Utapeli Kwa Njia ya SMS – Tuwe Makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utapeli Kwa Njia ya SMS – Tuwe Makini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Apr 19, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Utapeli Kwa Njia ya SMS – Tuwe Makini
  Ndugu zangu kuna watu wameanza kulalamika kwamba wanapata ujumbe kwenye simu zao za mikono kutakiwa kuchangia vyama kadhaa vya kisiasa nchini , nilipopata habari hii sikuamini kabisa kwamba sasa vyama hivyo vimeamua kuanza kutuma ujumbe wa kuomba michango kwa watanzania mbalimbali kutumia simu zao za mikono
  Ukicha hili huko nyuma haswa wale wateja wa mtandao wa tigo walikuwa wanapokea ujumbe unaofanana na huu ingawa wao walitakiwa kuchagua habari wanazozitaka kama ni za simba au yanga na kupokea habari toka klabu hizo au kuchangia klabu hizo kupitia simu zao za mikono ingawa mwishoni baadhi ya wanachama wa simba walilalamika kuhusu upotevu wa fedha hizo sijui kwa yanga .


  Ndugu zangu hali inaonekana kuwa mbaya sasa wajasiriamali wanaamua sasa kutumia mwanya wa kutokuwa na sheria kali za mawasiliano kuamua kuanzisha vitu na mengine mengi ambayo hayata tija kwa taifa kuchukulia wenzao fedha na kutokomea kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo kwenye sehemu kadhaa bila vigogo hao kujua kwamba nini kinachoendelea .


  Ndugu zangu tuwe makini sana na mialiko hii ya kuchangia vyama , makundi na aina nyingine zozote za michango tunazotakiwa kutoa bila ridhaa zetu huku ni kutunyanyasa na ninaomba utaratibu wa kushitaki kampuni ya simu ambayo inaruhusu mtandao wake kutumika kutuma matangazo na kuanzisha michango kama hii ambayo haina maslahi na imelenga katika kutapeli na udanganyifu wa hali ya juu
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Waganga njaaa hao Changia Polo Nishinde Ubunge Tuma neno Polo na voucher ya sh 500, 1000, au 2000 au zaidi kwenda number 0............2
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Chama kinacho tawala omba omba, serikali nayo omba omba sasa mtawalaumu wale omba omba pale ubungo????
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huku nje niishiko natumia voda na juzi nimepata sms eti nichancie ccm ishinde 300, 500 na 1000 nkasema hawa jamaa hawachoki?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Thanks SHY
   
 6. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hao jamaa naona wamejaa njaa isiyotibika. Hata kama wangeua watanzania wote na kubaki wao tu na rasilimali za nchi wasingeshiba.
  Tamaa iliyopitiliza inawateketeza matumbo yao.
  Shame on you!!! Eti kutoa ni moyo, je kutumikia jamii ni nini?
  Sichangii ng'o
   
Loading...