Utamfanyaje mtu anayeongea kwa sauti kubwa!

Nachukia kweli hio tabia. Sipendi zogo wala makelele na nahisi yananidhuru hasa.

Utakuta mtu anaongea kwa makelele, akiskiliza radio au kuangalia tv sauti Mpk nyumba ya kumi unaskia. Milango inabwatwa hadi roho inaruka. Yani kama ni wako wa karibu inabidi tu uvumilie but kusema kweli inaudhi
Hasa kwa sauti ya mziki hata kama ni mtu wangu siwezi kumvumilia
 
Na inakera zaidi ukute umepiga white shirt yako safi jitu linakuchafuwa kwa kukushika.

Yupo mwingine huyo funga kazi maongezi yakinoga ukiingia mkenge wa kugongeana naye anaweza kukuteuwa mkono, mimi huwa nauwahi mkono hukohuko juu kabla hajaushusha kwa nguvu ili kupooza speed na weight yake.
hahahahah lol!et unafanya kuwahi mkono juu kwa juu, mie hoi kwa kicheko huhuhu!
 
Hahhaaaa....hata shemeji yako anaongea kwa sauti kweli but huwa najitahid kumshusha angalau kidogo..

Sema naye taratibu kwamba kuna behaviour zake huzipendi halafu wakati huohuo mpe sifa pia eneo analoperfom vizuri, nina uhakika hatojisikia vibaya.

Sumu ya mwanaume usimseme tu kwenye udhaifu ila mweleze pia anavyokufurahisha hata akivaa vizuri au akijipulizia perfume fulani unajisikia raha sana.

Wanawake mkifanikiwa kutujuwa wanaume japo robo basi utashangaa kabisa hakuna uchawi wala ndumba.
 
hahahahah lol!et unafanya kuwahi mkono juu kwa juu, mie hoi kwa kicheko huhuhu!

sasa wewe mtu ameshiba vilivyo na mkono wake una afya tele unadhani utasubiri aliinuwe kono lake kutoka juu halafu wewe umetegesha mkono wako chini ili mgongeane hivi unajipenda kweli?
 
Umenikumbusha enzi cjaolewa kuna kaka mmoja alikuwaga anantongoza ila alianzia kweny kabla hajapata nafasi ya kukaa na mm anishushie mistari face2face, bwana cku niliyokutana nae nilijuta kila aliekuwa eneo lile alijua natongizwa huwa siisahau ile aibu

Waw! Nice story umewah kuikata bana. Mwisho wa siku ilifanikiwa au la manake nahis huenda ilikubidi kumkubalia mapema angalao kufupisha muda wa hiyo aibu. Teh teh teh...
 
fanya hivi mkuu:
1: Nunua hearing protector (e.g Ear plugs, Semi-insert ear plugs, Ear muffs)jamaa anapokuwa anaongea ww vaa hearing protector then sauti yake haitakuharibu unaendelea kufanya yako....
2. mfunge huyo jamaa voice controller, ukiona sauti kubwa unapunguza au ukiona ndogo unaongeza kiasi...
3.Akisumbua zaidi una mmute:redface:...
 
Nilipokuwa shuleni zamani mtu akiongea hivo wengine wanaanza kujifanya wameshika remonti wanapunguza volume,basi mhusika akiona hivo anakata tamaa,sasa kwa maofisini au sehemu zilizotulia na zenye heshima lazima na wewe itakubidi usimdiscourage kivile yaani unajifanya hauonyeshi ushirikiano mpaka anakata tamaa
 
Mwambie akuonyeshe KITUFE chake cha kupunguza sauti ili uipunguze......sasa hatujui kipo wapi maana kila Redio kinakuwa kipo mahali pake inaweza kuwa juu, chini ,nyuma, mbele au katikati...kama vipi muulize.
 
Sema naye taratibu kwamba kuna behaviour zake huzipendi halafu wakati huohuo mpe sifa pia eneo analoperfom vizuri, nina uhakika hatojisikia vibaya.

Sumu ya mwanaume usimseme tu kwenye udhaifu ila mweleze pia anavyokufurahisha hata akivaa vizuri au akijipulizia perfume fulani unajisikia raha sana.

Wanawake mkifanikiwa kutujuwa wanaume japo robo basi utashangaa kabisa hakuna uchawi wala ndumba.

Hahahaahaaaa...nimeshamjulia jinsi ya kumshusha hanipi karaha naona rahaaaa tu sasa

Uchawi na ndumba lazima uhusike kuimarisha koloni..kwikwikwi.....
 
Aisee kuna rafiki yangu hata tukiwa wapi hawezi kuongea kistaarabu kwa sauti ya chini,yaani hata kama kuna watu wengi unaona kabisa anaboa.Na ukimwambia haelewi ni kama unamwudhi tu ukimpa ukweli,kwa mliokutana na watu kama hao huwa mnachukuliana nao vipi?

huyo rafiki yako ana tatizo la kutosikia vizuri
 
Kuna lijamaa flani lipo bank flani hapa mjini (tena intaneshno benki) lipo front office, hilo jamaa hua linaongea kwa sauti kubwa mno. Ukiwa nje kabla hujaingia section yao unasikia mayowe kwa nje akiongea na subordinates wake. Wateja tukiiungia sasa ndo balaa...linaanza kubwata bwata hovyo maneno kibao tena kwa sauti kubwa sana. Linapenda kijisifu na kuwagombeza subs wake akiona wateja. Kazi hafanyi kazi kupiga domo tu.! Kelele mtindo mmoja!
 
Watu kama hao tabu tupu hata huwezi kuongea nao personally
 
Aisee kuna rafiki yangu hata tukiwa wapi hawezi kuongea kistaarabu kwa sauti ya chini,yaani hata kama kuna watu wengi unaona kabisa anaboa.Na ukimwambia haelewi ni kama unamwudhi tu ukimpa ukweli,kwa mliokutana na watu kama hao huwa mnachukuliana nao vipi?

Kama Nape Nnauye?
 
Hili ni tatizo na watu wa namna hii hawanaga siri kwenye kuongea.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa hajatulia kabisa kwenye ndoa. Siku moja tukiwa naye kwake nyumbani na familia yake tumekaa sebuleni simu ikapigwa. Jamaa kachukua simu faster katoka barazani kuongea. Kumbe kuna kademu kamemdanganya kana mimba yake akawa anatoa matunzo kumbe demu kampiga changa la macho ili azikusanye za kutosha.

Jamaa alivotoka nje akapayuka kwa sautikubwa sana akidhani ananongona. " Switie umenidanganya una mimba yangu nimekuhudumia muda wote kumbe umenidanganya" Nilikuwa na watoto wake na mkewe sebuleni ilikuwa aibu. Kilichoendelea baada ya hapo ngumu kuelezea.
 
mkuu hiyo ni kweli kabisa,kweli hawa majamaa wanaoongea kwa sauti huwa hawana siri
 
huenda hasikii vizuri . kwani hiyo ni ni moja ya dalili za uziwi/kusikia vziri
 
Back
Top Bottom