya kazi ya mwombaji. Taasisi hii inadai kuajiri watu kwa niaba ya shirika la Kimarekani ( halitajiwi) ambalo litaendesha harakati za kupambana na ukimwi kwa njia ya sanaa. inaelezwa shughuli zake zitafanyika Tanzania na DRC. Malipo yake, watu wanaambiwa kuwa ni Dola 900 kwa mwezi kwa dereva, pesa ya pango la nyumba dola 3000, malipo ya safari ni dola 100 kwa siku ukiacha mbali fedha za matibabu!

Nje nakutana na Dada moja ambaye amekuja kuomba kazi, katika mazunguzo anasema lazima atafute fedha za usaili mapema kwani shughuli katika shirika hilo la AMREF zimeanza huko tanga kwani ameona kwenye Tv. Lakini namwambia hapo sio AMREF anasema mbona kuna kibao hapo kwneye kona kinaonyesha hapo ni AMREF!

mwingine anasema amekuwa akifika hapo kwa zaidi ya miezi sita sasa na kusaini kitabu cha maudhurio baada ya kupatiwa kitambulisho cha kazi ambacho mwajiriwa hulipia shiilingi 5500. baada ya kusaini kitabu hicho wafanyakazi hawa hukusanyika nje ya ofisi hiyo kupiga soga. wameambiwa wazungu watafika hivi "karibuni" huku ofisi zao zikiwa zinamalizia kukarabatiwa eneo la Nyakato. Utapeli huu umeanza tangu mwezi February mwaka jana na kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa zaidi ya watu 900 wameajiriwa.

Wanahitajika watu wa fani zote unazozifahamu na elimu yoyote kwani kuna nafasi zote hata wafagiaji na wengine watapelekwa DRC!
ndugu tunakushukuru kwa taarifa hii ambayo pengine umeileta kwa nia safi na si kuwagutusha ili wakimbie... kwa maoni yangu ungalitoa taarifa kwa kamanda Polisi Mkoa; kabla ya kulileta humu
 
Hivi waandishi wetu wa habari huwa wanatafutia wapi habari zao? CC Manyerere Jackton , Tumaini Makene ,

Mkuu,

kinachofurahisha zaidi ni kuwa miongoni mwa "walioajiriwa" hapo ni pamoja na baadhi ya waandishi wa habari maarufu wa Mkoa wa Mwanza na wengine wako kwenye kazi zao wanasbiri shghuli zianze ili wajiunge na taasisi hiyo
 
Mkuu wa Ntunzu,

Siku hizi hayamambo hayaeleweki, hujui nani wa kumwamini. si hawa polisi huwa waanasema wana - Intelijensia? sasa vipi shughuli hii ifanyike hadharani, mchana kweupe, mita 50 kutoka Nyumbani kwa RC, sio zaidi ya mita 500 kufika makao makuu ya polisi mkoa?
 
Mkuu,

Yanayoendelea nchi hii yanashangaza sana haiwezekani suala hilo likaendelea kwa muda wote huo bila mamlaka husika kujua na kuchukua hatua.

vile vile ni bora zaidi kuweka taarifa hizi hapa badala ya Polisi au vyombo vingine huenda wanashirikiana

Kweli mkuu,vyombo vyetu vya ulinzi vina tatizo kubwa sana,si ulisikia hadi mke wa kamishna wa polisi mwaka juzi tu hapa alitapeli vijana zaidi ya 150 awape nafasi za usalama wa taifa!

Nilikutana na dada mmoja mwezi wa pili pale Geita katoka Tabora katapeliwa laki mbili kaambiwa aje kwenye usaili kufika mgodini wanamwambia hakuna usaili wa nafasi yoyote pale mgodini na ni wengi wamelizwa kwa staili ile.

Inabidi wanaotafuta ajira wawe makini sana,matapeli wanatumia nafasi hii kujinemesha,vijana waepuke sana njia za mkato,wapate ushauri kwa watu wao wa karibu kwa msaada zaidi wa mawazo,tukisubiri hili jeshi la polisi limeoza kabisa tusitegemee jipya.
 
Mkuu,

kinachofurahisha zaidi ni kuwa miongoni mwa "walioajiriwa" hapo ni pamoja na baadhi ya waandishi wa habari maarufu wa Mkoa wa Mwanza na wengine wako kwenye kazi zao wanasbiri shghuli zianze ili wajiunge na taasisi hiyo

Mkuu kwanza naomba nikushukuru na kukupongeza kwa hatua uliyochukua ya kuanika huu utapeli. Labda nikugutushe tu hao unaosema ni ''waandishi wa habari maarufu'' wanaweza kabisa kuwa kwenye huo mtandao wa utapeli, na wanatumika tu kama chambo cha kuvuta watu wengine. Unajua karata tatu inavyoendeshwa? Unakuta ''wachezaji'' wengi lakini kumbe wote lao moja. BTW Tanzania hakuna fani yenye matapeli kama fani ya habari.
 
Inaweza kuwa sahihi kuwa hao" waandishi wa habari maarufu" ni miongoni mwa wanaoshiriki utpeli huo lakini taarifa zilizopo ni kuwa hao watu wamepigwa kama walivyopigwa wengine.
 
Hili suala limeanzia hapa JF naona leo limetinga magazetini

Alisema mdau mmoja hapa kuwa wandishi wetu habari zao hutafutia mfukoni, wakikosa wanaenda google na za nje wanaangalia BBC, sasa hii ndio google yenyewe !
 
Huu utapeli tumezoea kuuona huku Dar
kumbe hadi Mikoani umefika?

Waswahili husema " yaliyoko Pwani hata bara pia yanapatikaa siku hizi" pamoja na mambo mengine unalazimika kujiuliza juu ya kiwango cha ulewa cha Watanzania. Nilifikiri ile "Common Sense" ingewapelekea hawa watu kujiuliza maswali mengi kabla ya kushiriki katika mtego huo ikiwa ni pamoja na kwanini nilipe ada ya usaili?
 
Back
Top Bottom