Utajuaje mwanamke kala ndoano?

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,966
Huu umekuwa mtihani mkubwa sana kwa wanaume, wavua samaki wao wanaweka boya, akiona linazama tu anajua tayari samaki keshakula ndoano basi kazi yake ni kuvuta tu. Mwanaume unaweza kurusha ndoano kwa mwanamke, mwanzoni anaweza kutoa nje asionekane cheap, sitaki nataka au labda kweli ana mtu wake kwa wakati huo, mtihani unakuja pale mwanamke anapoachika akataka kuja kwako sasa, kukuambia hawezi ila anaanza viishara tu, sasa utajuaje kala ndoano?

1. mwanzoni anaweza akawa hakuchekei, ukiona anaanza kukuchekea basi jua mambo tayari.

2. ataanza kukutumia msg za mara kwa mara, vuta mambo tayari.

3. ataanza kukueleza matatizo yake na ikibidi kuomba msaada wa hapa na pale, mara nilicharge.

4. ataanza kuponda wanaume, wanaume waongo, mara oooh mapenzi yanaumiza, jua tayari vuta kamba.

tafadhari ongezea tupate uelewa mpana.
 
Usimpompigia siku nzima au hata msg atakupigia au atatuma msg "Mbona umenisusa hivyo" huyo tayari vuta kamba
 
Usimpompigia siku nzima au hata msg atakupigia au atatuma msg "Mbona umenisusa hivyo" huyo tayari vuta kamba

hahahaha, kweli mkuu, nayo hiyo ni dalili tosha.
 
kucheka saa nyingne anakuzodoa ulivyomjinga kufikiri yeye saizi yako.

sijakuelewa mkuu, hii nayo ni dalili kuwa kala ndoano?
 
atakwambia yeye hakufai katafute warembo kwn wako wengi
 
akikupigia akakuta simu yako inatumika..afu ukampigia akawa na dukuduku kujua uliyekua unaongea nae..
uyo tayari..vuta kamba

kweli mkuu, kwa maana nyingine akionesha tu wivu vuta kamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…