Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,278
- 11,128
Ukiwa mfanyakazi serikalini au katika mashirika ya umma na binafsi kuna sheria kabisa ya nchi inayolazimisha kuwa lazima uwekeze kwenye NSSF.Na pesa yenyewe si ndogo,ni takriban 20% ya basic salary ya mwajiriwa.Mlimbikizano wa pesa hizi umeifanya NSSF kuwa tajiri sana.Cha ajabu hao wanachama wanapotaka pesa yao huzungushwa na hatimae wengine kufikia kufa kabla hawajazitia mkononi.
Hivi sasa NSSF imehemkwa kutokana na utajiri wake uliopindukia.Mara wanajenga daraja la juu ya bahari,mara maghorofa yasiyo na idadi,mara inalima mkonge.Jee ni halali kufanya yote hayo bila kushauriana na wenye pesa zao?.