Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Toka utawala huu wa sasa uingie madarakani kuna wafanyabishara wengi tu wamehamia nchi jirani kama Kenya, Uganda na Zambia na wanafanya shughuli zao bila matatizo yoyote.

Ile fikra kwamba wakenya wana roho mbaya ilikuwa ni zamani na kwa sasa hawako hivyo. Mimi natembelea mara kwa mara Nairobi na Kisumu na kulishuhudia hili.

Na kiukweli kwa sasa ni Kenya ndio inayoilalamikia Tanzania kwa kuwanyanyasa raia wake tofauti na ilivyokuwa hapo zamani ambapo Tanzania ndio ilikuwa ikiilalamikia Kenya kwa kuwanyanyasa watanzania nchini mwao.

Mkishakuwa majirani lazima mnahitajiana mpende msipende ila ukweli wakenya wamebadilika sana sio kama walivyokuwa zamani.
 
Unahitimisha mambo ya kipuuzi sana..., wewe sio mbongo? Lugha hiyo naisikia toka huko kwingine, wewe ni mmoja wa hao watu?

Tupe mfano wa "uoga wao" nasi tujue kweli ni 'waoga wa ushindani.'
Kwani wanaokwamisha shirikisho la EAC ni nani kama sio wabongo?
 
Hatuna tofauti ya kiutamaduni yeyote makabila ni yaleyale. Arusha huku na Nairobi hakuna tofauti , wa pwani hawana tofauti nk hatuna tofauti ya kiutamaduni maana hatuna utamaduni wa nchi bali utamaduni wetu ni makabila.

Pili mawazo yangu sio ya kunufaisha nchi mmoja mfano tukiwgiza dawa pamoja gharama zitapungua lakini zikifika hapa kila nchi inachukua kiasi walicho agiza ni sawa na ku share container lakini hata bei itashuka. Kuhusu ndege mfano ni share sasa kuna shida gani kama tutapata ulicho wekeza.

Elimu mbona hao viongozi wetu wamesoma nje? Kwanini tusiwe na system ina fanana ili isiwe kila siku tunaambiwa elimu ya nchi mmoja iko chini? Sasa hapo kuna ukenya na Utanzania upi?

Mnao shinda kuogopa Kenya bado sielewi ni wapi watanufaika zaidi yetu maana mawazo yangu bado kila mmoja ana haki sawa
Kama wewe wakati ule wa EAC ya zamani ulikuwa hujazaliwa, uwe unasoma basi angalao historia ya EAC kabla ya kuja na mawazo kama haya. Tunatakiwa kwanza kujua tulikotoka, mahali tulipo kabla ya kuamua tunakotaka kwenda.

Mara baada ya nchi za Uganda chini ya rais Milton Obote, Kenya (Jomo Kenyatta) na Tanzania (Julius Nyerere) kupata uhuru wake kutoka kwa muingereza ziliungana pamoja na kuunda EAC ambapo shughuli zote za kiuchumi na maendeleo za nchi hizi ziliendeshwa kwa pamoja kupitia umoja huo wa EAC. Hata pesa (currency) ilikuwa ni moja = East Africa shilling chini banki kuu moja ya EAC. Njia za mawasiliano, reli, ndege, meli, bandari na anga zote zilimilikiwa kwa pamoja. Viwanda vyote vilivyokuwa vinazalisha bidhaa mbali mbali hususani zana za kilimo, mafuta ya kula, blue band, beer na kadhalika vyote vilikuwa vinamilikiwa na EAC.

Lengo la waasisi wa umoja wa EAC lilikuwa baadaye nchi hizo tatu kuja kuungana kuwa nchi moja chini ya rais mmoja. Kilichokuja kutokea ni majonzi ambayo hatupaswi kuyasahau. Nchi ya Tanzania ilikuwa na siasa za kushoto, yaani za kijamaa, hivyo haikuwa inapendwa na nchi za magharibi. Nchi ya Uganda ilikuwa na siasa za kati. Kenya ilikuwa na siasa za kulia yaani za kibepari (capitalism) na hivyo ilikuwa kipenzi cha nchi za magharibi. Hata wazungu waliokuwa wakoloni wengi wao hawakuondoka Kenya baada ya uhuru. Wazungu hao walibaki huko wakimiliki mashamba makubwa makubwa (estates) na njia kuu za kiuchumi. Kwa kuwa wafadhili wakuu wa maendeleo ya nchi hizo za EAC walikuwa ni kutoka nchi za magharibi, walihakikisha karibu viwanda vyote vya EAC vilikuwa vinajengwa nchini Kenya - Nairobi, Mombasa etc. Ili kutupumbaza, kitu pekee kilichojengwa Tanzania ni jengo la makao makuu ya EAC pale Arusha.

Janja janja nyingi zifanyika kwenye jumuiya hiyo zikiendeshwa na upande wa Kenya walianza na kujitoa kwenye currency ya EAC. Wakaanzisha KSh na benki kuu yao. Mwaka 1977 wakati Tanzania tukigombana na Nduli Iddi Amini wa Uganda, Kenya walipora mali zote za EAC na kuvunja jumuiya hiyo. Kabla ya kuivunja walihakikisha vitu kama ndege zote za EAC, meli zote na train zote ziko nchini kwao. Hivyo tukajikuta hatuna hata kiwanda cha kutengeneza sabuni, bia, kiberiti, sindano wala cho chote kile. Yaani nchi yetu ikawa fukara wa kutupwa. Tukaanza upya from the scratch tena kwenye wakati mgumu sana kwani ilikuwa tunatoka kwenye vita dhidi ya nduli Amini iliyokuwa imetugharimu sana. Baada ya kufanya uporaji huo wa viwanda vya EAC, nchi ya Kenya ikawa ni nchi ya viwanda na soko kubwa la mazao ya viwanda hivyo likawa ni Tanzania na Uganda hadi leo.

Sasa baada ya kupitia yote hayo, tumejikongoja na kujenga viwanda, uchumi wetu unaendelea kupaa kwa spidi kubwa na karibu uchumi wetu utaupita huo wa Kenya: sasa utakuwa ni mjinga kiasi gani kuanzisha tena muungano wa aina hiyo na watu wa aina hiyo hiyo? Wanajifanya tumesahau waje watukwapue tena. Never over our dead bodies!
 
Yaani unavyosema wewe hakuna haja ya EAC sera za serikali ni tofauti! . Lakini sio shirika la Ndege pekee mifumo ni muhimu mfano mfumo wa elimu hata Afya tungeweka standard moja ingesaidia hasa Tanzania. Vita baridi imeisha na upande wetu wa kushoto ulishidwa vibaya!. Tumesema uchumi una kuwa kwa miaka 40 tupo palepale kila nchi uchumi una kuwa.
 
Bado hujaelewa tu? Tunakuambia huko ndiko tulikotoka. Huo mfumo wa elimu na afya ulioukazania ni kwamba ulikuwa ni mmoja. Baraza la mitihani lilikuwa ni la EAC likiitwa The East Africa Examination Council in colaboration with Cambridge University. Elimu ya chuo kikuu ilikuwa ya pamoja ikitolewa na The University of East Africa ambayo ilikuwa na colleges mbali mbali kwenye nchi zote tatu eg. Makerere University College ambayo ndiyo pekee ilikuwa ikitoa shahada za udaktari wa binadamu, Dar es Salaam University College ambayo ndiyo pekee ilikuwa ikitoa shahada za uanasheria, Nairobi University College ambayo ndiye pekee ilikuwa ikifundisha mafunzo ya shahada za uhandisi na udaktari wa wanyama, na kadhalika. Mwaka 1970 Kenya unilaterally ikajiondoa kwenye mifumo hiyo. Ikaanzisha university yake ya Nairobi ikifundisha mafunzo ya shahada zote kwa raia wake wa Kenya tu, na kuanzisha baraza lake la mitihani na mitara yake ya elimu. Ikabidi kila nchi ifanye hivyo. Huku Tanzania ikatubidi tuifanye University College ya Dar es Salaam kuwa University of Dar es Salaam kwa kozi zote kwa ajili ya vijana wetu. Tukaanzisha NECTA na NACTE za kwetu etc Uganda nao ikawabidi wafanye hivyo hivyo. Sasa hivi tunajitosheleza kwa kila fani hadi ziada ya maelfu na maelfu ya vijana wetu wenye hadi PhD degree wanaendesha boda boda. Kenya wana uhaba wa madaktari wa binadamu na hufikia kutuomba msaada na huwa tunawapatia expatriates hawa. Sasa wewe umeng'ang'ania kutaka kuturejesha tulikotoka? Kajifunze basi angalao kujua kwa nini Great Britain ime exit kwenye EU.
 
Yaani wewe ndiyo hujaelewa huwezi kutumia historia ya 1978 au 1979 kufanya maamuzi. Tulikuwa na vita miaka hiyo na Uganda, nchi zimeongezeka na vilevile vita baridi hakuna tena. Kama serikali hizi ambazo zinajua history hizo kuliko wewe wangekuwa wanafikiria hivyo wasingekutana tena kuanzisha hii jumuia! na kuna mpango wa kuwa na sarafu mmoja na wote wanakubali hilo. Hivyo tusije kujifanya kama vile serikali haitaki EAC kila wakiangalia strategy ina make sense kuwa na EAC na mambo niliyosema. Hatuwezi kuwa nchi ya kulalamikia kila kitu mara wakenya wamesoma zaidi.... tukisema tuweke standard sawa za shule ohh kimepanda kimeshuka! Sasa tunataka nini. Kuhusu ndege mashirika yote yanaenda kwa hasara kubwa sana kupunguza hasara ni kuwa na scale kubwa zaidi.
Hivyo sikubaliani na wewe najua history na nimeishi nchi tofauti kwa miaka zaidi ya 20 sasa
 
Kwa ufupi tu umoja ni nguvu. Ukiangalia vizuri kuna vitu ambavyo wana EAC tungeweza kufanya pamoja na kurahisisha maendeleo ya nchi zote

1. Madawa tungeweza kuagiza pamoja maana tunaumwa magojwa yale yale hii ingesaidia kupunguza bei ya uagizaji kwasababu tuna nunua kwa jumla. Lakini kwenye chanjo kama za Corona tungeweza kuagiza kwa pamoja na kugawana zikifika hapa!.

2. Mfumo wa elimu tungeweza kuweka mfumo mmoja hii ingesaidia wawekezaji wakija kwenye nchi mmoja kuwa na vijana wenye elimu zenye uwiano sawa. Vilevile ingesaidia kwa elimu za madaktari na walimu.

3. Usalama pamoja na kuwa na majeshi yetu tungeweza kuwa na jeshi ya EAC kwa ujumla kupambana na ugaidi na ku share hata satellite za usalama. Hii ingepunguza matumizi mabaya ya kijeshi maana tumekuwa dump la kuuziwa vifaa vya kizamani.

4. Shirika la ndege moja ni vichekesho kuwa na shirika la ndege kila nchi ! Tungefungua kampuni moja halafu wawe wanakodisha ndege kutoka nchi shiriki na kila nchi itakuwa na share kutokana na mchango wake hii ingepunguza gharama na kuongeza ushindani bila hivi mashirika ya nje yataendelea kutawala anga zetu.

5. Masoko ya mzao ya pamoja yaani kuwe na shirika la kuonhoza masoko ya biashara za mazao na bei ziwe wazi na kutangazwa kote kuwe na masoko ya jumla kila mpakani ya kisasa. Kama ilivyo dhahabu bei za mazao ziwe zinatangazwa kwa uwazi .

6. Tuwe na vyuo vya technologia na ufundi pamoja kufundisha teknologia mpya kama programming. Fungueni kampuni na kuingia mkataba na kampuni kama Microsoft, google, Apple na Oracle ili vijana wetu waweze kufanya kazi kutokea nchi hizi washiriki.

India mfano wana vijana kwa milioni wanafanya kazi za nchi nyingine kuanzia engineering design, customer service, payroll and accounting, bank support. kwanini sisi tushidwe wakati tuna vijana wengi.

Kwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa.
Kaka una mawazo ya ki liberal sanaa
Sijamaliza nimesoma namba 2 tu ikanishitua hapo ! Kwa uelewa wangu juu ya EAC hayo mawazo yako yote ni mazuri lkn HAITOTOKEA ndani ya EAC kuna nchi zina angalia maslai yake mfano Kenya ina taka inufaike kutoka tk nchi ambazo ni land locked ambazo zipo ndani ya EAC , at the same time Tz nayo inataka ilo soko
 
Sio kila kitu ni ushindani mfano kuweka viwango na mfumo sawa wa elimu hii haitanufaisha nchi mmoja. Kuagiza vitu kwa kwa pamoja ni yaleyale tofauti ni kwamba wauzaji watapunguza bei ya vitu mfano mimi nafanya kazi kama consultant kwenye kampuni ambayo ina shughulikia manunuzi ya hospitali hapa US. Tuna hospitali 3000 ambazo wote tunaenda kwa mkaba mmoja wa manunuzi ya dawa na hospitali kutokana na hii hospitali kwenye mkataba huu wanapata bei ya chini sana kulinganisha na zile zinanzafanya kipekee hii inaitwa GPO (Group purchasing Organization ) . Kwa mfano huu MSD na wenzao wa EAC wangeweza kuagiza vitu pamoja na kugawana vikifika hakuna ambaye anafaidika ni wote watafaidika. Bei ikiwa juu itafaidisha wauzaji tu! Mikataba ya pamoja lengo lake ndiyo hilo na ndiyo maana mbolea, mafuta tuna nunua kwa bulk procurement lakini tungenunua wote pamoja bei ingepungua zaidi na wote tungenufaika. Tunatumia muda mrefu sana kubishara na kuelezea nia za nchi ambazo ni mambo ya vijiweni wakati facts ziko wazi. Tukiweka uoga kwenye kila kitu hata logic hatutaweza kufikiria

Ukifuatilia mada zangu miaka 10 iliyopita niliongelea umuhimu wa vitambulisho sasa ndiyo serikali inafanikisha nilipigwa madongo ya kila aina kumbe niliona mbali kuliko wachangiaji wengine wakati ule. Na hili fikiria kwa makini miaka miwili ijayo utakubaliana na mimi.
 
..kila wakati waTz tunasema hatuko tayari ktk masuala ya EAC.

..yaani sisi waTz ndio wenye kigugumizi ktk mambo mengi ya EAC kuliko wanachama wenzetu.

..mimi nataka kujua jambo moja ambalo waTz tuko tayari, au tunalitaka ktk EAC, lakini wenzetu hawako tayari au wanaliogopa.

..kwa mtizamo wangu VIONGOZI wa Tz ni incompetent ktk kuwaandaa waTz ili kufaidika na fursa zinazotokana na malengo na mipango ya EAC.
 
Kama wewe wakati ule wa EAC ya zamani ulikuwa hujazaliwa, uwe unasoma basi angalao historia ya EAC kabla ya kuja na mawazo kama haya. Tunatakiwa kwanza kujua tulikotoka, mahali tulipo kabla ya kuamua tunakotaka kwenda.

Mara baada ya nchi za Uganda chini ya rais Milton Obote, Kenya (Jomo Kenyatta) na Tanzania (Julius Nyerere) kupata uhuru wake kutoka kwa muingereza ziliungana pamoja na kuunda EAC ambapo shughuli zote za kiuchumi na maendeleo za nchi hizi ziliendeshwa kwa pamoja kupitia umoja huo wa EAC. Hata pesa (currency) ilikuwa ni moja = East Africa shilling chini banki kuu moja ya EAC. Njia za mawasiliano, reli, ndege, meli, bandari na anga zote zilimilikiwa kwa pamoja. Viwanda vyote vilivyokuwa vinazalisha bidhaa mbali mbali hususani zana za kilimo, mafuta ya kula, blue band, beer na kadhalika vyote vilikuwa vinamilikiwa na EAC.

Lengo la waasisi wa umoja wa EAC lilikuwa baadaye nchi hizo tatu kuja kuungana kuwa nchi moja chini ya rais mmoja. Kilichokuja kutokea ni majonzi ambayo hatupaswi kuyasahau. Nchi ya Tanzania ilikuwa na siasa za kushoto, yaani za kijamaa, hivyo haikuwa inapendwa na nchi za magharibi. Nchi ya Uganda ilikuwa na siasa za kati. Kenya ilikuwa na siasa za kulia yaani za kibepari (capitalism) na hivyo ilikuwa kipenzi cha nchi za magharibi. Hata wazungu waliokuwa wakoloni wengi wao hawakuondoka Kenya baada ya uhuru. Wazungu hao walibaki huko wakimiliki mashamba makubwa makubwa (estates) na njia kuu za kiuchumi. Kwa kuwa wafadhili wakuu wa maendeleo ya nchi hizo za EAC walikuwa ni kutoka nchi za magharibi, walihakikisha karibu viwanda vyote vya EAC vilikuwa vinajengwa nchini Kenya - Nairobi, Mombasa etc. Ili kutupumbaza, kitu pekee kilichojengwa Tanzania ni jengo la makao makuu ya EAC pale Arusha.

Janja janja nyingi zifanyika kwenye jumuiya hiyo zikiendeshwa na upande wa Kenya walianza na kujitoa kwenye currency ya EAC. Wakaanzisha KSh na benki kuu yao. Mwaka 1977 wakati Tanzania tukigombana na Nduli Iddi Amini wa Uganda, Kenya walipora mali zote za EAC na kuvunja jumuiya hiyo. Kabla ya kuivunja walihakikisha vitu kama ndege zote za EAC, meli zote na train zote ziko nchini kwao. Hivyo tukajikuta hatuna hata kiwanda cha kutengeneza sabuni, bia, kiberiti, sindano wala cho chote kile. Yaani nchi yetu ikawa fukara wa kutupwa. Tukaanza upya from the scratch tena kwenye wakati mgumu sana kwani ilikuwa tunatoka kwenye vita dhidi ya nduli Amini iliyokuwa imetugharimu sana. Baada ya kufanya uporaji huo wa viwanda vya EAC, nchi ya Kenya ikawa ni nchi ya viwanda na soko kubwa la mazao ya viwanda hivyo likawa ni Tanzania na Uganda hadi leo.

Sasa baada ya kupitia yote hayo, tumejikongoja na kujenga viwanda, uchumi wetu unaendelea kupaa kwa spidi kubwa na karibu uchumi wetu utaupita huo wa Kenya: sasa utakuwa ni mjinga kiasi gani kuanzisha tena muungano wa aina hiyo na watu wa aina hiyo hiyo? Wanajifanya tumesahau waje watukwapue tena. Never over our dead bodies!

..nadhani mawazo yako ni ya KIZAMANI sana.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sio kila kitu ni ushindani mfano kuweka viwango na mfumo sawa wa elimu hii haitanufaisha nchi mmoja. Kuagiza vitu kwa kwa pamoja ni yaleyale tofauti ni kwamba wauzaji watapunguza bei ya vitu mfano mimi nafanya kazi kama consultant kwenye kampuni ambayo ina shughulikia manunuzi ya hospitali hapa US. Tuna hospitali 3000 ambazo wote tunaenda kwa mkaba mmoja wa manunuzi ya dawa na hospitali kutokana na hii hospitali kwenye mkataba huu wanapata bei ya chini sana kulinganisha na zile zinanzafanya kipekee hii inaitwa GPO (Group purchasing Organization ) . Kwa mfano huu MSD na wenzao wa EAC wangeweza kuagiza vitu pamoja na kugawana vikifika hakuna ambaye anafaidika ni wote watafaidika. Bei ikiwa juu itafaidisha wauzaji tu! Mikataba ya pamoja lengo lake ndiyo hilo na ndiyo maana mbolea, mafuta tuna nunua kwa bulk procurement lakini tungenunua wote pamoja bei ingepungua zaidi na wote tungenufaika. Tunatumia muda mrefu sana kubishara na kuelezea nia za nchi ambazo ni mambo ya vijiweni wakati facts ziko wazi. Tukiweka uoga kwenye kila kitu hata logic hatutaweza kufikiria

Ukifuatilia mada zangu miaka 10 iliyopita niliongelea umuhimu wa vitambulisho sasa ndiyo serikali inafanikisha nilipigwa madongo ya kila aina kumbe niliona mbali kuliko wachangiaji wengine wakati ule. Na hili fikiria kwa makini miaka miwili ijayo utakubaliana na mimi.

Unatema madini hadi basi, huwa siwaelewi wanaojitetea kwamba hawataki haya mambo kisa Kenya itakua inafuatilia maslahi yake, kwani kosa liko wapi hapo, kila nchi itaingia kwenye haya makubaliano baada ya kuzingatia maslahi yake kwanza, na hili umetaja la GPO litanufaisha maslahi ya kila nchii.
Wengne naona bado wameganda kwenye dunia ya 70s enzi za mababu zetu, leo hii tuko kwenye ulimwengu tofauti, mimi hapa kutwa nashinda na Watanzania, Wanigeria, Wachina n.k kwenye Skype tukifanya kazi pamoja, groups za kwenye Whastapp tumefungua za miradi tofauti tunachat utadhani tupo kwenye ofisi moja.
 
Ndoto ya kuwa na common currency nayo ilikuwa nzuri sana na ingekuwa more powerful kuliko hata shilingi ya Kenya lakini wasio na upeo wa kuona mbali na umuhimu mkubwa wa common currency wakaiua ndoto hiyo.
Ndoto haiwezi kutimia kwa kutarajia itimie mkuu. Inabidi uifanyie kazi. Kama kitu kinamanufaa kwanini usikifanyie kazi?
 
Ndoto ya kuwa na common currency nayo ilikuwa nzuri sana na ingekuwa more powerful kuliko hata shilingi ya Kenya lakini wasio na upeo wa kuona mbali na umuhimu mkubwa wa common currency wakaiua ndoto hiyo.

..hata mimi nilikuwa nafikiria kama wewe.

..kwanini EAC tusiwe na sarafu moja?

..kwanini tusiwe na mfumo mmoja wa elimu?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Yaani wewe ndiyo hujaelewa huwezi kutumia historia ya 1978 au 1979 kufanya maamuzi. Tulikuwa na vita miaka hiyo na Uganda, nchi zimeongezeka na vilevile vita baridi hakuna tena. Kama serikali hizi ambazo zinajua history hizo kuliko wewe wangekuwa wanafikiria hivyo wasingekutana tena kuanzisha hii jumuia! na kuna mpango wa kuwa na sarafu mmoja na wote wanakubali hilo. Hivyo tusije kujifanya kama vile serikali haitaki EAC kila wakiangalia strategy ina make sense kuwa na EAC na mambo niliyosema. Hatuwezi kuwa nchi ya kulalamikia kila kitu mara wakenya wamesoma zaidi.... tukisema tuweke standard sawa za shule ohh kimepanda kimeshuka! Sasa tunataka nini. Kuhusu ndege mashirika yote yanaenda kwa hasara kubwa sana kupunguza hasara ni kuwa na scale kubwa zaidi.
Hivyo sikubaliani na wewe najua history na nimeishi nchi tofauti kwa miaka zaidi ya 20 sasa
Swali la msingi turudi tulipotoka?kwa utaratibu upi? Machache ya kuchangia

TANZANIA inataka mahusiano ila sio ya muda mfupi yaani lengo likikamilika baasi hakuna mahusiano.
Hayo maeneo ya afya na elimu na curency tulitoka huko je una hakika kwa nn tulishindwa na leo tunataka kurudi bila kutibu chanzo?.
Unadhani iyo milengo ya kijamaa au kibepari au kilibelali haiko?
Tatizo ambalo jumuia ya afrika mashariki hasa Kenya na Rwanda wanaona TANZANIA inasuasua ni suala la Ardhi. Na si vinginevyo.
Rejea mazungumzo kuhusu jumuiya kupitia bunge na vyanzo mbali mbali tangu enzi za rais Mkapa.
Awamu ya kwanza walipambana viwanda vikawa kwao tukabaki na majengo....sasa kipaumbele si viwanda bali ni ardhi.
Unaposema elimu ya yule kubwa au ndogo unapotoa ulinganifu inabidi mwenye kubwa aende kumfundisha mwenye ndogo?
Unashauri mitaala.yetu iende kutatua changamoto za kikanda zaidi kuliko za kitaifa ?
Hitimisho
Kukaa kando si kwamba hutaki kusafiri ila unajipa mafasi kuanza safari kwa uhakika zaidi..upendo ndani ya nyumba hauokotwi unajengwa na unajengwa kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho..ukiwa na upendo wa masika na kiangazi lazima ndoa iwe na makando kando yasiyo na sababu
 
La elimu nalipigia chapuo sana, muhimu tuwe na mtaala mmoja wa elimu, mengine yanaweza yakaja taratibu lakini kwanza sote tuwe kwenye level moja kielimu. Huku Kenya tumezindua mtaala mpya unaolenga uwezo wa mtu na kumboresha na sio tena kusoma ilmradi uonekane umekwenda shule na una vyeti ila hamna kikubwa unachoweza kubuni.

Viongozi wote ukanda huu waliangalie hili la kutuunganisha kielimu. Sawa kunao wameng'ang'ania eti lilikuwepo enzi za EAC ya kitambo na likabuma, sasa sielewi hilo wanalitumia vipi kama kijisababu cha kukatalia hili wazo, siku zote usiwe mtu wa kughairi kitu kisa ulijaribu kikaangukia pua, waliobuni umeme, tarakilishi/computers na mengine wangekua watu wa kukata tamaa leo hatungekua tunanufaika nawo.

Kuna wengine wanasema tusiungane kisa ardhi ya Tanzania itatwaliwa yote, sawa basi mbona tusiungane kwenye mengine ibaki ardhi tu, natamani sana hili la soko la watu milioni 150.
 
Kila siku watu mara kufungiana mipaka, mara kuchoma moto bidhaa za nchi jirani. Tunajua tunachokitaka kweli? Bora ivunjwe tujue moja.
 
Yaani wewe ndiyo hujaelewa huwezi kutumia historia ya 1978 au 1979 kufanya maamuzi. Tulikuwa na vita miaka hiyo na Uganda, nchi zimeongezeka na vilevile vita baridi hakuna tena. Kama serikali hizi ambazo zinajua history hizo kuliko wewe wangekuwa wanafikiria hivyo wasingekutana tena kuanzisha hii jumuia! na kuna mpango wa kuwa na sarafu mmoja na wote wanakubali hilo. Hivyo tusije kujifanya kama vile serikali haitaki EAC kila wakiangalia strategy ina make sense kuwa na EAC na mambo niliyosema. Hatuwezi kuwa nchi ya kulalamikia kila kitu mara wakenya wamesoma zaidi.... tukisema tuweke standard sawa za shule ohh kimepanda kimeshuka! Sasa tunataka nini. Kuhusu ndege mashirika yote yanaenda kwa hasara kubwa sana kupunguza hasara ni kuwa na scale kubwa zaidi.
Hivyo sikubaliani na wewe najua history na nimeishi nchi tofauti kwa miaka zaidi ya 20 sasa
Wewe utakuwa ni mkenya au kibaraka wa Kenya.
 
Back
Top Bottom