๐—จ๐˜๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ๐—ท๐—ฒ ๐—ž๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ป๐—ถ ๐—™๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ?

๐—จ๐˜๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ๐—ท๐—ฒ ๐—ž๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ป๐—ถ ๐—™๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,346
Reaction score
2,750
Namna ya kutambua Kama simu Yako ni feki

Unajua unaweza kutambua simu ambayo unapenda kuitumia Kama ni feki au original kabla ujainunua ??

Hii ni moja wapo ya changamoto ya watu wengi Sana wanalalamika juu ya simu wanazomiliki sio zile ambazo waliziona kwenye picha au walizoambiwa kabla hawajanunua.

Unakuta mtu anataka simu labda Samsung , Infinix , Oppo , Realme , Google pixel nk Ila baada ya kununua tu ndani ni tofauti kabisa umeambiwa specs zake labda ni ram 8 , storage yake ni 128 , camera yake mp50 kwenye boxi Ila ukitumia sasa unaona maajabu.

Kupitia IMEI namba ni sehemu moja wapo muhimu ya kutambua Kama simu unayomiliki ni kweli yenyewe au umepigwa !!! Kwani itakupa taarifa kamili ya kifaa chako.

Emei namba ni namba ambazo zipo katika Kila kifaa Kama utambulisho wala haziwezi kufanana daima Kila kifaa (simu , tablet, kompyuta) nk ina IMEI namba yake.

Ukitaka kupata IMEI namba bonyeza *#06# au kwenye boxi la simu unayotaka kununua utaona kwa nje Kisha fungua kivinjari chochote Cha browser Kama chrome , Mozilla , brave nk

Kisha andika www.imei.info utaweza kuweka IMEI namba zako weka ya Kwanza watakuletea taarifa ya simu Yako Kisha utaangalia Kama zenyewe pia utaweka ya pili na kuangalia Tena Kama taarifa zilizopo kwenye IMEI ndo zilizopo kwenye simu Yako.

Kabla ujanunua simu dukani au kwa mtu ukitaka Kujua Kama simu ujapigwa tumia iyo njia utakua salama !!
 
Sometimes, simu fake inaweza ikatumia IMEI za simu original. Kitu cha muhimu zaidi ni kutumia apps zinazoonesha specs kama CPU-Z, ama app za ku-benchmark, hapa utapata kuona specs halisi ambazo unaweza kucompare na za mtandaoni pamoja na speed / performance ya simu (kama utatumia benchmark apps)
 
Back
Top Bottom