The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 10,433
- 13,417
Babu yangu alikuwa na wake watatu kupitia dini yetu ya asili inayoruhusu wake kulingana na uwezo wa kipesa na kingono, nikiwa mdogo nilibahatika kuwaona maisha yao, babu yangu alikuwa ana ukwasi kwa level za kijijini kila mke alimjengea mji wake na duka nje cha ajabu tuliishi kwa amani sana wajukuu tulikuwa tukiamua kulala kwa bibi mkubwa wote tunalala huko.
Mimi nilitokana na mke wa tatu ambaye babu alimpenda zaidi nadhani ila kimatumizi alikuwa hawagawi kabisa ukiacha maduka aliyoyaacha chini ya uangalizi wao alikuwa ana fiat mbili za kusomba mazao kwenda Dar akirudi na mikate, nanasi, samli, vitenge (havikuwepo mkoani kwetu) anagawa kwa usawa, aliweza kuwalea watoto kupendana wakawa wajasiliamali wazuri na 70% ni matycoon alifariki kabla ya wakeze akiacha mali bila migogoro kwani aliandika usia kila mke na mji wake na watoto wake.
Mpaka leo tunaishi kwa upendo na yeye ndo nguzo yetu, aidha wake wawili wa mwisho aliwakuta wameshazaa bila ndoa na aliwaoa na maisha yangu yote sikuwahi jua baba zangu wengine si wanae hadi namiaka 20, sasa cha ajabu wakati anafariki aliacha usia huu kwa baba zetu juu ya maisha ya ndoa:
1. Alisema katika dunia hakuna mtu muhimu kuliko mke/mumeo.
2.Hakuna zawadi unayoweza mpa mke kuzidi kuwapenda na kuwalea vyema watoto wake.
3.KAMWE USIOE MKE ZAIDI YA MMOJA, AKARUDIA KWA KILUGHA ''SIVO SIVO NDEPELILE''
Sasa wakuu huwa najiuliza kuna nini kwenye ndoa za mitara alichokiona babu?