Utamu wa "Ukubwa". | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamu wa "Ukubwa".

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MAMMAMIA, Jul 10, 2011.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hii ingefaa kubaki kwenye jukwaa la siasa kwa ajili ya wanasiasa wetu, lakini kwa kuwa ni utani, hapa pia itafaa, lakini badala ya kucheka, naomba utafakari:

  Kuna mfalme mmoja aliamua kusafiri mbali ya ufalme wake. Kwa kuwa alikuwa haamini kumwachia ukaimu binadamu yeyote kwa hofu ya kusalitiwa, akaamua kumweka mbwa wake kukaimu. Akampa yule mbwa maelekezo yote juu ya nini anatakiwa kufanya, "kulinda kiti cha ufalme".

  Mbwa ikawa akishakuamka asubuhi, anaingia kwenye ukumbi wa baraza la mawaziri na kukaa kwenye kiti cha mfalme, anatulia tuliii huku mawaziri wanaendelea na shughuli zao. Wakimaliza kazi, wote wanatoka, anafunga mlango na kuondoka na ufunguo. Utaratibu ulikuwa vile kwa mwezi mzima wakati mfalme alipokuwa safarini.

  Mfalme alirejea usiku, asubuhi yake baada ya chai akaenda kwenye ukumbi wa mkutano. Kufika kule akamkuta mbwa ameshawahi na tayari yupo katika kiti cha ufalme. Mfalme alitarajia mbwa angelinyanyuka kumlaki na kumpisha kiti chake, lakini mbwa alibaki pale pale. Mfalme alipomkaribia, mbwa "ghrrrrrrr", ananguruma kuonesha kukerwa kwake. Mara ya pili Mfalme alipokaribia achania akang'atwa mkono, wengine akawachania nguo. Ikawa kazi, mbwa alikasirika, akawa mkali, anamtafuna yeyote anayekaribia kwenye kiti.

  Utamu wa uluwa ulishamkolea na hakuwa tayari tena kuukosa. Suluhisho la mwisho, mfalme akaenda kuchukua gobore na kumaliza maisha ya mbwa, vyenginevyo asingeweza kurudi katika kiti chake.
   
 2. kisute

  kisute Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu umetumia lugha ya picha. ujumbe umefika. asante
   
Loading...