Njanga Tz
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 843
- 655
Toka niwe member hapa sijawahi fikiria siku moja nitakuja kukutana na mawazo mbadala ya kubadilisha status ya uchumi wangu hapa. Nilikuwa shabiki namba moja wa jukwaa la SIASA,kimsingi sio dhambi kushabikia jukwaa hilo lakini dhambi ni pale unaposhabikia halaf huingizi kitu.
Kuna siku moja nikakaa nikatulia kusoma jukwaa hili la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali, MAKENIKIA niliyoyaokota hapo yamenifanya nisirudi tena kusoma jukwaa la SIASA.
Nilipitia mabandiko kibao hapa, lakini nilivuitwa sana na mijadala kuhusu biashara ya nafaka, na kwa kupitia IDEA za hapa nilichukua hatua za kuanzisha biashara hiyo kama ifuatavyo;
Nilitumia mtaji wa milioni tatu tu. Nilitafuta fremu niliyolipia laki moja kwa mwezi, nikailipia miezi sita yaani laki saba pamoja na udalali. Nikabakiwa na milioni mbili na laki tatu. Nikatumia hiyo pesa kununua mzigo wa kuanzia biashara, nikanunua Mchele, Maharage, Unga na Mafuta ya Alizeti ya Singida.
Siku ya kwanza ya biashara niliuza laki moja na ishirini lakini toka hapo kwa wastani nauza laki tatu na nusu kwa siku na hivyo kwa wiki nauza wastani wa milioni 2.4M na kwa mwezi ni milioni 9.6.
Hii biashara nilifanya kama kutest nikaweka mtaji mdogo lakini nmegundua ukitaka kuendelea ondoa uwoga. Kwa hii miezi mitatu niliyofanya hii biashara faida ninayoipata kwa kila mwezi baada ya kuondoa takataka zote inakaribia mara mbili na nusu ya mshahara wangu kwa mwezi(Mshahara wa serikali TGSE).
NB: Ubunifu unahusika; kupaki vizuri, usafi na mrembo wa kuchangamkia wateja.
Tuamke utajiri uko mikononi mwetu.