Utamaduni wa kuvishana pete

Utamaduni wa kuvishana pete

Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.
Pete huvishwa mbele ya kadamnasi ili kuanza kujiwekea kinga ili kuzuia wanyakuzi dhidi ya yule uliyemchagua ktk wengi. Pia si lazima mhusika avishwe baada ya kutoa mahari. Na mwanaume kumpigia goti mwanamke wakat wa kumvika pete ni ishara ya heshima kuwa umemfanya awe km dunia jinsi ilivyo beba kila kitu ukionacho hapa ardhini, hivyo ni heshima ya hali ya juu sana.
Naona pete ivalishwe siku ya kupeleka mahari au kama mtaandaa siku ingine fresh kikubwa mahari ya watu ushatoa hapo unajihakikishia naam ni mchumba wangu napaswa kuweka uthibitisho kidoleni.


Kupiga goti kwa mwanaume ni ishara ya kuomba na wala sio utumwa na pia sio lazima ni wewe tu upendavyo.

Ni lazima uombe tena kwa unyenyekevu sababu unapoomba kuna kukataliwa pia, imagine umeandaa surprise watu kama wote mwisho wa siku bibie anasema " I'm not ready".... tumeshajionea sio mageni.
 
NaUnGa mKoNo hOjA....[emoji30][emoji30][emoji30]
Hata mimi naunga haja kubwa mkono...

Yaani wavalishane pete au minyororo watajua wenyewe... ila tu huu ukuda wa mwanaume kumpigia goti mwanamke kwangu mimi sioni tofauti yake na ushoga.

Hii mitamthilia itatuharibia vijana wetu wallah. Wameanza kuiga hii ya kupigiana magoti soon wataiga ya kubanjuana wao kwa wao.

Ndio, nimeandika mimi babu yao ODM original
 
Pete huvishwa mbele ya kadamnasi ili kuanza kujiwekea kinga ili kuzuia wanyakuzi dhidi ya yule uliyemchagua ktk wengi. Pia si lazima mhusika avishwe baada ya kutoa mahari. Na mwanaume kumpigia goti mwanamke wakat wa kumvika pete ni ishara ya heshima kuwa umemfanya awe km dunia jinsi ilivyo beba kila kitu ukionacho hapa ardhini, hivyo ni heshima ya hali ya juu sana.
zote mbwembwe tu umvalishe pete au usimvalishe kama sio muaminifu sio kikubwa uaminifu na uvumilivu nyingine mbwembwe tu nimewha shuhudia binti kavalishwa pete jion then usiku kaenda kumegwa na ex boy wake hii dunia tunapenda sana kuiga
 
Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.

Basi sawaaaa..... usijali
 
Kwa utaratibu wa Kikristo haswa waliookoka. Ukipata mchumba unamwambia Mchungaji wako.. Mchungaji anakupa baraka zake ndo unapeleka barua ya posa. Barua inajibiwa, unapeleka Mahali, Siku ya mahali ni mahali tu.

Ukimaliza hapo unarudi kwa mchungaji na hapo sasa ndo utatangaza uchumba kanisani kwako na kanisani kwa mwanamke. Siku ya kutangaza uchumba ndo siku ya kuvisha pete. Baada ya hapo mnabandikwa kanisani kote(Tangazo) kwamba nyie ni wachumba. Kwasasa nipo hapo na mimi huko mbele sijui ila ndoa yangu ni mwakani.

Sasa kwenye style ya kuvisha pete ni nyie tu maamuzi yenu. Mimi binafsi nilipiga goti wakati navisha pete. Niligoogle sana na kuuliza sana kwama je kupiga goti ni sana nikaona ni sawa tu maana goti lenyewe moja tu.. ni ishara ya unyenyekevu. Afu nimejichanga kwenye kibubu miaka 2 nimemnunulia mchumba wangu pete nzuri ya Gold k yenye Tanzanite stone amefurahi sana.

Nkaona wanapendaga kunyenyekewa basi nkajishusha nkapiga goti moja nkamvisha pete yake nzuri kabisa alifurahi sana sana. Kama kupiga goti ni ubwege basi mzee baba nlipiga ili tu afurahi.
 
Mimi sielewi tu, mtu unamvalisha pete mwanamke kwa misingi ipi haswa wakati unajuwa kabisa atakusaliti ama utamsiliti yeye.
 
Utamaduni wetu toja enzi, ukivutiwa na msichana kwanza unawashirikisha wazazi, badae unaenda kujitambulisha kwao binti, binti akikukubalia unatoa posa, unachukua binti unaingia kwake anakuwa mkeo....
habari kwisha
Haya mambo ya kuvishana Pete na kunyonyana mate a.k.a kubadilishana uchafu/bakteria ni tamaduni chafu zilizoingizwa na wazungu kwenye hizi dini za kimamboleo.
 
Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.
Usijali kuhusu hilo mkuu, tuko pamoja
 
Back
Top Bottom