Utapeli.bayport.mikopo

Utapeli.bayport.mikopo

Poleni sana, watumishi na wajasiriamali mliokopa kwnye hizi taasisi binafsi za fedha.

KINACHONISIKITISHA SANA SERIKALI KUPITIA HII WIZARA ISIYO NA HURUMA NA WANANCHI BALI MASLAHI YAO KWANZA/WIZARA YA FEDHA. Hakuna hatua wanachukua.

Hizi taasisi ni wakopaji kama wewe kwny taasisi kubwa za kifedha kama Bank.
Yaani wewe na wakina Bayport ni wateja sawa wa NMB au CRDB.

Lakini kwa kuwa wao ni taasisi wanakopesheka zaidi yako. Wakishapata mkopo mkubwa wanakuja mtaani wanakopesha kidogo kidogo hata kwa mwezi mmoja huku riba ikiwa ni ile ya Bank JUMLISHA riba yao yenye faida Yao.
Kwa hali hiyo ni LAZIMA RIBA ZAO ZIWE KUBWA MNO almost mara mbili ya zile za Bank.

Hapa wizara ya fedha ilibidi kuweka muongozo na si kukaa kimya huku wananchi wakiteseka na madeni makubwa.

Ikumbukwe tu Riba tu za Bank zenyewe kwa nchi hii bado ni kubwa mno pamoja na kujinadi wamepunguza mpk 17%.
Sehemu watu mlipo chezeshewa dish ni kuongeza miaka mpka 5 au 7 ya kurejesha Deni. Hakika nafuu haipo ila wengi hamfahamu hilo, kwa kuangalia makato kidogo ya kila mwezi.
Riba zinatakiwa kubakia asilimia isiyozidi 9%.
Maisha haya magumu kwa nchi maskini zote ni kutokana na madeni yenye Riba kubwa. Umaskini huu hautaisha kwa Miaka mingi ijayo.

Nafikiri kila kukicha mnasikia serikali ikikopa tena madeni makubwa Sana, hapo Riba hiyo yote ni yetu sisi Raia wa chini, TUTAPATA TAABU SANAAAA.

Ushauri wangu usikope BAYPORT na ndugu zake wala watu Binafsi. Tumieni Vikoba kwa wafanyabiashara wadogo, SACCOS kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa. Anzisheni mifuko ya kusaidiana na Harambee za Mitaji.

TATIZO KUBWA WATANZANIA NI WATU WA KUTAKA HELA YA HARAKA, KWA MFANO MNALENGO MOJA KWA NINI MSIJIUNGE WATU 50 MKAJIPA MUDA HATA WA MIEZI 6, YA KUCHANGIA NA KUKUZA MTAJI WENU AMBAO HAUTAKUWA NA RIBA YA MTU VILEVILE BIASHARA YENU IKIANZA MNAKUWA MMESHAJIPATIA AJIRA YENU YA KUDUMU NA VIZAZI VYENU??

TAFAKARI HILO ANZA SASA.
Hiki ndiyo kitu chanya nimekisoma asubuhi hii.

Unastahili likes.
 
BAYPORT HAWANA UTOFAUTI NA WALE WANAOANDIKA WAKISEMA " Ile pesa itume kwenye namba hii jina litakuja Public Enemy, tuma haraka nipo kwa wakala simu yangu ina matatizo ya mic"
 
Hizi kampuni ni za kukopea pesa isiyozidi Milioni 1,kadri mkopo unavyokuwa mkubwa na riba ndio inapaa,Mf. Ukikopa M10 unaweza kurudisha hata M27,Ni wazuri ila sio kwa mkopo mkubwa,take into account..
 
Back
Top Bottom