Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Sherehe ya ndoa ina gharama!!kwani ndoa ina gharama? ama nyie ndio mnaleta gharama.... nijuavyo mimi.. ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili ambayo kawaida hua mbele za MUNGU akiwakilishwa na viongozi wa dini.. sasa hizo gharama mnatoa wapi?
Kwanza kabisa naanza kwa kusema swala la kuishi na binti kabla ya ndoa kwa kutegemea uwepo wa ndoa ni kiasi kidogo sana inawezakuwepo ndoa.
....:::Mtazamo::....
Swala la ndoa ni jambo lenye mapana yake tukianzia kwenye msingi wa kiimani(dini) ama vinginevyo.
Kimsingi ndoa huwa nikama fumbo na ndiyo maana hauwezi kumjua utakae muoa ni yupi, unaweza kutembea na wanawake zaidi hata ya mia mbili lakini usioe hata mmoja yule wa mia mbili na moja ndiyo ukamuoa.
Ebu nianze kama nilivyo toa mfano hapo na kuiita ndoa ni fumbo, ninapolinganisha ndoa na fumbo nafikiri naeleweka vizuri sana,, kimsingi unapokuwa na binti katika mahusiano halafu ukategemea ajekuwa mkeo wakati huo mmeshaanza kuyatengeneza maisha yenu katika mfumo wa ndoa(fumbo) na kujamiana ni kama kujitungia mtihani ukaujibu na kujisahihishia mwenyewe, kisha ukaenda kumuongopea mtu kwa umefauru...
Hapana nimelizungumzia hili jambo katika mtazamo wa kaiwaida tu bila kuhusisha imani(dini) yoyote ile nitarudi..
Bado hujaeleza ni kivipi kuishi pamoja kunasababisha wanaoishi kutooana
Hapa naona umeweka maelezo ambayo hayajibu hoja husika!
....:::Naam::.....
Nilitoa kama utangulizi hapo ili nitakapoanza kutoa maelezo yaende ndani ya kile nilichotangulia kusema..
Unapokuwa na binti katika mahusiano ya kimapenzi kiujumla inapunguza ile hamasa ya kuitamani ndoa sababu tayari mnakuwa mmeshajuana, na msingi mkubwa wa hayo mahusiano kwa wakati huo unakuwa ni ngono. Ni swala ambalo nikowazi kabisa thamani ya mahusiano ya watu wanaofanya tendo na wasio fanya ikotofauti kabisa,,inapotokea mkajuana thamani ya mwanzo inakuwa sio sawa,,hapa ni sawa kusuburia chakula kati ya mtu mwenye njaa kabisa na mtu ambae ameshaweka tonge mbili mdogomo japo hajashiba.
Angalizo; Nipinge kwa hoja sio maswali, sikatai maswali lakini ni vizuri tukapingana kwa hoja ili tuweze kutengeneza mtililiko mzuri wa majadiliano,,maswali yasichukue sehemu ya hoja.
Kwani mkuu thamani ya ndoa ni vitu vingapi?
Kuishi bila ndoa ni uChungu na propability ya kuoana ni ndogo
Kwanza kabisa naanza kwa kusema swala la kuishi na binti kabla ya ndoa kwa kutegemea uwepo wa ndoa ni kiasi kidogo sana inawezakuwepo ndoa.
....:::Mtazamo::....
Swala la ndoa ni jambo lenye mapana yake tukianzia kwenye msingi wa kiimani(dini) ama vinginevyo.
Kimsingi ndoa huwa nikama fumbo na ndiyo maana hauwezi kumjua utakae muoa ni yupi, unaweza kutembea na wanawake zaidi hata ya mia mbili lakini usioe hata mmoja yule wa mia mbili na moja ndiyo ukamuoa.
Ebu nianze kama nilivyo toa mfano hapo na kuiita ndoa ni fumbo, ninapolinganisha ndoa na fumbo nafikiri naeleweka vizuri sana,, kimsingi unapokuwa na binti katika mahusiano halafu ukategemea ajekuwa mkeo wakati huo mmeshaanza kuyatengeneza maisha yenu katika mfumo wa ndoa(fumbo) na kujamiana ni kama kujitungia mtihani ukaujibu na kujisahihishia mwenyewe, kisha ukaenda kumuongopea mtu kwamba umefauru...
Hapana nimelizungumzia hili jambo katika mtazamo wa kaiwaida tu bila kuhusisha imani(dini) yoyote ile nitarudi..
Soon utakuwa mke wangu kama hauko kwenye ndoa usijali...!
Kwanini unampa hongera?
uKwa upande wa wakristu amri ya 7 inasema...................................
Kwa ndungu zetu waislamu wanasema usiikaribe dhinaaa........................................
Kazi kweli kweli............................kuuona ufalme wa allah ni kazi
Siku hizi watu wanachukuana wanazaa baadaye ndiyo ndoa,inaitwa kupasha kiporo.
Umesoma angalizo nililoweka hapo chini? iko hivi mtu anapokujibu swali kwa kutoa maelezo halafu wewe ukaanza kuchambua maelezo yake na kuuliza viswali visivyo jenga mantiki nzima ya kile unachotaka kusema nikama unakuwa umepungukiwa hoja..
Ngoja nikujibu kifupi tu.
Thamani ya ndoa haihusiani na vitu.