Utapeli Duniani

Utapeli Duniani

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,228
Reaction score
10,738
Utapeli kiukweli ni suala lililokuwepo tangu zamani. Na limekuwa gumzo na Tatizo kubwa duniani. Maendeleo ya Teknolojia ikiwemo Pesa mtandaoni hususani Pesa kwenye laini za simu na benki. Katika karne hii ya leo utapeli umechukua suala la pesa mtandaoni kama ndo kitega uchumi na upenyo.

Mwanzoni mwa Mwaka huu nilipokea Moja kati ya zile sms za “Hiyo pesa itume kwenye namba hii 0765 385 234 Kwa Majina ya Debora Elia. Sasa wakuu kweli kipindi kile ndo nilikuwa nimetoka kufanikisha kufikisha pesa ya kodi laki 4 ili nimpatie Mama mwenye nyumba. Roho ilikataa nikasema ngoja nitafanya muamala baadaye kisha ile namba nikaisave kwa jina la mama mwenye nyumba.

Niliendelea na mambo yangu na ilipofika jioni nikasema ngoja niendee kufanya muamala lakini wakati niko njiani ghafla nikapigiwa simu na Binti wa Mama Mwenye Nyumba kuwa Mama amepata tatizo ghafla na amelazwa hospitali Aga Khan hivyo nikipata muda niende kumjulia hali.

Nikaona sio vyema nitume pesa mtandaoni ila niende nayo mkononi mpaka kwa Mama ili kama kutakuwa na Malipo ya matibabu iweze kusaidia. Nilifika hospitali na kumjulia hali alikuwa anaendelea vyema tu amepata nafuu.

Kisha nikampa pesa yake lakini nikamuuliza kuwa Je nilipaswa kutuma pesa kama alivyoniambia kwenye ujumbe mfupi au??? Yule Mama akadai kuwa hakuwahi kunitafuta wala kunitumia ujumbe ule [emoji15] Aisee nilishtuka sana kuangalia majina ya ile namba ni majina ya Mwanamke (Debora Elia) ila ni tofauti Kabsa na Mama Mwenye Nyumba Kwani Mama Mwenye nyumba anaitwa Aisha Jumanne.

Yaani nilikuwa nakwenda kutuma zaidi ya laki nne kwa mtu bila kujua [emoji24] Duuh jamani matapeli hawa yaani mpaka nimewachukia watu wa mitandao. Nilikwenda polisi kutoa ripoti na suala linashughulikiwa. Sio kwa ajili ya nia mbaya bali ni kwa ajili ya Mama Mwenye Nyumba Aliniambia nifanye hivyo sio kwamba wakamatwe ila kuwa na amani ya roho tu.
Nisameheni sana niliufuta ujumbe ule. [emoji120]

Jamani wakuu Tuendelee kuwa waangalifu [emoji120]

Mchana Mwema
 
Ngoja na wenyewe waje watoe comment
 
Ww jamaa n bwege, et huwezi kuweka majina ya huyo tapeli kwa sababu za kiusalama [emoji23][emoji23][emoji23] kwan ungetapeliwa ungeenda kwa nani kushtaki.?

Asante kwa kunipa cheo kipya [emoji120]
 
Ww jamaa n bwege, et huwezi kuweka majina ya huyo tapeli kwa sababu za kiusalama [emoji23][emoji23][emoji23] kwan ungetapeliwa ungeenda kwa nani kushtaki.?

Afu umeenda polisi kupeleka taarifa [emoji24][emoji24][emoji24] unadhani kuna jipya utapata baada ya kupeleka hizo taarifa.?

Nakazia.
 
Nimewaelewa kwenye vitu hivi viwili:
1. Hamtukata kabsa nikaripoti au kutoa ripoti polisi kuhusu jambo hilo. Kwa hofu ya kutokufanyiwa kitu chochote au upelelezi.
2. Nilitakiwa niweke jina na namba ya mtu aliyetaka kunitapeli ingawa sijafanya hivyo.
NB: Nashukuru sana kwa hoja hizo [emoji120]
 
Ww jamaa n bwege, et huwezi kuweka majina ya huyo tapeli kwa sababu za kiusalama [emoji23][emoji23][emoji23] kwan ungetapeliwa ungeenda kwa nani kushtaki.?

Afu umeenda polisi kupeleka taarifa [emoji24][emoji24][emoji24] unadhani kuna jipya utapata baada ya kupeleka hizo taarifa.?
Naunga mkono hoja.
 
Screenshot_20210127-021703.png
 
Unaanzaje kutuma Pesa bila uthibitisho wa kumpigia simu mtu unayetakiwa kumtumia tena kwa namba yake unayoifahamu? Binafsi siwezi kuibiwa kwa kutuma meseji ya ile pesa tuma kwenye namba hii. Hao wezi wanatumia udhaifu wa wa TZ wengi kutuma pesa bila ya kuthibitisha upande wa pili ilimradi tu alikua anadaiwa na mtu fulani. BTW unaweza kuiripoti hiyo namba polisi/Kwa mtandao unaokupatia huduma za mzwasiliano na itafungiwa mara moja. Ukitaka ifuatiliwe kwa kina zaidi Ripoti polisi
 
Ni kweli mkuu Asante kwa mawazo yako. Ila kwa watanzania hawana imani na polisi [emoji2960] Jaribu kuona comments za mwanzoni Kabsa [emoji16] Mtu anakuuliza kuwa unakwenda polisi ili iweje?? [emoji15] Na sijawahi kutuma kiasi kikubwa kuanzia 50k bila kuwa na hakika na mpokeaji.
All in all Shukrani sana
 
Back
Top Bottom