Utafiti-Wanawake msichelewe kuzaa

Utafiti-Wanawake msichelewe kuzaa

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
14,563
Reaction score
22,838
Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.

Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Wanawake wengi wanaofanya kazi huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofika umri a miaka 35 badala ya kuzaa wakiwa na umri wa miaka 24-28.

Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi.
Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''

Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.

Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.

Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .

Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.

Source:BBC

Mmm!!!! HIV inarelate vip na kuchelewa kuzaa? Pia huyo dr kasema eti age ya kuzaa ni kati ya 24_28, hivo dada zetu walio na 29 yrs wanashauriwa wasizae?
 
Mmm!!!! HIV inarelate vip na kuchelewa kuzaa? Pia huyo dr kasema eti age ya kuzaa ni kati ya 24_28, hivo dada zetu walio na 29 yrs wanashauriwa wasizae?
Amesema huo umri ndo mzuri na siyo kwamba ukifika 29yrs hauwezi kuzaa
 
Mmm!!!! HIV inarelate vip na kuchelewa kuzaa? Pia huyo dr kasema eti age ya kuzaa ni kati ya 24_28, hivo dada zetu walio na 29 yrs wanashauriwa wasizae?

HIV.......kupigwapigwa sana!! miaka35 hawezi kuwa mchumba mmoja toka ana 24!!!!
 
Nikweli hii, wanawake hasa wamujini na mkishazaa hamtaki atakunyonyesha...
 
Mi wasemege tu vyote kwakweli......mengine nitayatimiza kwa wakati/nafasi yangu!
Mbona kulikuwa na kina Sara, Hanna (biblical fact) n.k ambao walichelewa kupata watoto na hawakupata madhara hayo?

Unless otherwise....nipate maelezo ya kutosha! Akili yangu inanituma kwamba kuna mengi yanachangia katika hilo rather than kuchelewa tu kuzaa.
 
Hao walikuwa na imani wakimtegemea mungu na kuwa na imani kubwa sasa kizazi chenye iman haba hiki na magonjwa lukuki hata huyo sara ilikuwa mpango wa mungu hebu niambie baada ya kuzaa mtoto isaka alizaa nan mwingine? kizazi hiki wanachoropoa mimba wakiogopa maisha madhala yake huonekana baadaye
 
Tusiarakishane bana. Maisha yenyewe haya unamalizia chuo na kukaa nyumbani miaka hata miwili ndo upate kazi ya kueleweka. .. Hapo majukumu kibao,watoto now days st kayumba aziwafai akiwa tu baby class tatakiwa nitenge kiasi cha kutosha kwa ajili ya ada.

Ngoja tu nichelewe mwanangu asitaabike.
 
Hakuna anayekuharakisha chaguo ni lako tu,huo ni utafiti
 
Back
Top Bottom