Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,550
8,642
Kwa ufupi tu umoja ni nguvu. Ukiangalia vizuri kuna vitu ambavyo wana EAC tungeweza kufanya pamoja na kurahisisha maendeleo ya nchi zote

1. Madawa tungeweza kuagiza pamoja maana tunaumwa magojwa yale yale hii ingesaidia kupunguza bei ya uagizaji kwasababu tuna nunua kwa jumla. Lakini kwenye chanjo kama za Corona tungeweza kuagiza kwa pamoja na kugawana zikifika hapa!.

2. Mfumo wa elimu tungeweza kuweka mfumo mmoja hii ingesaidia wawekezaji wakija kwenye nchi mmoja kuwa na vijana wenye elimu zenye uwiano sawa. Vilevile ingesaidia kwa elimu za madaktari na walimu.

3. Usalama pamoja na kuwa na majeshi yetu tungeweza kuwa na jeshi ya EAC kwa ujumla kupambana na ugaidi na ku share hata satellite za usalama. Hii ingepunguza matumizi mabaya ya kijeshi maana tumekuwa dump la kuuziwa vifaa vya kizamani.

4. Shirika la ndege moja ni vichekesho kuwa na shirika la ndege kila nchi ! Tungefungua kampuni moja halafu wawe wanakodisha ndege kutoka nchi shiriki na kila nchi itakuwa na share kutokana na mchango wake hii ingepunguza gharama na kuongeza ushindani bila hivi mashirika ya nje yataendelea kutawala anga zetu.

5. Masoko ya mzao ya pamoja yaani kuwe na shirika la kuongoza masoko ya biashara za mazao na bei ziwe wazi na kutangazwa kote kuwe na masoko ya jumla kila mpakani ya kisasa. Kama ilivyo dhahabu bei za mazao ziwe zinatangazwa kwa uwazi .

6. Tuwe na vyuo vya technologia na ufundi pamoja kufundisha teknologia mpya kama programming. Fungueni kampuni na kuingia mkataba na kampuni kama Microsoft, google, Apple na Oracle ili vijana wetu waweze kufanya kazi kutokea nchi hizi washiriki.

India mfano wana vijana kwa milioni wanafanya kazi za nchi nyingine kuanzia engineering design, customer service, payroll and accounting, bank support. kwanini sisi tushidwe wakati tuna vijana wengi.

Kwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa.
 
Hamna jipya haya unayoyaongea tulishayafanya na mpaka sasa tunajaribu lakini haitawezekana kwasababu ya tofauti zetu za kijamii,mila na desturi, malengo ya kiuchumi ,kisiasa na ubinafsi ndani yake.

Hujiulizi leo hii kwanini Britain anajitoa katika umoja wa ulaya.? Tuendelee kuvumiliana labda siku moja ndoto yakuwa pamoja itatimia.
 
Sidhani, wao na sisi "ndoto ya kuwa pamoja" itimie?

Hiyo na ibaki kuwa ndoto tu!
 
Hili jambo ni gummy sana kutimia kwasababu ya malengo tofauti ya nchi wanachama.

Tofauti za uchumi nafikiri nalo limechangia kwa kiasi kikubwa.Nchi kama Kenya yenye uchumi mkubwa lengo lake kuu ni soko kubwa na imekuwa ikijitahidi sana kutaka kuendelea ku dominate nchi nyingine.Wakati huo huo nchi kama Tanzania na Uganda zimekuwa zikijitutumua kuondoka na utegemezi wa bidhaa za viwandani kutoka Kenya eg maziwa,sukari,bidhaa za plastic na nk.

Kwakuwa kila nchi imekuwa na tabia ya kulinda soko lake la ndani dhidi ya bidhaa za nchi mwanachama matokeo yake EAC imekuwa dubwana linalokataliwa na viongozi wenye malengo tofauti tofauti ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.
 
Hamna jipya haya unayoyaongea tulishayafanya na mpaka sasa tunajaribu lakini haitawezekana kwasababu ya tofauti zetu za kijamii,mila na desturi, malengo ya kiuchumi ,kisiasa na ubinafsi ndani yake.

Hujiulizi leo hii kwanini Britain anajitoa katika umoja wa ulaya.? Tuendelee kuvumiliana labda siku moja ndoto yakuwa pamoja itatimia.

Hatuna tofauti ya kiutamaduni yeyote makabila ni yaleyale. Arusha huku na Nairobi hakuna tofauti , wa pwani hawana tofauti nk hatuna tofauti ya kiutamaduni maana hatuna utamaduni wa nchi bali utamaduni wetu ni makabila.

Pili mawazo yangu sio ya kunufaisha nchi mmoja mfano tukiwgiza dawa pamoja gharama zitapungua lakini zikifika hapa kila nchi inachukua kiasi walicho agiza ni sawa na ku share container lakini hata bei itashuka. Kuhusu ndege mfano ni share sasa kuna shida gani kama tutapata ulicho wekeza.

Elimu mbona hao viongozi wetu wamesoma nje? Kwanini tusiwe na system ina fanana ili isiwe kila siku tunaambiwa elimu ya nchi mmoja iko chini? Sasa hapo kuna ukenya na Utanzania upi?

Mnao shinda kuogopa Kenya bado sielewi ni wapi watanufaika zaidi yetu maana mawazo yangu bado kila mmoja ana haki sawa
 
Kamlilie Jomo na Njonjo hayo unayoota wakati huu.

Naona kuna kitu kinawasumbua sana watu wa nchi ile, maana hamtulii; ni kama kuna kitu kinachowaogopesha sana juu ya maisha ya nchi yenu hiyo.
Sijui ni kitu gani hicho.

Hakuna chochote zaidi na negativity uliyonayo. Ukiwa negative kila kitu utatafuta cha kulaumu au kulalamika ndiyo maana nchi yetu iko hapa leo.
 
Hamna jipya haya unayoyaongea tulishayafanya na mpaka sasa tunajaribu lakini haitawezekana kwasababu ya tofauti zetu za kijamii,mila na desturi, malengo ya kiuchumi ,kisiasa na ubinafsi ndani yake.

Hujiulizi leo hii kwanini Britain anajitoa katika umoja wa ulaya.? Tuendelee kuvumiliana labda siku moja ndoto yakuwa pamoja itatimia.
Umemjibu vyema Kamundu maana kakurupuka bila kufanya utafiti
 
Mimi Mkenya hapa, ila huu uzi ukijadiliwa na great thinkers wasiokua wazembe wa kushirikisha ubongo unaweza ukawa uzi muhimu sana JF. Afrika yote hii kinachotukwamisha ni hii mipaka ya mkoloni, hatuna nguvu ya wingi au volume inayotumika na walioendelea, kwa mfano China wale wako bilioni moja, yaani ukikuza matikiti yako uko na uhakika wa soko la watu bilioni ambao unaweza ukawafikia bila kikwazo, Marekani wako zaidi ya milioni mia tatu, watu wote hao kama soko moja.

Afrika hapa tuko watu zaidi ya bilioni moja ila tunabanana na kuzongana kwa misingi ya viinchi, vingine hata saizi ya mkoa kama vile Rwanda na Burundi, hauwezi kuvusha chochote uuze hapo Kigali bila kupitia usumbufu wa kufa mtu.

Hapa EAC siku tutakuja kubuni mtaala wa pamoja ndio huu uwoga wa kuogopana utaisha, mzawa wa huko mbali Kigoma akiwa kwenye level moja kielimu na mzawa wa huku Kenya maeneo ya mbali kama vile Laikipia, hapo hapatakua na kijisababu cha kuogopana. Nimeishi Bongo, nimekatiza mikoa na wilaya nyingi sana, sijaona chochote tofauti na kwetu huku, masela mitaani ni wale wale, vijana vijiweni pande zote mbili hujadili yale yale tu ya akina Manchester United sijui Arsenal.
 
Hakuna chochote zaidi na negativity uliyonayo. Ukiwa negative kila kitu utatafuta cha kulaumu au kulalamika ndiyo maana nchi yetu iko hapa leo.
"Ndiyo maana nchi yetu iko hapa leo"? Nchi 'isiyokuwa hapa leo' ni nchi gani, ile uliyoikimbia?
Ingekuwa hivyo usingeikimbia.

Unapojifanya wewe ni kondoo, unajificha kwenye kundi la kondoo, kumbe wewe ni fisi, unadhani watu hawawezi kutambua?

Ukweli ni kwamba hiyo ngozi ya kondoo haikufai kabisa, kwa sababu haifichi chochote wakati tabia ni zile zile za fisi.

Nisome vizuri unielewe nilichoandika hapa. Usirukie tu kujibu kwa mihemuko. Ni ujumbe mahususi niliokupa.
 
Hapa EAC siku tutakuja kubuni mtaala wa pamoja ndio huu uwoga wa kuogopana utaisha, mzawa wa huko mbali Kigoma akiwa kwenye level moja kielimu na mzawa wa huku Kenya maeneo ya mbali kama vile Laikipia, hapo hapatakua na kijisababu cha kuogopana. Nimeishi Bongo, nimekatiza mikoa na wilaya nyingi sana, sijaona chochote tofauti na kwetu huku, masela mitaani ni wale wale, vijana vijiweni pande zote mbili hujadili yale yale tu ya akina Manchester United sijui Arsenal.
Sasa tuambie: "ulipoishi Bongo ulimwona mzawa wa huko mbali Kigoma", ulimwona huyo mkigoma akiwa na kisababu cha "kumwogopa mtu kutoka Laikipia?"

Na mtu wa kule Kwale au Kilifi, hapana, hata pale Baringo na sehemu nyingi tu huko Kenya yupo 'level' gani kielimu na mzawa wa huku Tanzania??

Ni vitu kama hivi msivyovitambua kuwa vinawasumbua sana watu wa huko, kiasi kwamba mnajisahau na kudhani nyinyi ni bora zaidi ya wengine, kumbe hamna lolote. Uoga wenu ndio unaowafanya mhangaike na vijimada visivyokuwa na mbele wala nyuma kama hii hapa.
 
Ndio maana nilisema uzi kama huu unapaswa kujadiliwa na wenye uwezo kushirikisha ubongo, wengine mtaishia kukojoa humu bila umuhimu wowote.
Hii ni mijadala inayoangalia zaidi ya miaka 100 ijayo.
 
Mimi Mkenya hapa, ila huu uzi ukijadiliwa na great thinkers wasiokua wazembe wa kushirikisha ubongo unaweza ukawa uzi muhimu sana JF. Afrika yote hii kinachotukwamisha ni hii mipaka ya mkoloni, hatuna nguvu ya wingi au volume inayotumika na walioendelea, kwa mfano China wale wako bilioni moja, yaani ukikuza matikiti yako uko na uhakika wa soko la watu bilioni ambao unaweza ukawafikia bila kikwazo, Marekani wako zaidi ya milioni mia tatu, watu wote hao kama soko moja...
One China Policy inaelekea kuwaumbua Unaona kinachoendelea pale Hong Kong?
 
Humohumo east afrika kuna ukabila wa kutisha, watu wa nchi moja lakini hawawezi shirikiana kufanya kazi kwa umoja sembuse mataifa tofauti?

Kuliko kufanya vitu ambavyo havitafanikiwa wacha kila nchi ikomae na hali yake
 
Umeongea jambo la msingi lakini bahati mbaya bado nchi haijakomaa kiakili kujua hili ni la muhimu. Tungeanza hata kwa kuweka soko huru la EA tungekuwa hatushikiki. Soko la watu zaidi ya 150m si mchezo. Hakuna kitu utafanya kikakosa soko. Tungekuwa na sauti duniani.

Utaifa na uzalendo ni viini macho tu, watawala wanatumia hivyo kupumbaza wananchi na kuendelea kubaki madarakani .
 
Hamna jipya haya unayoyaongea tulishayafanya na mpaka sasa tunajaribu lakini haitawezekana kwasababu ya tofauti zetu za kijamii,mila na desturi, malengo ya kiuchumi ,kisiasa na ubinafsi ndani yake.

Hujiulizi leo hii kwanini Britain anajitoa katika umoja wa ulaya.? Tuendelee kuvumiliana labda siku moja ndoto yakuwa pamoja itatimia.
Ndoto haiwezi kutimia kwa kutarajia itimie mkuu. Inabidi uifanyie kazi. Kama kitu kinamanufaa kwanini usikifanyie kazi?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom