Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi


Wewe binafsi unao utajiri huo (unaodai wa kishirikina)?
 
Kwa uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wengi wenye hela/matajiri utajiri wao sio wa halali au wa kutoka jwa Mungu. Haijalishi awe ni mfanyabiashara au mfanyakazi wengi huwa wanakitu nyuma ambacho kinawapa huo utajiri kupitia hizo kazi au biashara wanazofanya.
ukianzia kwa wafanyabiashara, hawa ndo wanaongoza kwa sababu mwanzoni wakati unaanza biashara utapata faida kidogo basi na mtaji utakua taratibu nao. itafikia mahali utaona mtaji hauongezeki wala faida haikui sanasana unaanza kushuka. Hapo manaake uwezo wako wa kibinadamu umeishia hapo na hapo ndo huwa crossrod kwa wafanyabiashara wengi ambapo ili kusogea mbele au kupga hatua inabid uchagua moja kati ya Mungu au shetani. Wengi sana sana sana huchagua njia ya shetan kwa sababu huwa ni rahisi kwa macho hivyo huanza kwenda kwa waganga na wengne kujiunga na vikundi vya kishetan kulingana na ukubwa wa biashara yako na mahitaji yako. kumbuka haimaanishi kuwa ukijiunga huku ndo unaacha kufanya juhud, hapana.. juhud inaendelea pale pale sema unakua na busta ya kukunyanyua juu kwa spid ya ajabu. Unaweza ukatangaza kidogo watu wakajaa telee na kadhalika.
Kwa upande wa wafanyakazi, huku ndo kule ambapo wengi huwa wanalogana wao kwa wao kugombania cheo kazini. Kiuhalisia ukiachana na hii hali ambayo tunaiona kwa macho kuwa flani ni mtendaji kazi mzuri, huwa kuna nguvu nyuma inayobadilisha mwonekano wako mbele ya macho ya watu kiasi kwamba kila mtu anakua anatambua mchango wako kwa namna ya ajabu. Wafanyakazi wengi huwa wanalogezea kwa namna hii ili waonekane bora kuzid wenzao na huwa wanaendelea kufanya kazi vizuri tu. Hata wakati wa kuomba kazi, sio kila mtu hua anapata kazi kiuhalali. Wengi huwa wanaenda kwa waganga kupata mvuto ili wachaguliwe. Mara nyingi wafanyakazi hujificha wasionekane kama wanatumia mambo ya kishirikina kuliko wafanyabiashara. Taasisi nyingi za serikali na binafsi huwa unakuta mtu flan anakufa gafla , kumbe kashaangushwa na mwenzaje anayetaka hicho cheo. Kusoma au kuwa na PHD hakuusiani kivyovyote na iman ya kishirikina kwa maana hata maprofesa ni wachawi na vitu hvo viko katika pande mbili ambazo haziingiliani yaan mchana profesa usiku mchawi. Hivyo usijidanganye kuwa unapomuona mfanyakaz mwenzako pale ofisin ukajua ni elimu ndo imempa kile cheo. Mara nyingi hua ni hapana japaokua wapo wachache tena wachache sana wanaopata kwa style hiyo. ila wafanyakzi ni wanafiki sana na huwa wanakataa kukiri kuwa wengi wao wanatumia ushirikina kulinda kazi zao.

Mwisho nataka kusema kuwa Mali na fedha vyote hutoka kwa Bwana.. mtafute Bwana na vyote vitakuja maana ni vya ziada tuu!!!
 

kama hawaendeshi magari,hawali nyama,hawavai vizuri,hawendi vacation,hawa enjoy .hiyo pesa haina maana.mi nawaona ni masikini.siyo matajiri. Tajiri unaogopa kula nyama? Ha ha ha h..
 
Teh teh teh mbavu zangu...eti kujifyokonyoa naniliu haa haa JF!
 
Kwani naomba kuuliza hivi uhusiano wa pesa na hivyo vitu ni UPI?
Yaani kifo cha kiumbe hai na mie kuwa tajiri ni process gani inafanyika?
 

Nimehisi kutapika (kinyaa kikuu) ......Daaaah

Mwanzo na mwisho kula kwenye migahawa uchwara. Lol
 
Kuna vitu huwa vinafanyika mpaka mtu kuwa tajiri ndio mana unaambiwa utoe kafara ya damu unapokwenda kwa mganga japo kuna utajiri mwingine unaweza kuupata bila kutoa damu ila nao huitaji ujasiri wa hari ya juu
 
Mkuu huyu hawajui wakinga anawasikia,atuulize tuliokua nao na kuishi nao

Kuna mmoja nikikua naambiwa ukiingia dukani kwake anakuona upo uchi nikabisha nikaenda na mazivu yangu nikanunua vitu wakati nataka kuondoka akanipatia nyongeza ya kiwembe nilibaki tu nashangaa.
Halafu akienda mdada yupo period anahudumiwa na Mke wake tu..usichezee mkinga na watu wanapanga foleni dukani kwake
 

Kuna watu wananishangaza sanaaa eti wanakuambia wana muamini Mungu yet hawatambui uwepo wa shetani (uchawi). Ni unafiki tu. Wakati misahafu ina muelezea Ibilisi in and out.

Ndio maana hata kwenye hesabu kuna hasi na chanya.

Mtu yeyote aliyeishika dini vilivyo ana uelewa wa shetani na uchafu wake wote. Unatatua vp tatzo (nguvu za giza) kama huelewi zinavyo function ?? Otherwise utakubaliana na mada ya mshana jr fika. Tusifanyane watoto humu.
 
Last edited by a moderator:
zipompa

Thank you.
Nilikua mbishi sanaaa mpaka nlivyo shuhudia Moshi huko kwa macho yangu ni shida ndugu.

There are lots of things going on in the spiritual world. Mila za kichagga ni very powerful na ukifanya masihara wataanguka watu utashangaa na macho yako kama sio kudhurika.

Yupo Aunty yangu flan alitoka nnje ya ndoa akashika mimba nnje na mtu mwingine akamdanganya mmewe ni yake. Yule mtoto wa nnje alivyozaliwa kwenye ile nyumba yao. Kulitokea balaa.

Watoto wengine wa ile nyumba ilikua full kuumwa, hospital ugonjwa hauonekani vitimbi kibao, watu wametoa pesa kibao kutibia. Babu yetu wa ukoo akabutuka akasema ile mimba sio ya nyumba yetu (ukoo wetu) ndio maana.

Mwanamke kubanwa akakubali cz watoto wale wengine wangeweza dhurika kwa kiasi kikubwa. Ikafanywa mila kile kichanga kikarudishwa kimila kwenye ukoo wao (baba yake). Watoto siku mbili nyingi wakapona wote.

Kuna makabila haya dhulumiwi watajua tu, kuweni makini mnapo oa / kuolewa.
 
Last edited by a moderator:

Hilo ni kweli kabisa hawa mama ntilie ni noma kuna huyo mmama yeye Yale maji ya kutawaza kila asubuhi au mkojo wana changanya kwenye msosi au ile ya ble.... Ana chaganya kwenye misosi yake.Mteja akila una shangaa tumbo linamsumbua kila Mara plasi na aliyonenea inakua mkosi mtupu. Cha msingi before eating mtu asali kwa imani yake.
 
Na kwenye haya masharti kuna
-ya kulala na mamaako/babaako/mwanao
-kulala na mtoto mdogo/mchanga.ndio maana kuna habari nyingi sana za watu kubaka vitoto vidogo kabisa tena vingine vya miezi tuu

Hyo ya kulala na mzazi inatumiwa sana hadi na wasanii wakubwa wa kibongo aisee ushirikina ni hatari sana kwa kweli. Ubaya vitu vya kishetani havidumu kabisa hata utimize masharti lazma siku viku geuke wewe.
Kuna baba mmoja alienda kwa mganga kusaka utajiri mganga akaangalia nyota ya wana ukoo akamwambia mtoe ndugu flani na flani na mwanawe akawa tahira. Yeye huyo baba akamuua ndugu yake kwa siri watu wakajua kapotea.
Huyo baba alikua tajiri wa kutisha mijumba magari siku kakosea masharti vyote vilipotea kuanzia magari kuungua nyumba utajiri wote ukawa kwishney. Nowadays kafulia hatari.
Ushirikina ni mbovu siku kikibuma unaumia na ndugu umewapoteza.
 
Senior Boss mila za kichaga usipofata ka ni ukoo lazma uangamie bila kupenda watu kuenda kinyume na miiko ya kikoo na familia bora hyo kuliko kutoa mikafara.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…