Utapeli mpya mjini | Mawakala wa huduma za kifedha kuweni makini sana

Huu ni uzembe wa hali ya juu sana huwezi kumpa mteja ajaze namba mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utahudumia wateja wangapi kwa siku kwa staili hiyo ? Imagine uko na wateja wa5 kwa wakati mmoja, kila mtu ukisema uanze kuandika taarifa zake si wengine watakukimbia.
 
Mimi kwenye biashara ni kauzu zaidi ya dagaa sicheki hata kwa bahati mbaya ukija na blablaa nikikuangalia tu mara moja unaondoka bila kuaga


Sent using IPhone X
 
Inatakiwa umakini sana matapeli wana njia nyingi sana, juzi kitaani hapa kuna dada na akiwa dukani kwake kapokea mteja, mteja aliomba soda take away dazan kadhaa akidai wana part jirani na hapo, akaomba wamsaidie kabisa na kubeba hadi katika nyumba aliodai amepanga, kule wakamkuta mdada anafua nguo na hakushtuka na ujio wa vinywaji, walipokua wanaenda kuchukua vinywaji mara ya pili jamaa akaomba atumiwe 250,000/= katika m-pesa ili wakimaliza kubeba vinywaji atoe hela yote, alipotumiwa tu akawapiga chenga na kutokomea. Walipoenda pale kuulizia yuko wapi wakaambiwa jamaa alikuja pale na kuomba aweke vinywaji kwa muda kwani anataka azunguke kutafuta mahitaji mengne ndo mana alipokuja hakuna aliekua anamshangaa. Ndo dada wa watu kujua ameshapigwa 250 fasta, akaanza kulia na kubeba soda zake dah
 
Uondoke ofisini kwangu halafu urudi na stori zako za alinacha

Utasimulia ntavyojitoa ufahamu sikujui,maana hamna ruhusa kwa wakala

kutuma pesa kwa mtu wa mbali,wakala anatakiwa kumuwekea pesa

mteja mwenye simu yake mkononi sio simu ipo kwa mtu mwingine

sasa wewe urudi ulete story zako za Ba Be Bi Bo Bu,nakuruka futi 100
 

Huyo atakuwa mgeni kwenye biashara au alikuwa na mambo mengi kichwani. Yaani mtu unatoa laki sita bila kuangalia salio? Mimi ule muda nakuhesabia hela huku natuma voda sms ya kuangalia salio i.e narequest kuona salio kabla sijatoa hela.
 
Daaah,huu ni ushauri mzuri sana.
 
Utahudumia wateja wangapi kwa siku kwa staili hiyo ? Imagine uko na wateja wa5 kwa wakati mmoja, kila mtu ukisema uanze kuandika taarifa zake si wengine watakukimbia.
Ndugu yangu wee. Ulikimbia umande nini. Usiniambie watu watano ni vigumu kuwahudumia huku ukichukuwa details zao! Kwani unapowahudumia unahudumia wote kwa wakati mmoja? Unahudimia wa kwanza huku wengine wanaandika Ukimalizana naye wengine wanakuwa tayari
 
duhh, ukae na simu ya wakala muda wote huo asipokushtukia basi yeye ni mzembe
 
Huna hata haja ya kupiga hesabu hapo, kwa kawaida mteja anatakiwa apate confirmation sms kabla hajamalizana na wakala. Kama ulimwekea nae akathibitisha kuwa tayari imeingia ndio imeisha hivyo.
Huo ndio ukweli, maelezo mengi ya mleta mada hayana msingi. Mteja haondoki mpaka taarifa ya sms ionekane kwake. Akisha kupa kisogo biashara imekwisha. Wakala anaehadaiwa kiasi cha kudiriki kupiga simu huduma kwa wateja ujue ama ni mgeni ktk biashara, au akili imeanza kuingia kutu au Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unayazungumza hayo kwa kuufikiria ulimwengu wa ushindani ? Unajua sifa za wateja ? Nani anayependa kusubirishwa ilihali pembeni kuna huduma kama hiyo ambayo inatolewa pasipo hizo interview za kukusafanya details ?
 
wamekuonamo tu unashindwa kumtandika ngumi moja takatifu kabisa uyo jamaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao matapeli wanajuana,izo mbinu za matapeli kila cku zinakuja mpyaa...
 
Mbona unaonesha wewe wakala hauna uhakika! Unapoamua kithibisha toka Airtel ni kwamba hauna uhakika na kazi yako, ulichokifanya usithubutu kumuuliza mtu mwingine kama ulikifanya unajifunga, kataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…