Utapeli kwa kushirikiana na jeshi la polisi?

Jovanny hm

Member
Jun 5, 2019
31
25
Kumetokea utapeli mpya, huu nimeushuhudia manispaa ya Moshi Mjini.

Iko hivi, kunawafanyabiashara wa vyombo vya electronics kama vile Simu na Computers ambao wanauza hivi vifaa vipya na vingine used.

Hawa jamaa wakikuuzia kifaa used (let's say Simu) huwa wanakaa baada ya muda fulani then mteja aliyeuziwa anapigiwa simu na mtu ambaye anajitambulisha kuwa ni askari polisi kitengo cha upelelezi (huwa anakuwa ni askari kweli lakini anashirikiana na hawa wafanyabiashara) na kuambiwa kuwa kifaa alichonacho ni cha wizi hivyo anatakiwa kureport kituo cha polisi.

Na hivyo ndio jinsi mtu anavyopigwa, mteja akireport kituoni basi kile kifaa alichokinunua kinachukuliwa kama mali ya wizi na pia mteja huyo hulazimika kulipa fidia ya gharama zilizotumika kumtafuta na pia wanaweza wakaenda mbali zaidi wakaongeza na vitu vingine watakavyodai kuwa viliibiwa pamoja na simu/kompyuta.

Kuweni makini, hao wauzaji wa hivyo vifaa ambavyo ni used mara nyingi huwa hawana maduka ila ukifika sanasana maeneo ya stand watakukaribisha kwenye duka la Simu/ Computers na wao huwa wanaongea kuliko hata wamiliki wa maduka hayo na chaajabu mmiliki wa duka husika yeye hukaa kimya, na hapa ndipo ushahidi unakosekana ikiwa utawalazimisha askari polisi uwende nao sehemu ulipo nunua kifaa chako, maana ukifika mmiliki wa duka anakukana.

Kumbuka; Wanaweza wakakukatia receipt feki yenye jina tofauti na lile la usajili wa duka...

Kuweni makini, askari wetu siku hizi nao ni njaa tu.
 
Dah biashara ya used items inakuwa ngumu, Hawa matapeli wanaaribu biashara za watu.
 
Umejua leo?

Soma FB wanavyolia. Mkome kununua simu za Mkononi. Nendeni madukani. Ujanipa simu labda aniuzie Mama yangui.
 
OMBAA WASIKUTANE NA WEWE UTATAJIWA HELAAMBAYO IMETOLEWA KWENYE SIMU HATA MWENYESIMU AKUWAHI KUSHIKA MPAKA AFE
 
SIKUHIZI #06#
SAVE HINAMBA INAYOKUJA WAKIKUGUSA UNAPELEKA HOSP POLICE WANAMPATA FASTA
 
Back
Top Bottom