storyteller
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 1,544
- 1,874
Nawasalimu wote MMU
Huwa najiuliza huu utamaduni wa kuvalishana pete hapa kwetu Tanzania.
Je, mwanaume anatakiwa amvalishe pete mwanamke siku ya kuomba uchumba, au siku akishakubalika nyumbani kwa mwanamke?
Kwa uelewa wangu, naamini makubaliano kati ya mwanamke na mwanaume yanatakiwa kufanyika na kuvalishana pete kunaweza kuwa kwa namna yoyote (siri ama mbele ya kadamnsasi).
Sasa naomba kueleweshwa, kwa wale wazoefu walio katika ndoa, ama walioingia katika ndoa na kutoka. Utaratibu uliopo(ambao wengi wanaufanya) ni kuvalishana pete siku ya kupeleka mahari(ama wakishapeleka mahari wanapanga siku ya kuvalishana pete), je uko sahihi, ama wanatakiwa kuvalishana kwanza ndipo mahari ipelekwe?
Na pili, suala la mwanaume kupiga goti wakati wa kuvalishana pete, je ni utaratibu sahihi hasa kwa mila na desturi za kiafrika, tujadiliane.
wasalaam.