Utajuaje umefanya maamuzi magumu?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,512
Habarini wadau wa jukwaa pendwa

**** ushawahi kufanya moja kati ya maamuzi haya we ni nouma sana

1. Unatoa mimba alafu unalala na midoli kitandani..
- Ni maamuzi magumu.

2. Huna hata kitanda na unaamua kuoa -
-Hayo pia ni maamuzi magumu.

3. Huna uwezo wa kumlisha mkeo kazi yako ni kumjaza ujauzito - -Ni maamuzi magumu.

4. Shule haina waalimu unampeleka mwanao -
- Pia ni maamuzi magumu....

5. Daladala imejaa mpaka mlangoni na unaamua kupanda - -Ni maamuzi magumu.

6. Unalipwa laki mbili unamhonga binti laki moja - - Hayo ni maamuzi magumu.

7. Kama utasoma hapa na kushindwa kuweka maamuzi magumu unayoyajua - -Utakuwa unamaamuzi magumu mnoo...!

8. Mdada unavaa nguo ya laki saba mshahara laki tu- -Hayo ni maamuzi magumu

9.Binti unamwacha kijana mwenzio wa rika moja unaamua kuolewa na babu umri kama wa baba yako - -hayo ni maamuzi magumu

10.Unapanga nyumba ya milioni saba kwa mwaka huku mshahara ni laki tano kwa mwezi - -Hayo nayo ni maamuzi magumu

11.Unamfumania mkeo au mkeo anakuzalia watoto wanne nje ya ndoa na bado unaendelea kumwamini- -Hayo nayo ni maamuzi magumu kupitiliza

12. Unamuadi mtu utamchangia ela katika sendoff au harusi yake wakati unajua hata kuwalipia Ada ya shule kuwalipia watoto Hakuna. hayo ni maamuzi magumu sana

13. Unambembeleza mwanamke kuwa unataka kumuoa na unajua kwamba unataka tu kumchezea na kumuacha - Hayo ni maamuzi ya kishetani

BADILIKA!!!!
 
Kama jamaa mmoja huko Nigeria. Mtoto kadai anunuliwe iPhone X apewe zawadi siku ya birthday.Hela aliyo nayo jamaa ni ya kulipa kodi ya nyumba. Kwa kuwa mtoto alisisitiza kuwa bila iPhone na uhusiano uishe jamaa kafanya mamuzi magumu. Alitumia hela ya kodi kununua simu ya mpenzi wake na kumpa zawadi siku ya birthday. Penzi alilopewa siku hiyo ni la kufa mtu. Lakini siku iliyofuata ilikuwa ndio ya kukabidhi kodi kwa mwenye nyumba. Jamaa hela hana mwenye nyumba kachachamaa anadai jamaa kama hana hela afungashe aondoke. Jamaa kichwa kinauma.
 
:D:D:D:D:D:D:D
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom