Utalii una fursa kubwa sana ila njia tunazozitumia ndio zinatufanya tusifaidi matunda ya utalii

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
697
1,000
Utalii ni mpana sana una vitu vingi sana ambavyo kuulewa inataka muda. Na si kila mtu anaweza fanya kazi katika taasisi za utalii ile ni professional kufikia hadi level ya PhD. Kwa mfahamu wa wengi wetu tunawafahamu tu waongoza watalii (tour guides), receptionists katika hotels ambao wamefanya kazi kubwa sana mpaka kuufikisha utalii wetu sehemu ulipo leo. Ila tunachoshindwa kutambua watu hawa wanakutana na mtalii katika hatua ya mwisho kabisa.

Kuna kazi kubwa sana inafanyika kabla ya mgeni kufika, kitu ambacho wengi wetu hatuna ufahamu nacho na ndio maana katika nchi yetu utalii umechukuliwa tu kama shamba la bibi kila mtu anaingia tu. Kutangaza utalii sio kama kutangaza Unga wa ugali ambayo nayo si kazi nyepesi.

Kwanza kwa mtalii mpaka afikie maazimio ya kwenda kutalii, ni mpaka awe na kipato cha ziada (Surplus income), kumaanisha kua ameshalipia vitu vyote vya ulazima kama ada za shule, kodi ya nyumba na mahitaji mengine ya nyumbani. Kile kiasi kilichobaki ndio anaweza kutumia kwa ajili ya kufanya utalii. Hivyo mtu wa masoko anakazi ya kutambua uchumi wa watu wa jamii husika kabla hajaenda kufanya matangazo.

Pili, kutangaza utalii mtu wa masoko inampasa kutambua utamaduni wa jamii husika kabla ya kupeleka bidhaa. Mfano kwa nchi za Mashariki ya Kati, India na nchi nyingi za kwenye ukanda wa Mediterranean bidhaa ambayo kama nchi tunaweza kuitilia mkazo kwa mataifa hayo, ni fukwe za Unguja na Pemba, Bagamoyo, Tanga na Mafia, sababu ndio asili ya watu wao. Kwa nchi za Belgium, Germany, UK, Scandinavian Countries, na Marekani safari na mlima Kilimanjaro ndio bidhaa ya kutilia mkazo. Nchi kama China, Malaysia, Indonesia, Korea na Japan ni safari na mlima pia, ukichanganya na utalii wa utamaduni.

Tatu, Tanzania na mataifa mengine ya Afrika kama Kenya, South Africa, Botswana, Namibia, Zimbabwe... Wengi tunauza bidhaa ambayo zinafanana ni kweli hizi nchi nyingine hazina Serengeti wala Ngorongoro ila zina Simba, Tembo, Duma na wanyama wengine wote wanaopatikana katika Serengeti na Ngorongoro. Hivyo tukitegemea majina tu ya vivutio pasi na kujenga hamasa na kumpa sababu kwa nini mgeni aje tutapoteza tu kwa wenzetu.

Mfano Wakenya wameitumia vizuri tu ile fursa ya "The lion King" kwa kujulisha ulimwengu kua setting ya ile Movie ni Hell Gate National Park ambayo IPO Kenya wakati kiuhalisia ni Serengeti National Park, point yangu ni kwamba Wakenya wameipa thamani hifadhi yao ili kumpa hamasa mgeni kuja nchini mwao kitu ambacho sisi kimetushinda.

Kuna watu ambao wana ufahamu wa utalii ndani na nje ila watu ambao wamepewa dhamana ya kufanya kazi hii wanahisi ni kila mtu anafaa.. Angalia bodi ya utalii (TTB) asilimia kubwa ya wahusika (Decision makers) hawaufahamu utalii ila wanafahamu vivutio vyetu tu... Sidhani kama katika body nyingine let's say bodi ya Afya/Wahandisi inaundwa na watu ambao si wanataaluma wa Afya/Uhandisi.

Ombi langu wekeni watu ambao wataweza kufanya maamuzi na kuwa na technical justification ya kwa nini walichukua maamuzi husika, si kuwa na watu ambao huongozwa na hisia tu. La sivyo tutaendelea kupiga mark time tu mbali ya vivutio tulivyo navyo.
 

tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
574
1,000
Umeongea ukweli mkuu
Kinachonishangaza Mimi hata ni TTB na wizara zinamaliza miaka mitano huoni hata cha maana wanachofanya.

Waziri mwenyewe kiukweli hajui namna ya kuiinua hii sekta ndo mana leo utamwona kakurupuka na kundi la wasanii mara kesho yupo kwenye Marathon lakini ukifwatilia impact ya vitu wanavyofanya huoni .

Kwenye upande wa kudhibiti ujangili tumejitahidi ila katika kutangaza utalii kiukweli bado.
 

spurz11

JF-Expert Member
May 26, 2014
881
500
Safi mkuu nimepata kitu, je uko TTB NA kwingine hatuna tourism experts au wapo ila hawajui wanachofanya kama juzi nilisikia mbunge flani akishangaa Bongo movies wakitangaza utalii, badala ya kina roger federa
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
697
1,000
Safi mkuu nimepata kitu, je uko TTB NA kwingine hatuna tourism experts au wapo ila hawajui wanachofanya kama juzi nilisikia mbunge flani akishangaa Bongo movies wakitangaza utalii, badala ya kina roger federa
Tanzania mwanzoni tulikua tumejikita katika kutunza rasilimali zetu kuliko kufanya tourism, hivyo tukawa na wataalamu wengi katika uhifadhi. Miaka ya 2005 na kuendelea ndipo tukaanza kidogo kuwa serious na utalii. Ingawa wageni wanakuja kazi kubwa inafanywa na Tour Operators katika kutangaza utalii, taasisi za serikali kama TANAPA hifadhi zake zina idara ya utalii ambazo watendaji wake wengi ni wahifadhi na si tourism experts, vivyo hivyo katika TTB na MNRT hakuna pure Tourism breeds. Utalii kwa taasisi za kiserikali wanaichukulia si professionalsm na ndio maana katika wale wafanya maamuzi kuhusu uelekeo wa utalii ni watu wa taaluma nyingine, ambapo si dhambi, dhambi ni pale wanaposhindwa kuja na mikakati yenye tija kwa utalii.

Sehemu pekee ambapo kuna pure Tourism Experts ni katika kampuni za Utalii na ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa wageni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom