Utapeli kwa wastaafu

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Tarehe 30 Januari, 2017 muda wa saa tano hivi. Kwanza Mama mmoja akanipgia simu akanisalimia vizuri na kuniuliza siku hizi uko wapi na baada ya kumaliza mwanaume akapiga simu tukasalimiana na baadaye akanieleza kuwa Mhe.Rais ameunda TUME ya kuhakiki taarifa za wastaafu na katika kupitia taarifa yangu inaonekana kuna fedha nilipunjwa sasa wanataka wanisaidie. Nikawauliza mtanisaidiaje?. Wakanieleza kuwa watafanya utaratibu ili nipate mapunjo yangu. Baada ya kumdadisi sana nikaona huyu ni tapeli nikakata simu. Kuweni maakini na matapeli kama hawa.
 
Back
Top Bottom