Kuwa tajiri hata kama ni kupindukia sio vibaya kama ni kutokana na nguvu zako. Na hili linawezekana sana hapa bongo kwa watu waliokuwa na opportunities kama kina D.Yona, F.Masha, F.Mosha, etc (Soma cv zao) actually wakiwa fukara tunatakiwa kuwacheka!
Ila Haya ndo mambo tunasema kila siku, ukiwa kiongozi wa umma unatakiwa kuwa clean "in fact, and in appearance"! Na hapa nadhani ndipo Yona anapo chemsha, kutokana na tuliyo yasikia Kiwira tu, tunashindwa tenganisha kati ya mali za wizi na za halali.
Kwa kuwa hili jukwaa ya thinkers! Tu - reason kidogo hii kesi.
kwa madaraka, na opportunities alizo wahi shika huyu bwana Yona, miaka nenda garuka, kuwa na utajiti huu wa makongo, sijui nyumba ya tegeta - tena ya mwanae mimi sioni ajabu!
Isitoshe kila nyumba iliyopo pale ilijengwa kabla jamaa hajawa mbunge, na nyumba anayo ishi ni ile ile (hata alipokuwa waziri) amabyo aliijenga toka akiwa THB - bila shaka ni kwa mkopo! Tena iko barabarani - vumbi loote lina ingia ndani!
Nasikia Yona alinunua eneo lake pale kama eka 8 kwa sh 120 - mwaka 1968 so sio hatari kuwa na mali hizo leo miaka zaidi ya 40.
Ni sawa na wanaokamata ma-ardi leo kibaha eka 1 - sh laki 3. Baada ya miaka 20 itakuwa kaa makongo.