Father of All
JF-Expert Member
- May 30, 2026
- 475
- 863
Rasmi, Tundu Lissu ni mfungwa. Je, hii imelenga kumzuia kugombea tena urais? Hivi, Samia anafaidikaje na ukatili na uvunjaji sheria huu ulioandamana na ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.
Kwa wale wenye mawazo kama yangu kuwa haki haikutendeka, mnaweza au mnataka kumshauri nini rais Samia? Nini afanye kuondoa huu upuuzi na uvunjaji wa haki za binadamu na upindishaji sheria kwa kutumia kwa upendeleo wa kisiasa?
Kwa namna Samia alivyojionyesha na kujifanya kumjali mbali na kumhaidi Lissu wangeyamaliza, amejionesha kuwa ni kigeugeu asiyepaswa kuaminika? Je, Lissu amefungwa kwa ajili ya Samia kutaka mwaka 2030 kutuletea kibaraka chawa wake? Je, nini kifanyike kuzuia hii hujuma dhidi ya taifa? Maswali ni mengi kuliko majibu ila Watanzania, naamini, mna majibu yake sahihi.