mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 6,499
- 18,166
Katika maisha ya hapa bongo, unaweza kutana tu na mtu labda tuseme ni mfanyakazi mwenzako, au ni mfanyabiashara au hata bodaboboda akiendelea kupiga mishe zake tu za kawaida na mambo yanaenda.
Lakini mtu wa namna hii unaweza kukuta ni mwajiriwa anayefanya kazi kwenye idara ya kijasusi. Japo kazi yake let's say kama ya bodaboboda ni coverup ili asijulikane , lakini kwa mtu ambaye ni mdadisi unaweza kujua tu mtu fulani anafanya kazi idarani pasipo hata kuambiwa bali kwa kumtambua madhaifu yake Fulani fulani ya kibinadamu mfano kupenda wanawake au kupenda attention kulikokupitiliza.
Yaani jambo kidogo alilofanya tu anataka asifiwe au kutongozatongoza hovyo. Hizi tabia za namna hii huwa zinamu expose sana mtu kwa haraka baadaye inakuja kumgharimu na kuigharimu nchi kwa ujumla . .., anyway ni mfano tu wa kile nachotaka ku share nanyi.
Ipo hivi , nchini Israel, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imeanzisha project ya siri sana ya utengenezaji na urutubishaji wa uranium kwa ajili ya nyuklia. Eneo ambapo kulikuwa kunafanyika hii project palikuwa ni sehemu ambayo haikupaswa kujulikana kwa gharama yotote ile."TOP-SECRET". Eneo hili paliitwa Dimona nuclear reactor ambapo uranium ilikuwa ikirutubishwa kwa ajili ya matumizi ya utengenezaji wa silaha za nyuklia.
Kutokana na eneo hili kuwa la siri sana, waliobahatika kuajiriwa hapo walikuwa wanapitishwa kwenye mchakato mrefu sana kabla ya kuajiriwa . Mfano unafanyiwa background checks, kuhojiwa kwa muda mrefu(interrogation), kujaza baadhi ya fomu za usahili ambazo majibu yake yangechukua muda kidogo kujibiwa na vyombo vya ulinzi na wataalamu wengine wa kiusalama ndani ya Israel. Na hata kama mtu angepita na kuajiriwa eneo hili la Dinoma, bado pia angeendelea kuwa kwenye surveillance ya kufuatiliwa kwa kila analofanya in daily basis.
Sasa basi yupo jamaa mmoja aliyeitwa Mordechai Vanunu ambaye aliamua kutuma maombi ya kazi eneo hili la Dimona baada ya kuona tangazo kwenye gazeti la The Daily la Israel na kuziwasilisha barua zake kwenye ofisi iliyohusika katika utumaji wa maombi iliyokuwa kwenye mji wa Beersheba. Baada ya kufanyiwa security checks ,huyu jamaa alibahatika kuajiriwa eneo hili la Dinoma zilipo facility za kuchakata Uranium pasipo shida yoyote ile .
Lakini huyu Mordechai Vanunu alikuwa ni mtu wa itikadi kali za mrengo wa kushoto ambapo kwa nchi ya Israel kulikuwa na chama cha kikomunist cha Rakah ,ambacho kiuhalisia kilikuwa kikipinga sana harakati za kizayuni . Yaani kilikuwa chama cha Anti-Zionist na kwa sera zake kilikuwa kikipata sapoti na waarabu ambao ni radicalists walioko ndani ya Israel na ambao pia walikuwa pro-palestines. Lakini huyu bwana alikuwa akikisapoti. Na sijui nini kilitokea kwenye usaili wa huyu bwana Vanunu akapita licha ya mrengo wa huyu jamaa aliokuwa kisiasa ambao ulikuwa una m-disqualify kufanya kazi eneo hili. Maybe ni Human Errors za wahusika.. anyway....
Kiuhalisia huyu jamaa alikuwa ni mtu mwenye kipaji sana ila background yake ya kisiasa na vyama alivyokuwa akisupport vilipaswa kuwa red flags za yeye kutokupata kazi eneo hili la Dimona. Kwanza alikuwa na marafiki wengi wa kipalestina na pia kabla ya hapo alikuwa akisupport chama cha Likud cha mrengo wa kulia ambacho sera zake zilihusisha kuikalia kimabavu Palestina lakini baadaye huyu bwana akahama na kuhamia vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo vilikuwa vikipata support ya waarabu. Inadaiwa alihama mrengo baada ya vita kati ya Lebanon na Israel ya mwaka 1982. Hii vita ilimfanya ajihisi mpweke kutokana na uonevu wa Israel kwa waarabu ikizingatiwa yeye origin ya mmoja wa mzazi wake ni Morocco .
Pia huyu bwana aliwahi kufeli Admission test ya kujiunga na jeshi la anga la Israel na kumpelekea kujiunga na Engineer Corps. Hii ilimfaya achukie sana harakati za kizayuni.
Baada ya kutoka jeshini alijiunga na chuo kikuu cha tel Aviv kusoma uhandisi, na baadaye akatoka tena na kurudi mji wa Beersheba na kuanza kusoma masomo ya uchumi Ghafla akaacha tena na kuanza kuchukua masomo ya falsafa.
Huyu bwana Mordechai Vanunu alikuwa ni mtu mwenye njaa ya pesa sana tokea akiwa anasoma chuo. Kwa mfano kila mara alikuwa akiwaambia ma classmates wake yeye anataka kuwekeza kwenye Stock market na alikuwa ameweka kama top priority somo la stock market kati ya masomo yake ya chuo. Huyu bwana kutokana na kupenda pesa, chuoni alikuwa akifanya part-time jobs kama model wa picha za uchi. Yaani anapiga picha za uchi na kuziuza kwenye makampuni yaliyokuwa yakizinunua hizo picha.
Kwa kifupi huyu bwana Mordechai maisha yake ya chuo ya kupenda pesa au kupiga picha kama model haikuwa kipengele sana cha kumzuia yeye kuja kuajiriwa eneo hili la Dimona Facility, ila mrengo wa chama alichokuwa akisupport kingeleta na kuzua maswali kadhaa wakati wa kufanyiwa background checks yake.
Hata baada ya kuajirwa eneo hili huyu bwana alionekana kuendelea ku support chama cha Rakah waziwazi na alionywa mara kadhaa na wakubwa lakini ni kama hakuwa anasikia la wakubwa wake. Hata faili lake kumhusu huyu Mordechai lilipofikishwa mezani kwa wakubwa kwenye idara ya usalama wa ndani ya Israel iliyokuwa ikisimamiwa na kitengo cha shin bet, bado hatua stahiki hazikuchukuliwa inavyopaswa.
Sasa basi huyu bwana Mordechai alikuwa akifanya kazi kwenye idara iliyojulikana kama "institute no.2" kama operator sehemu hii ya Dimona na department aliyokuwa akiifanyia kazi ilikuwa ya siri kiasi kwamba kati ya waajiriwa 2,700 waliokuwa eneo hilo la Dimona,ni 150 tu peke yake waliruhisiwa kufika kwenye institute no.2.
Kwa upande wa huyu jamaa ni kwamba alikuwa na vitambulisho viwili maalum au badge zenye namba maalum za kumruhusu kuingia eneo hili la Dinoma. Moja ya badge ilikuwa na namba 9567-8 iliyomruhusu kuingia eneo hilo la Dimona na nyingine yenye namba 320 ya kumruhusu kuingia kwenye jengo maalum lililopo chini kabisa ya ardhi ambapo ndipo institute no.2 inapatikana.
Kwanza kabla hatujaenda sana nikudokezee kitu. Eneo hili la Dimona ni kwamba majengo yake yalikuwa ya kawaida tu ila ni ya kisasa . Lilikuwa ni jumba la ghorofa mbili tu peke yake kiasi kwamba kwa mtu wa nje angedhania ni hoteli ya kawaida au duka kubwa lenye ghorofa mbili hivi . Ila kwa mtu mwenye akili ya udadisi angejiuliza swali inakuwaje nyumba ya ghorofa mbili inakuwa na Lift ya elevator wakati kwa nyumba kama hiyo haiitaji kuwa na lift. Sasa lift ya nini wakati ghorofa ya pili mtu hata mtoto anapanda kwa mguu na kushuka? Ni kwamba hiyo lift haikuwa ya kwenda juu bali kushuka chini ardhini kabisa huko umbali wa ghorofa 6 ambapo facility za kuchakata Uranium zipo huko na kuliitwa Institute no. 2. Na huku ndipo Mordechai Vanunu alikuwa akifanya kazi na alikuwa anazijua kona zote za mle chini.
Na kila floor ilikuwa na kazi yake na zilikuwa zimegawanyika kama ifuatavyo.
Floor ya kwanza kwenda chini ardhini ya eneo hili la Dimona lilitengwa special kama eneo la ofisi na idara kadhaa pamoja na cafeteria au mighahawa ya kupata mlo. Pia floor hii kulikuwa kuna upande uliotenganishwa na milango au mageti ambapo rods za uranium zilikuwa zikipitishwa hapo kwa ajili yakupelekwa kwenye kinu cha kurutubisha uranium yaani nuclear reactor.
Kwenye floor ya pili hapo palikuwa ni ukumbi maalum ambapo wageni maalum walioruhisiwa na wenye high level security clearance walikuwa wakitazama urutubishaji wa nyuklia ulivyokuwa ukiendelea chini huko na palijulikana kama Golda balcony. Eneo hili palikuwa kama ni control room ya mitambo yote ya eneo hili la Dimona.
Na kwenye floor ya tatu ilikuwa ni sehemu maalum ambapo wataalamu walikuwa waki size zile rods za Uranium kwa ajili ya kusimikwa kwenye kinu kwa ajili ya urutubishaji.
Kwenye floor ya nne sasa hapa ilikuwa ni eneo kubwa kiasi na lenye upana ambapo uchakataji ulikuwa ukifanyika.nyaani production plant na facility zingine zilikuwa zimesimikwa hapa. Na hapa sasa ndipo Element ya Plutonium inayozalishwa kwenye kinu cha kurutubisha uranium inapotengenezwa na kutenganishwa kutoka kwenye Uranium rods baada ya kufanyika uchakataji wa kufyonza Neutrons ndani ya kinu..... Kwa mliosoma chemistry kidogo hapa wanaelewa hili... Wazee wa half life particles and decay pamoja na Electrolysis 😎😎😎😎👊. Anyway acha tuendelee.
Kwenye floor ya tano ndipo zilipokuwa Labs maalum kuchakata na kuunda mabomu yenyewe ya uranium na floor ya sita ilikuwa ni sehemu special ya kukusanyia taka zote za eneo hili la kuchakata Uranium na kuhifadhiwa kwenye container maalum. Huo ndio mchanganuo kiufupi wa eneo hili.
Sasa tukiendelea , huyu Mordechai alikuwa mara nyingi anafanya night shift kama operator wa eneo hili la Institute 2. Na alikuwa anajua kila eneo kila idara na mchakato mzima wa kuunda hizi uranium bombs eneo hili.
Sasa siku moja huyu bwana pasipo sababu ya kueleweka alijikuta amekuja na camera eneo hili pasipo kushtukiwa ambalo haikuruhusiwa kifaa kama hicho eneo hilo. Na alihifadhi kwenye locker lake personal . Hakushtukiwa na yeyote wala walinzi wa eneo hili. Sasa wakati wa lunch ambapo kwenye institute 2 hakukuwa na mtu hata mmoja huyu bwana alikuwa akipiga picha sehemu zote zile nyeti za eneo hili la Institute 2 kuanzia maabara, production plant na facilities zingine zilizokuwa eneo hili. Michoro yote na ramani ya eneo hili zote alizipiga picha na hata alikuwa akiingia kwenye baadhi ya ofisi na kupekua baadhi ya documents na kuzipiga picha... Hakuna aliyemshtukia😳😳😳😳. One very big Mistake. Hili likapita.
Sasa basi baada ya miaka tisa ya kufanyia kazi eneo hili la Dimona institute huyu bwana Mordechai Vanunu alifutwa kazi mwishoni mwa mwaka 1985. Kibarua kikawa kimeota nyasi. Na sio kwamba alifutwa kazi kwa kukutwa na kosa lolote bali ilikuwa ni Azimio lilipitishwa ya kukata au kupunguza gharama za kuendesha kituo hiki cha Dimona.
Hata hivyo hakuwa peke yake na alipewa mshahara wa miezi nane kwa mkupuo pamoja na malipo 150% ya kusitishiwa mkataba wa kazi ambayo kitaalum wanaita severance package payment. Lakini licha ya hivyo huyu bwana hakuridhika sana na alikuwa amekasirika haswa. Aliamua kuchukua maamuzi magumu na kuamua kuuza kila kitu na kusafiri kwenda mbali .
Hivyo jamaa akaamua kuuza gari na nyumba yake kisha pesa yote akaitia kwenye akiba yake ya benki na kutokomea mashariki ya mbali. Kwanza alienda Russia akakaa kidogo kisha akaunga hadi Nepal. Hapo Nepal alitaka kubatizwa na kuwa buddha ila akakutana na totoz moja yenye asili ya ki Israel .. akajikuta amenogewa na penzi akajikuta hiyo ndoto ya kuwa buddha ikayeyuka ghafla.
Baada ya kukaa hapo nepal jamaa akaamua kusafiri Australia na huko alikaa kwa miezi kadhaa akifanya kazi za kawaida sana za hapa kule hapa kule. Katika harakati za kukaa hapo Sydney na anasa za hapa na pale hakuwa na makazi rasmi hivyo aliamua kwenda kwenye kanisa moja hapo jijini na kuamua kubatizwa kwenye kanisa la Anglican la mtakatifu George lililokuwa likiendeshwa na kasisi John McKnight.
Bwana Mordechai alijikuta amebatizwa kwa jina la john Crossman. Haya yalikuwa mabadiliko makubwa sana kwa huyu Mordechai. Kwanza mzaliwa wa asili ya Marrakech Morocco,aliyesomea shule za Talmud na yeshivahs zilizopo Beersheba Israel hakika yalikuwa ni mabadiliko makubwa ya kiimani.
Na sio kwamba mabadiliko haya yalisababishwa na uyahudi uliokuwa ndani yake au kuwa disappointed na kuachishwa kazi Israel bali ni hakuwa stable kifikra kutokana na tamaa yake ya kutamani maisha mazuri na Pesa.... 🤑
Sasa basi kwakuwa huyu jamaa Mordechai au John Crossman aliamua kumpokea yesu awe mwokozi wa maisha yake🤣🤣🤣 Alijikuta ametengeneza mazoea na waumini wenzake hapo church ambayo ni kawaida tu kwa mshirika yoyote yule. Katika mazoea haya alijikuta akiropoka shughuli alizokuwa akifanya huko Israel kabla ya kuja Australia. Mpaka alianza kutengeneza slide kama presentation za chuo kuwaelezea kiundani alichokuwa akifanya,maswala ya nuclear reactor kwenye eneo la Dinoma na kila kilichokuwa kikiendelea humo katika kutengeneza mabomu ya nyuklia 🥺😳😳😳. Sasa waumini wenzake walikuwa wanashangaa stori za huyu jamaa nini anachowaambia.. walikuwa hawaelewi jamaa anazungumzia nini. 🤣🤣🤣
Lakini katika kuwaeleza hayo yupo mshirika mmoja alivutiwa na stori za huyu jamaa Mordechai alichokuwa akikieleza kuhusiana na utengenezaji wa silaha za nyuklia za Uranium.🤔🤔 Huyu bwana alikuwa ni oscar Guerrero raia wa Colombia ambaye kitaaluma alikuwa ni mwandishi wa habari.
Huyu bwana Guerrero kwakuwa alikuwa akikaa apartment mmoja na Mordechai alijaribu kumweleza jinsi angetengeza pesa ndefu kwa picha alizopiga huko Dinoma kwa kuziuza kwenye magazeti au kuziuza kwenye kituo cha televisheni🥺🥺.
Ushauri huu Vanunu aliupokea ila kwa mashaka sana endapo siri ya utengenezaji wa silaha za nyuklia ulivyokuwa ukiendelea Israel ikajulikana duniani nini kingemtokea yeye binafsi na pia kwa Israel. Alibaki kwenye dilemma. Na Mordechai aliamini hata picha hizi zikitoka atakuwa ameionyesha dunia kwamba kumbe hata Israel ilikuwa ikijihusisha na kutengeneza nyuklia .
Kwa kusitasita na kishingo upande Mordechai na huyu bwana Guerrero walikwenda moja kwa moja hadi kwenye studio moja ya kusafisha picha iliyopo hapo Sydney kwa ajili ya kuzitoa picha alizokuwa nazo kwenye mkanda wa camera kisha na kwenda kuzipeleka kwenye ofisi za gazeti moja la hapo mjini zilizokuwa zikimilikiwa na Wamarekani na pia wakazipeleka picha zingine kwenye vituo vya runinga . Lakini kote huko walionekana ni wahuni wawili tu amabao wamekutana na wanataka kutengeneza pesa rahisi kama za wale wauza makopo na scrapes😆😆😅. Laiti wangejua picha hizo zilikuwa ni Siri nyeti zilizofichwa kwa gharama kubwa ,wasingezidharau.
Hilo likapita. Sasa ikatokea kwamba huyu Guerrero rafiki wa Mordechai akasafiri kwanza uhispania kisha hadi London uingereza . Na huko Akakutana na wahariri wa gazeti la Sunday Times kisha akawaelezea stori kuhusu hili jambo la Israel kumiliki kinu cha nuclear na pia kuna picha za eneo hilo la Dimona kama ushahidi. Hivyo wakakuta stori ya huyu Guerrero kama inaweza kuuza kwenye magazeti ila ilibidi wawe makini kuepuka kuzusha mtafaruku wa kimataifa maana swala la kuwepo kwa kinu cha nyuklia ndani ya Israel haikuwahi kusikika popote pale. Hivyo walimtaka Guerrero apitie vizuri stori hii na kuidhibitisha kabla ya kuchapishwa.
Sasa na wakati huo hili likiendelea, Afisa mmoja wa kituo cha televisheni kwenye mji wa Canberra Australia aliamua kuwasiliana na balozi wa Israel nchini Australia ili kumuuliza kwamba kama ni kweli picha zilizoletwa kwenye kituo chao na "MTU"(Mordechai Vanunu)mmoja kama kweli amewahi kufanya kazi ndani ya Dimona institute. 🤔🤔🤔😳😳.
Ghafla stori hii ikatua kwa mwandishi mmoja wa habari wa Israel hapo Israel kisha akatuma ripoti hii hadi Israel na kuripotiwa kwenye gazeti moja la mjini tel Aviv. Wee! Wee! Wee! 😶🌫️😶🌫️😱😱😱. Kama mlipuko au ngurumo za radi habari hizi zikatikisa vyombo vya usalama vya Israel kwamba: A FORMER
OPERATOR AT INSTITUTE 2 IN DIMONA WAS TRYING TO SELL ISRAEL MOST VITAL SECRET .
Lilikuwa ni pigo moja takatifu kwa idara ya usalama ya Israel haswa kutokana na ukweli kwamba siri waliyokuwa wakiilinda kwa gharama kubwa kuvujishwa na mfanyakazi wa zamani wa DIMONA.
Habari hizi zilifika mezani kwenye ofisi ya P.M wa Israel wa wakati huo bwana Shimon Peres. Ikatolewa amri moja tu kwamba bwana Mordechai Vanunu atafutwe na aletwe hadi Israel na awaelezee alizitoa wapi picha hizo😅😅🤣. Baadhi ya wasaidizi wa huyu waziri mkuu walitoa wazo la kwamba huyu Mordechai auliwe 🔫 lakini Azimio hili halikupitishwa.
Faili la maagizo ya kutafutwa kwa Mordechai Vanunu yakatua mezani kwa mkurugenzi wa Mossad wa wakati huo bwana Nahum Admoni.
Nikudokezee tu jambo kidogo kuhusu kipindi mossad ikiongozwa na huyu bwana miaka hiyo ni kwamba, ilikuwa ni kipindi cha kuanzia 1982-1989 ambapo Shirika la mossad lilipitia kwenye misukosuko kadhaa iliyoisababishia kashfa ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Moja ya misukosuko waliopitia Mossad, ni pale majasusi kadhaa wa Israel kukamatwa nchini marekani na baadhi ya nchi zingine wakihusishwa na kufanya espionage kwa ajili ya Israel na kashfa mbaya zaidi ni kumhusu huyu mjuna wetu tunaemjadili hapa bwana Mordechai au John Crossman baada ya kuvujisha picha za Dimona Facility. Hii ilionekana Mossad wameshindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo. Sasa basi ikawa kwamba Mossad tena ikapewa jukumu la kumnasa huyu bwana. Na operation hii ilijulikana kwa jina la uficho "KANIUK".
Sasa basi kikatumwa kikosi kazi "MAALUM" au special unit cha Mossad hadi Australia ili kumnasa huyu Mordechai. Ila kikosi kazi hiki kilifika "too late", Mordechai alikuwa ameshaondoka na kuruka hadi London uingereza.😁😁🤣
Huko uingereza bwana Mordechai alikutana na waandishi na mabosi wa gazeti la Sunday Times la hapo London kutaka kujua ukweli haswa kuhusiana na uwepo wa mitambo ya kutengeneza nyuklia ndani ya Israel. Alihojiwa haswa huku baadhi ya wanasayansi na wataalamu wa uingereza wakizipitia na kuzichambua picha alizopiga huyu bwana kujiridhisha kwa kile alichokuwa akisema bwana Mordechai.
Mordechai alifunguka ukweli wote kuhusu Dimona institute na zaidi alizidi kuropoka na kusema kwamba ISRAEL wanatengeneza pia bomu la neutron lenye uwezo wa kuua kila kiumbe hai pasipo kugusa na kuharibu majengo au miundombinu yoyote ile. 😱😱
Lakini katika kuropoka kote huku huyu bwana alikuwa na wasiwasi sana na hofu kuhusu maisha yake. Hata wamiliki na wahariri wa gazeti la Sunday Times walijaribu kum-cool down ila bado akawa na wasiwasi. Akiishi hoteli ,mara kesho ahame akakae hoteli nyingine, ilimradi tu atulize akili. Staff wa kampuni hii ya gazeti la Sunday Times ndio waliokuwa wakimhudumia kwa kila kitu kwenye hotel aliyokuwa akikaa.
Na la zaidi alipewa ofa ya donge nono sana la dola laki moja cash money 💰 💰 💰 💰 kama shukrani na malipo ya stori yake pamoja na picha alizopiga huko kwenye institute 2. Pia alilipwa asilimia 25 ya hakimiliki ya stori yake hij kuchapishwa kama kitabu na asilimia 40 ya kuchapishwa kama makala kwenye magazeti.😋😋. Pia mmiliki wa gazeti la Sunday Times ambaye alikuwa anamiliki kampuni ya kutengeneza filamu ya Twentieth Century Fox walitaka kutengeneza filamu kuhusiana na hii stori yake ambapo steringi ambaye angeigiza kama Mordechai Vanunu Angekuwa Robert de Niro.
Hakika Mordechai aliangukia bahati . Na hapo London kila starehe na anasa alizotamani kwenye jiji hilo la malkia ,wenyeji wake walimpatia. Ila starehe moja tu aliikosa na alikuwa akiitamani. "MAPENZI NA JOTO LA MWANAMKE". Alitamani kuwa na mwanamke🥰🥰🥰♥️♥️♥️. Hata mmoja wa wafanyakazi wa Sunday Times aliyejulikana kama Rowena Webster aliyekuwa akimpa kampani jamaa alipoombwa mzigo akamgomea lilimuumiza sana. Wanawake walikuwa ni kama dozi ya paracetamol ya kutuliza maumivu kwa huyu bwana.🤣
Kosa moja walilolifanya hawa wamiliki wa gazeti la Sunday Times ni kutotambua kwamba huyu mgeni wao kwa vyovyote vile angetafutwa na Israel na hata kuuawa. Kosa pa pili walilofanya ni kumtuma mmoja waandishi wa habari wa Sunday Times hadi Israel ili kudhibitisha yale yote kuhusiana na bwana Mordechai na kuhusiana na uwepo wa kinu cha kurutubisha uranium ndani ya Israel.
Mwandishi huyu baada ya kufika Israel na kukutana na mwandishi mwingine wa hapo Israel kuhusiana na bwana Mordechai kama yote ni ya kweli, huyu mwandishi akawasanua kitengo cga usalama wa ndani wa Israel cha shin bet au Shabak kwamba Mordechai yupo London tena akiwa chini ya usimamizi na gharama za kampuni ya Sunday Times.
Ndani ya masaa machache kikosi kazi cha Mossad kilikuwa kimeshatua London 😆.
Muda si muda majasusi wawili wa mossad walikuwa tayari wamekita kambi kwenye majengo ya ofisi za Sunday Times wakijifanya wapiga picha . Lengo lao ni kumnasa Vanunu Mordechai. Sasa siku hiyo hawa majasusi wa Mossad walifika kama waandishi wa habari na wapiga picha wakitaka kuchukua habari za mgomo wa wafanyakazi uliokuwa ukiendelea na kweli katika kuchukua Matukio ya picha walimnasa Mordechai Vanunu kwenye picha .
Sasa kazi iliyobaki ni kumfuatilia kwa siri Huyu Mordechai kwenye mitaa aliyokuwa akikatiza ndani ya London ili waweze kumnasa . Pia walikuwa wanahakikisha wanatambua mitaa yote na Maeneo yote Vanunu aliyokuwa akipendelea kutembelea mara kwa mara na kufika hapi kabla ya yeye kufika. Mbinu hii ya kijasusi ya kumfuatilia target au mhusika kwa ujumla wake hujulikana "Combing method" ambapo anayefuatiliwa hujulikana movements zake zote ikiwemo atakuwepo wapi, mda gani na possiblity ya watu atakaowakuta hapo n.k na atakula nini ,ataondoka saa ngapi na atatumia usafiri gani n.k.
Sasa basi mwezi September tarehe 24 , Mordechai alifika kwenye makutano ya barabara ya Leicester Square , eneo maarufu ambalo watalii hupendelea kufika. Kwenye eneo moja la kununulia magazeti, bwana Mordechai alimwona mrembo mmoja amesimama hapo. Jamaa akajisogeza ili apate kununua gazeti na zaidi aweze kumtongoza huyu mrembo baada ya kumwangalia kwa muda mrefu.
Jamaa kwa kusita alianza kufunguka kwa mrembo .
Alimwomba waongee na mrembo bila hiyana akakubali.
Katika kujitambulisha mrembo alisema yeye anaitwa Cindy akitokea Marekani kwenye mji wa Philadelphia na yupo ulaya kwa vacation 🥰🥰. Mungu ampe nini tena bwana Mordechai Vanunu au bwana John Crossman?
Kwanza ikumbukwe muda huu ambao jamaa akibembeleza mapenzi ,kampuni ya Sunday Times iliamua ku delay kuchapishwa kwa habari alizozitoa Vanunu kuhusiana na kilichokuwa kikiendelea Israel kuhusu Dimona institute. Hii ni kupata uhakika pasipo na shaka na zaidi ni kuhakikisha bwana Mordechai asingeweza kuingia matatizoni. Lakini tayari bwana Mordechai alikuwa yupo bize kubembeleza mapenzi huko Barabarani 🤣🤣.
bro wetu Mordechai kutokana na kumwelewa mrembo na mrembo akawa kama AMEMWELEWA jamaa , alijikuta akimweleza maswahibu yote ili apewe faraja na mrembo huyu kwa jina la Cindy. Mrembo akamshauri aende hadi Marekani pengine ataweza kupata usaidizi na akauza stori yake na akapiga pesa.. jamaa akakataa. Alichokuwa akitaka kwa muda huo ni mapenzi tu kutoka kwa Cindy 😅😅🥰
Siku kadhaa zikasogea , Mordechai na Cindy kwenye mitoko ya hapa na pale hadi kuangalia movie pamoja huku mabusu motomoto 💋 💋 💋 😘 😘 akipokea bwana Mordechai kutoka kwa mrembo Cindy.
Sasa siku moja Mordechai akaomba mzigo kutoka kwa Cindy, madam akakataa katukatu. Sababu aliyoitoa ni kwamba asingeweza kulala naye kwakuwa chumba alichokuwa akilala cha hotel ana share na rafiki yake wa kike hivyo asingeweza kumkaribisha jamaa🥺🥺🤣🤣😆.
Demu akamwambia Mordechai kama unataka kulala na mimi na ku enjoy mapenzi na mahaba motomoto afanye hivi waende hadi Rome italia kwenye apartment ya sista yake anayeishi huko😁😁😅. Ili waweze kuenjoy mapenzi kwa uhuru kabisa..jamaa Mordechai kwanza alisita lakini baadaye alikubali baada ya madam kununua ticket ya ndege ya first business class ya kwenda huko. Naye jamaa ikabidi akubali na demu akamnunulia tiketi ya ndege ili wasaidizi hadi Rome italia.
Maskini Mordechai..... 😱😱😱😱🥺🥺🥺🥺🥺🥺🥺🥺🥺🥺 Kwisha habari yake . Ashki na Ny¥∆§£g zake zikawa zinamponza na kujipeleka kichinjioni in the name of MAPENZI. Hakujua huu ulikuwa HONEY 🍯 🍯 TRAP 🪤 🪤 🪤.
Huyu bwana Angekuwa anatumia akili zake vizuri kwa mtu makini angetambua mapema huu ulikuwa mtego ,tena mtego mbaya sana unaotokana na udhaifu wa tamaa zako..
Demu inakuwaje mna date naye almost wiki na zaidi..mnafanya kila kitu ,sex hakupi ila kisses za hapa na pale then anakwambia ili tutimize tendo lazima wasafiri tena nje ya nchi kabisa demu mwenyewe hamjajuana kiundani kivile... Kirahisi tu mwanamke akwambie hatuwezi ku sex London ila mnaweza ku sex Rome Italy HOW?🤔🤔 Na ticket ya ndege unanunuliwa?
Hapo kabla , kabla huyu jamaa hajakolea kwenye penzila mtoto Cindy alikuwa amekwisha onywa na baadhi ya watu kwenye kampuni ya Sunday Times kuhusiana na harakati zake za mapenzi awe makini kidogo . Alijaribu kuonywa asijaribu kuondoka London kwa hizo siku chache alizosema anaenda vacation na mrembo wake na akaambiwa hata passport yake ya kusafiria asijaribu kuacha kwenye mapokezi ya hotel aliyokuwa akikaaa...Wooi... It was too late jamaa hakusikia aliamua kusafiri kwenda Rome kula utamu 😋♥️ . Mtego huu................