Utapeli mpya kwa wafanyabiashara

Utapeli mpya kwa wafanyabiashara

Habari ndugu zangu, huu utapeli unaweza ukawa ni mpya kwangu ila kwa wengine ni wa kizamani. Ipo hivi jana kuna mteja alipiga simu dukani anataka betri za gari(N150 mbili na N70 moja) tukakubaliana apelekewe Masaki, tukamtafuta bodaboda wetu mwaminifu tukampa mzigo. Yeye(tapeli) alichofanya hapo Masaki alitafuta sehemu akawaomba wenyeji
Mkuu hizo betri akatolee kaunta ya polisi.

Huyo ni kumkomesha kwa kumfungulia kesi
 
Kama wana makando yao basi hawawezi kwenda wataogopa.

Ila kukabidhi mzigo na kusepa bila kupokea hela, hapo wamezingua.
Biashara ilikuwa ya halali haina makando kando
 
Yaani mmepigwa kiuzembe kabisa

Alafu kwa taarifa yenu sahvi matapeli

Wanapenda kutumia address za masaki,obay,mbezi beach maana wanajua nyie mnashobokoa na watu
Wa huko na mnawaamini

Ova
 
Habari ndugu zangu,

Huu utapeli unaweza ukawa ni mpya kwangu ila kwa wengine ni wa kizamani. Ipo hivi jana kuna mteja alipiga simu dukani anataka betri za gari(N150 mbili na N70 moja) tukakubaliana apelekewe Masaki, tukamtafuta bodaboda wetu mwaminifu tukampa mzigo.

Yeye(tapeli) alichofanya hapo Masaki alitafuta sehemu akawaomba wenyeji kuwa kuna mzigo wake kuna mtu anamletea alikuwa anaomba amkabidhi then atakuja kuuchukua baada ya mda. Bodaboda alivyofika walipokubaliana akampigia simu huyo tapeli ila jamaa(tapeli) akamwabia kuna mlinzi hapo amkabidhi afu pesa ya betri pamoja na ya usafiri aje achukue Mikocheni mana amepata emergency kidogo(kumbe kuna sehemu kajibanza anamchungulia)

Bodaboda akauacha mzigo kwa walinzi akijua ndo nyumbani kwa jamaa kisha akaanza safari kuelekea Mikocheni, na yule jamaa baada ya kuona boda kasepa akaja na bajaji akapakia mzigo akaondoka zake. Boda kufika kule simu haipatikani, kurudi alipoacha mzigo wale walinzi wakamwambia jamaa kashachukua mzigo wake.

Boda inabidi arudi dukani kutupa taarifa, boss akamwambia ampeleke alipouacha mzigo walivyofika pale kwa bahati nzuri kulikuwa na CCTV camera, jamaa akaonekana na bahari nzuri tena jamaa tunamjua ni jirani yetu(tupo ghorofa moja) akapigiwa simu kwa no yake ya kawaida akasema atarudisha betri ila mpaka naandika hapa bado betri hazijarudi.

Mnisamehee kwa uandishi mbovu
Somo zuri
 
Back
Top Bottom