Utamu wa pesa, kwako ni upi?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,483
40,500
Siku zote pesa inatakiwa ikupe mahitaji ya msingi, ndio maana tunatumia nguvu nyingi katika kuzitafuta.

Tunaamini na imethibitika, hatuwezi kuishi miaka 150; mara nyingi tumezidi sana tena kwa wale wachache sana wanaweza kubahatisha miaka 100.

Sasa, maisha ni nini, Je ni kuishi kwa furaha katika maisha yako yote au kuishi kwa mateso ndani ya hiyo miaka 100 kama utafika?

Pesa unayo; sehemu za starehe huendi kuondoa msongo wa mawazo, pombe hunywi, kutalii nje ya nchi huendi, mbuga za wanyama hutembelei, pisi kali huna, zaidi ya kuwaona kwenye mtandao kama wale wanaopatikana Peru, Colombia, Venezuela n.k

Sasa, kwako utamu wa pesa nini?​
 
Sasa, kwako utamu wa pesa nini?
Utamu wa pesa ni mwingi mkuu..
° Unaishi sehemu unataka
° Unakula aina ya msosi unaojisikia kula
° Unakula pisi unayotaka
° Unatumia usafiri unaopenda
° Unakuwa huru kwenda popote unapopenda
° Nk, nk..
° Kwa kifupi, pesa inakupa uhuru wa kuishi utakavyo ili mradi huvunji sheria
1701941991142.png
 
Utamu wa pesa ni mwingi mkuu..
° Unaishi sehemu unataka
° Unakula aina ya msosi unaojisikia kula
° Unakula pisi unayotaka
° Unatumia usafiri unaopenda
° Unakuwa huru kwenda popote unapopenda
° Nk, nk..
° Kwa kifupi, pesa inakupa uhuru wa kuishi utakavyo ili mradi huvunji sheria
View attachment 2835564
Swali; Je, wote wenye hela wanafurahia au wanautumia uhuru huo?
 
Utamu wa pesa ni kujihudumia mambo/mahitaji ambayo wewe mmiliki wa hizo hela unayapenda na una enjoy,

Utamu zaidi wa hela ni kusaidia watu wasio jiweza,ukimsaidia mtu basi nafsi yako inakua na amani ya ajabu sana na una relax.
Inategemea, kama wewe kutoa inakupa furaha ya asilimia 200%; ni vizuri kufanya hivyo
 
Mzee mmoja alisema anamshukuru Mungu sababu hajui shida ya kuwa tajiri lakini pia hajaonja umaskini.

Raha ya pesa ikupe mahitaji muhimu kwa wakati halafu ibaki kidogo ya kukupa assurance kwamba hata likitokea lingine pesa ipo

🚀
 
Utamu wa pesa ukutimizie mahitaji yako na familia yako, pia ukupe moyo wa kuweza kusaidia wengine wenye uhitaji
na la zaidi sana, usikupe kiburi cha kudharau wengine ambao hawana hizo pesa kwani kuna wengine wanafanya kazi kubwa na ngumu kuliko wewe lakini hawazipati hizo hela.
In general, pesa isikubadilishe kutoka mtu mwema na kuwa mtu katili ila ikufanye uongeze busara zaidi kwenye maisha yako. Pia umkumbuka muumba wako kwa kumshukuru kwa ajili ya pesa alizokupa na uzima/uhai.
 
Back
Top Bottom