Utafiti wangu kuhusu "profile pictures" za watumiaji wa mitandao ya kijamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Nilifanya kautafiti kadogo juu ya Profile picture na picha wanazoweka watu kwenye Account zao za mitandao ya kijamii.

Nikabaini mambo yafuatayo:

1. 90% ya walioweka picha Nusu/Passport size (kuanzia kiunoni mpaka kichwani) ni Wafupi.
Pia hawana maumbo ya kuvutia.
Hii ipo kwa pande zote, wakike Kwa wakiume.

UTAFITI wangu ulionyesha kuwa watu Wafupi hawapendi kujitambulisha kama ni wafupi kupitia DP (Profile picture) zao, hivyo hujikuta wakizikata/Crop na nyingi zipo nusu/passport size

Waliowarefu na wenye maumbo mazuri ndio huweka DP ambazo ziko full zinazowaonyesha mwili mzima.

Hata hivyo wapo wanawake Wafupi wenye maumbo nao huweka picha Full DP lakini wakionyesha upande wa nyuma wa miili yao yalipo matako.

Utafiti wangu unaonyesha kuwa, Wafupi wakiweka picha Full DP, basi ujue wamevaa viatu virefu, au mpiga mpicha ameichukua kamera kwenye pembe tokea chini. Hii humfanya Mhusika/object kuonekana ni mrefu.

Nilipowahoji baadhi ya watumiaji wa mtandao kuwa walishawahi kukutana na watu wasiowajua kupitia mtandao walikubali lakini wengi wao walisema walitarajia kuwaona watu hao kuwa ni warefu Kama waonekanavyo kwenye picha za mitandao.

2. DP nyingi za watu 70% zimeiditiwa,

3. DP nyingi ni picha za zamani au mpya zilizopigiwa katika Mazingira maalumu

4. Waweka DP wengi zenye picha zao huwa ni makundi Yafuatayo;

1. Wanafunzi wa chuo hasa wenye Sura za kuvutia

2. Watu wazima hasa wenye vyeo, hadhi au umashuhuri

3. Vijana wenye Sura za kawaida au kuvutia.

Makundi ambayo hayaweki DP za picha zao halisi

1. Wenye Sura za tafadhali nipigie

2. Wenye makovu au majeraha au kasoro yoyote

3. Wazee waliokwisha kuzeeka kabisa, Sura zina makunyanzi.

4. Wasiojiamini na kujivunia vile walivyo.

Kundi hili hupenda kuweka DP yenye picha zifuatazo

1. Watoto au wazazi wao

2. Kuweka picha za vitu vya kifahari walivyonavyo wanavyojivunia navyo Kama vile picha za magari, nyumba, au Jambo lolote

3. Kuweka picha za watu mashuhuri Kama viongozi, wacheza mpira, maua, Fahari ya mandhari ya Dunia, Aya za Biblia au misahafu n.k.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa uwekaji wa DP unategemeana na mambo Yafuatayo:

1. Umri wa Mhusika
2. Mtazamo na ideolojia yake
3. Maumbile ya Mhusika
4. Elimu na Uelewa wa dunia iendavyo (Exposure)
5. Hali na hadhi ya Mhusika
6. Watu wanaomzunguka.

Hata hivyo Nimebaini kuwa 95% ya DP zenye picha za wahusika ndizo picha wazipendazo Kwa wakati husika.

Watu wengi huweka DP picha nzuri Ile aipendayo kwa wakati husika.

Hata hivyo uchunguzi wangu ulibaini kuwa endapo DP ya mtu ikipondwa na watu wasiopungua kumi basi mtu hujisikia vibaya na huweza kuibadilisha Kwa haraka Sana.

Uchunguzi wangu ulienda mbali kuhusu uwekaji wa picha Mtandaoni na nini dhamira ya wahusika kuweka picha zao mitandaoni.

Sababu zifuatazo zilijitokeza:

1. Kama Fasheni
Wengi hutuma picha Mtandaoni Kama Fasheni, kwa vile watu wengi hupost picha.

2. Kutunza kumbukumbu
Wapo hu-post picha mitandaoni Kama sehemu ya kuzihifadhi picha zao.

3. Kukomesha na kujigamba Kwa mahasimu wao. Hii inaweza kukushangaza, lakini uchunguzi wangu ulibaini kuwa Asilimia kubwa hu-post picha mitandaoni kuwatisha, kuwakomoa na kujigamba Kwa mahasimu wao.

Wengi hutuma picha kujionyesha nao wamo, mambo Yao Safi, kila kitu kipo shwari kabisa. Ndio maana 99% ya picha za zitumwazo na watumiaji wa mitandaoni huwa ni nzuri wakiwa sehemu za ufahari, Raha, wakiwa wamependeza. Zingine hupiga wakiwa na watu mashuhuri au wakiwa Maeneo Maarufu.

4. Kupenda picha
Baadhi hupost picha Kwa sababu wanapenda kupiga picha na kuzipost.

5. Kutafuta marafiki na mahusiano Mapya.

Wapo pia wanaopost picha kwa lengo la kutafuta wenzi wa maisha au kwa ajili ya biashara ya ngono.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa, kutokuwa na mavazi mazuri na mahali pazuri pakuishi huwafanya wengi washindwe kupiga picha za ku-post mitandaoni.

Pia lipo kundi ambalo halipendi na pengine halijawahi ku-post picha yoyote Mtandaoni licha ya kuwa limejisajili na linatumia mitandao ya kijamii.

Kundi hili Kwa uchunguzi, nilipolifikia nikagundua mambo YAFUATAYO:

1. Wengi wao hawajiamini, na wanamatatizo ya kisaikolojia.

2. Wengi huogopa kukosolewa, au kusemewa maneno mabaya kuhusu maumbile Yao

3. Dhana potofu, kasumba na ushamba kuwa kuweka picha Mtandaoni ni hatari.

4. Wachache hawapendi tuu kutambulika. Hili ni lile kundi lisilipenda kutambulika au kujitambulisha hata kwenye mambo ya kijamii achilia mbali Mtandaoni.

5. Wafanyakazi hasa wa kazi maalumu, iwe ni Usalama wa taifa, Utapeli, au kazi yoyote inayomtaka mtu afiche utambulisho wake.

Lipo kundi ambalo haiwezi kupitisha siku bila ku-post picha zao, tena wengine Kwa siku hu-post picha mbili mpaka tatu mtandaoni.

Kundi hili pia uchunguzi wangu ulibaini linamatatizo ya kisaikolojia Kama lilivyo kundi lile lisilopost picha yoyote.

Uchunguzi huu hauna tija kwako hasa tija ya kiuchumi.

Karibuni Kwa mjadala

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Mafinga
 
Du Safi mkuu Kwa tafiti ,japo yapo mambo ya msingi ya kufanyia tafiti Kama lishe ,magonjwa n.k.ambayo ungeisaidia serikali kupata suruhu.
Badala ya makalio ya picha za kina Dada mtandaoni,Mana wao sirikali wako bize kumnyosha mtu huru na wenzake mpaka waseme pooo
 
Du Safi mkuu Kwa tafiti ,japo yapo mambo ya msingi ya kufanyia tafiti Kama lishe ,magonjwa n.k.ambayo ungeisaidia serikali kupata suruhu.
Badala ya makalio ya picha za kina Dada mtandaoni,Mana wao sirikali wako bize kumnyosha mtu huru na wenzake mpaka waseme pooo


Nashukuru Mkuu,
Nitayafanyia kazi mawazo yako
 
Du Safi mkuu Kwa tafiti ,japo yapo mambo ya msingi ya kufanyia tafiti Kama lishe ,magonjwa n.k.ambayo ungeisaidia serikali kupata suruhu.
Badala ya makalio ya picha za kina Dada mtandaoni,Mana wao sirikali wako bize kumnyosha mtu huru na wenzake mpaka waseme pooo
Huyu jamaa amewaza nini mpaka kufanya utafiti huu,inawezekana in mhanga mmojawapo Wa hayo aliyoainisha hapo kwenye tafiti zake.

Kimtokacha MTU nje ndo alivyo ndani.
 
Huyu jamaa amewaza nini mpaka kufanya utafiti huu,inawezekana in mhanga mmojawapo Wa hayo aliyoainisha hapo kwenye tafiti zake.

Kimtokacha MTU nje ndo alivyo ndani.


Hiyo ni moja ya Hobby zangu.
Hivyo Relax

Kwani huo ndio uchunguzi wangu WA Kwanza kwako kuusoma?
 
Hiyo ni moja ya Hobby zangu.
Hivyo Relax

Kwani huo ndio uchunguzi wangu WA Kwanza kwako kuusoma?
Sawa mkuu,nkadhani na wewe umeweka picha yako hapo juu kuanzia unyayo hadi juu kuficha ufupi,jokes.

Nishasoma chunguzi zako nyingi tu mkuu hii so ya kwanza.
 
Back
Top Bottom