utapeli mwingine tanesco....

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,052
Tanesco yapinga kuvunja mkataba wa bima
broken-heart.jpg
Na Claud Mshana

SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limefungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliotolewa na Mamlaka ya Rufaa ya Manunuzi ya Umma (PPAA) kuitaka ivunje mkataba wake wa bima ya afya na kutangaza upya zabuni ya kupata huduma hiyo.

PPAA iliagiza kuvunjwa kwa mkabata huo wa Sh3.6 bilioni kati ya Tanesco na muungano wa makampuni matatu ya Alexander Forbes (T) Limited, Strategis Insurance Company Limited na PharmAccess International baada ya kubaini kuwa sheria za manunuzi ya umma, hazikufuatwa.

Uamuzi wa PPAA ulitokana na rufaa iliyokatwa na Tanzania Consortium of Hospitals and Clinics (TCHC) ambao ndiyo iliyokubaliwa kutoa huduma hiyo mwezi Januari, lakini ikajikuta ikitupwa katika mazingira tatanishi na kusababisha ikate rufaa

Lakini, kwa mujibu wa maelezo yaliyowasilishwa mahakamani, Tanesco inaitaka mahakama isikubaliane na PPAA na kutambua uamuzi wa shirika hilo la umma wa kutoa zabuni hiyo kwa muungano wa makampuni hayo matatu kuwa ni wa halali na kwamba taratibu zote za kutoa zabuni hiyo zilifuatwa.

Novemba mwaka jana, Tanesco ilitangaza zabuni ya kutoa huduma za afya kwa wafanyakazi wake wapatao 5,000 na baada ya tathimini ya kina ya bodi ya Tanesco, zabuni hiyo ilitolewa kwa TCHC.

Hata hivyo, wakati kampuni ya TCHC ikijiandaa kuanza kazi, zabuni hiyo ilitenguliwa na baadaye kupewa muungano wa kampuni za Alexander Forbes (T) Limited, Strategis Insurance Company Limited na PharmAccess International, ambazo mwanzoni zilishindwa katika mchakato wa zabuni.

Katika maelezo yake, Tanesco imesisitiza kuwa ilifuata taratibu zote zinazotakiwa kisheria na zinazotumika katika manunuzi ya umma.

Kwa mujibu wa Tanesco, PPAA ilikosea ilipotoa amri ya kurudiwa kwa mchakato wa zabuni wakati tayari mzabuni alishapatikana na ameshaanza kufanya kazi.

Imeongeza kuwa uamuzi wa kubatilisha matokeo ya mchakato wa zabuni hiyo si sahihi kwani kuna ushahidi kuwa TCHC walitolewa baada ya kushindwa kujaza fomu za zabuni.

Pia katika hoja za Tanesco zilizowasilishwa Mahakama Kuu ni pamoja na uhalali wa PPAA kusikiliza na kuamua rufaa zilizowasilishwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Tanesco, mamlaka ya rufaa ilifanya kazi zaidi ya uwezo wake kisheria kwa kuamua masuala ambayo hayapo ndani ya uwezo wake kwa mujibu wa kifungu namba 82(4) cha sheria Na 21 ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 004. “Kama maelekezo yanayotakiwa hayatafanyiwa kazi, Tanesco itakuwa katika hali mbaya na kupata hasara kubwa na mambo mengine mengi kwa sababu tayari wafanyakazi wake wameshaanza kupatiwa huduma za matibabu na kampuni iliyoshinda zabuni,” kwa mujibu wa maelezo ya Tanesco.
 
mtajiju vunjilia mbali iwe fundisho kwa wengine
 
Back
Top Bottom