Utamkumbuka Samia kwa yapi?

Utamkumbuka Samia kwa yapi?

Ukiachia mbali hayo ongezea pia atakumbukwa kwa damu zilizomwagika wakati wa uchaguzi ambapo watu wengi waliuawa na wengine hadi leo familia zao hazijapata miili ya ndugu zao

Pia, kutekwa na kupotezwa kwa watu wote waliojaribu kumkosoa au kupinga utawala wake

Tuhuma za ufisadi na matumizi ya fedha za umma huku kukiwa na madai na ushahidi unaotajwa kuhusu mwanawe kipenzi yule Waziri wa Ulinzi mwanamke na mkuu wa majeshi
Ushahidi uliwekwa hadharani

Pia, mikopo mikubwa aliyoingia pamoja huku kukiwa hakuna miradi ya maendeleo inayoonekana kutokana na pesa za mikopo hiyo na mengine mengi 🤝
Kabisa, japo binafsi siamini kama anapaswa kubeba lawama peke yake kwenye masuala ya demokrasia.

Ni hicho chama kizima chenye falsafa za Mao kutoka kwa Nyerere.

WanaCCM wakubwa wanaamini chama kinakuja kabla ya nchi.
 
Hapa tunamzungumzia yeye kama mtu mwenye kauli ya mwisho kwenye nchi hii I mean Final Say
Kama Amiri Jeshi Mkuu anabeba dhamana na uwajibikaji wa mwisho kwa maamuzi na matendo ya utawala wake usijaribu kulemba mwandiko kijana

Hivyo lawama za kisiasa kuhusu yaliyotokea haziwezi kumkwepa
Hili halina haja ya kupepesa macho
 
Kafungua milango ya elimu, Diploma wanapata boom siku hizi,

Samia scholarship inawafunulia milango masikini wenye vipaji,

Chini ya mradi wa HEET vyuo vimepata miundombinu mbali mbali na kuongeza huduma na ufanisi,

Mitaala mipya imeletwa(japo changamoto hazikosekani) ila nimefurahi naona hata vitoto vya darasa la 3 vinasoma TEHAMA.

Fimbo zimepigwa chini...

Mazuri ni mazuri, na yanastahili pongezi.
Samia kwenye swala la TEHAMA kwenye elimu, Afya, mpaka data center,etc yuko vizuri ✅
 
MImi ni kati ya walioumizwa sana na jinsi Samia alivyobadilishwa na waovu kwa kasi ya ajabu. Kwa namna alivyoanza, sikuwahi kudhani kama angeweza kubadilika japo kufikia hata robo ya mahali alipofikia. Kuna wakati nilipokuwa nikitoa maoni yangu kumsifu kwa baadhi ya kauli zake kwenye mwelekeo wa haki, kuna watu waliokuwa na misimamo tofauti, walifikia mpaka kunisema vibaya, niliwaona ni wehu. Lakini kwa tulipofikia sasa, ndiyo najiona nilikuwa mjinga kuweka imani kubwa kwake, kumbe ni mtu ambaye hakuwa akiyanena yaliyokuwa nafsini mwake, labda yaliyokuwa yakitoka kinywani mwake ilikuwa ni hadaa. Samia ambaye kadhaa aliwalaumu polisi waliokuwa wakiwaonea watu, na hata kuwaua mahabusu, leo anawasifia kwa kuwaua wananchi holela! Ni ajabu kubwa!!
 
Hapa tunamzungumzia yeye kama mtu mwenye kauli ya mwisho kwenye nchi hii I mean Final Say
Kama Amiri Jeshi Mkuu anabeba dhamana na uwajibikaji wa mwisho kwa maamuzi na matendo ya utawala wake usijaribu kulemba mwandiko kijana

Hivyo lawama za kisiasa kuhusu yaliyotokea haziwezi kumkwepa
Hili halina haja ya kupepesa macho
Siamini kama ana kauli ya mwisho(Naweza nikawa nakosea).

Nazidi kugundua kwamba, kwenye tawala za kidemokrasia, mara nyingi rais sio msemaji wa mwisho.

Siamini kama ana kauli ya mwisho(Naweza nikawa nakosea).

Nazidi kugundua kwamba, kwenye tawala za kidemokrasia, mara nyingi rais sio msemaji wa mwisho.

View attachment 3708425
Sasa kama hana kauli ya mwisho
Mbona alisimama akasema mimi ndio rais na amiri jeshi mkuu

Unavyotaka kumsafisha ni ngumu sana hasafishiki yote yalioyotendeka na yanayoendelea kutendeka ni chini ya utawala wake over
 
Simsafishi...

Ila yanayotokea ni matokeo ya mfumo flani kuendekezwa.

Na bila mfumo huo kuondolewa, mambo kama haya yatajirudia tu.

Wanaharakati wanapotosha watu. Wanamuongelea yeye tu. Tundu Lissu ndo yupo vizuri ameweka wazi tatizo la mfumo mzima.
 
Kafungua milango ya elimu, Diploma wanapata boom siku hizi,

Samia scholarship inawafunulia milango masikini wenye vipaji,

Chini ya mradi wa HEET vyuo vimepata miundombinu mbali mbali na kuongeza huduma na ufanisi,

Mitaala mipya imeletwa(japo changamoto hazikosekani) ila nimefurahi naona hata vitoto vya darasa la 3 vinasoma TEHAMA.

Fimbo zimepigwa chini...

Mazuri ni mazuri, na yanastahili pongezi.
Hii mbona kama DNA ya Lucas
 
Hawezi kuhimili negative criticisms.
...kwa udhaifu wake anahisi hadi serekali yake inaweza pinduliwa na mtu mmoja.
 
Timu ya mawakili kusikiliza kero za wananchi; nchi nzima. Huu ndio ulikuwa mlango wa kupata haki zetu kwa sisi tuliodhulumiwa
 
Kwa mengi mazuri!!aiseh Kuna ile arosto ya 2014-2021,hakuna kupanda cheo!!aiseh alipoingia mzigo ulisoma mara mbili chap chap 2021,2024!!

Ile shoot to kill,alishafundishwa na watangulizi wake kina mkapa kule Zanzibar 2001,hii ya juzi ilikua marudio TU,sema kwa vile ilitokea huku,kule Zanzibar walishazoea MAZOMBI huku tunaanza kuzoea WASIOJULIKANA NDIO MAZOMBI ya huku,ndio maana kelele zimekua nyingi,ni Yale Yale tu SEMA hatujazoea!!!

uchaguzi wa 2025,ulikua na noti aiseh,kweli tuliitwa maafisa uchaguzi ,ile kauli mbiu ya kazi na utu tuliiona kupitia KAZI NA NOTI.

Kazi na utu,tunasongambele!!!
 
Back
Top Bottom