Elections 2010 Utafiti wa Synovate wabadilishwa kuisaidia CCM?

utabiri wa shehe yahya,synovate na redet ni sawasawa! wakati shehe anatumia nguvu za giza kutabiri, synovate wanatumia nguvu ya fedha na redet nguvu ya watawala!!!!
Utabiri wa wengi ni kwamba Waaminio mizimu hawatauona ufalme tena.
mwaka 2005, mkwere alikuwa chaguo la mungu, sasa amekuwa chaguo la she yahya, nguvu za giza.
tupe wako halafu tukutane novemba mazee,acheni kulialia na ninyi si m publish poll zenu za JF ambazo zinaonesha wa kwenu ana 90%.
 
Tetesi nilizopata ni kuwa wale watafiti wa Synovate Tanzania (ambayo inaongozwa na Wakenya) wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu media ya Tanzania ambao unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya habari kwenye vyombo hivi ni kuhusu chama tawala CCM.

Pengine hii inaashiria kuwa zile posho za CCM kwa waandishi wa habari kwenye kampeni ya Kikwete za shilingi laki moja kwa siku (100,000/-) zinafanya kazi. Utafiti unadhihirisha kuwa waandishi wa Tanzania wamenunuliwa na CCM na sasa wanalipa fadhila kwa kutoa habari za kukipamba chama tawala.

Haya ni matokeo:

1. Zaidi ya asilimia 50 ya habari kwenye media ni kuhusu CCM

2. Chadema inapata coverage ya kama 20%

3. Vyama vilivyobaki, CUF, NCCR, TLP, etc vinagawana asilimia iliyobaki.

Binafsi sijaiona hii taarifa ya utafiti, ila nina fahamu kuwa magazeti ya kesho ya kila siku yatatupa taarifa.

Pia, utafiti umeonyesha kuwa gazeti la serikali la DAILY NEWS ndiyo linaongoza kwa kuipendelea CCM. Kaimu mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali (Daily News, Sunday News na Habari Leo), Mkumbwa Ally, anasifika hapa mjini kwa kujipendekeza kwa Kikwete ili ateuliwe yeye kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali.

Utafiti huo umetoa marks/grades kwa magazeti na televisheni mbalimbali kuhusu coverage yao kwa vyama vya siasa, ikiwemo Habari Leo, Uhuru, Mwananchi, The Citizen, na magazeti mengine.

* ANGALIZO: Utafiti haujaeleza lolote kuhusu mgombea gani kati ya Dk. Willibrod Slaa, Kikwete au Lipumba anakubalika zaidi na wananchi, umeangalia mwenendo wa media tu.
 
SYNOVATE hawawezi kutoa taarifa threat kwa CCM. hili la coverage ni minor kwa jamii ambayo haijaelimika kuhusu matumizi wiano ya vyombo vya habari.
Lakini kama wangesema kuwa mgombea wa CHADEMA anaongoza ktk kura ya maoni nakwambia tungesikia yamewakuta kama yule meneja wa kiwanda cha mtibwa.

Kesho kutwa tutawasikia REDET wakija na tafiti za kuijenga Tume ya Uchaguzi.

TUSIDANGANYIKE
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari TBC1 kuhusu utafiti huo wa coverage ya vyombo vya habari kuhusu kampeni za uchaguzi.

Vinatia aibu, hasa hivi vya serikali/umma.
 
Katika kile kinachoendelea kutokea na kuaminika ya kwamba watanzania wengi wamekuwa na imani na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imedhihirika baada ya kampuni moja ya hapa nchi inayofanya tathimini zake kuibuka na tathimini iliyo kuwa inasema ni chama gani kinacho kubalika kwasasa kutokana na muelekeo wa taifa katika uchaguzi mkuu ujao.

katika tarifa hiyo ilionyesha ya kuwa chama cha CHADEMA kinaongoza kwa asilimia 44% kikifuatiwa na chama cha CCM kwa asilimia 41% na asilimia zilizo salia kugawanyika kwa vyama vingine,

kutokana na ushabiki uliopo kwasasa taarifa hiyo ikapindishwa na kuandikwa visivyo baada ya kuonekanika ya kuwa CHADEMA inaongoza, ndipo ikaamuliwa taarifa hiyo iachwe isomwe ile ya ya vyombo vya habari, katika hili makada waliyo ingia ubia na chama cha ccm kukikampenia ambao ni wamiliki wa kituo kimoja cha radio station alipo pata taarifa hiyo aliamua kupiga simu kwa boss wa kampuni hiyo ya utafiti ya SYNOVATE kwakuwa ni rafiki yake na kumuamuru taarifa hiyo isitoke

boss huyo ndipo akaamua kupinndisha taarifa hiyo nyeti iliyo kuwa ikiwahusisha wananchi mbali mbali na sekta mbalimbali hapa nchini, MUNGU ENDELA KUIBARIKI CHADEMA
 
shauri yao na utafit wao sisi tuko Mara tunachanja mbuga.
Chadema tuko Juuu sana.
 
Mbona hawatafiti na kutoa data za kwenye mitandao kama watafiti makini wanavyofanya?
Hakuna ndugu wala jamaa yangu hata mmoja aliyewahihojiwa na SYNOVATE wala REDET labda nduguyo
 
Kuna taarifa kuwa Synovate wapo njiani kutoa matokeo ya maoni ya watanzania kuhusiana na uchaguzi 2010.

Wasiwasi wangu ni kuwa bado watatumia sampuli ya watu 1,000 - 2,000 ambapo huenda wasipate uhalisia wa mambo ingawa report yao itaweza kutumiwa na baadhi ya wagombea kisiasa. Kwakuwa sijajua nini kitaongelewa basi fuatilia comments chini...

Tutarajie nini?

Mimi nafananisha kampeni ya CCM kuwa sawa na mashua iliyoundwa kwa mti wa mpodo, ambao hauwezi kustahimili vishindo vya maji ya chumvi kwenye bahari kubwa ya Tanganyika, huku nahodha wake, JK, akijitahidi kuchota maji ndani yake ili isizame kwani mashua ina matundu mengi yanayoingiza maji ndani (soma: hoja zisizo na msingi na ahadi kede kede zisizotekelezeka na za uongo...). Kadri jinsi nahodha JK anavyojitahidi kuchota maji, kumbe ndivyo anavyozidi kuadhirika, kwani sasa matundu yanaongezeka na kuwa makubwa, mashua inazidi kuzama baharidi.

Kwa upande mwingine - hapa ngoja nizungumze kwa Kiitaliano kidogo.... Inoltre, nell'alta parte ... mashua inayoongozwa na nahodha wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa, imeundwa kwa miti ya mitiki, ambayo ndiyo haswa inayofaa kwa safari za baharini, kwenye maziwa na mito. Slaa hana tatizo la kuchota maji toka ndani ya mashua yake ya kampeni; haina matundu yoyote. Kila kitu ni shwari. Anaendelea, polepole na salama. Hana shida. Ingawa CCM wanajaribu kurusha makombora kuiharibu mashua, mitiki inastahimili vishindo, hakuna madhara. Ila makombora wanayorusha kumbe yana milipuko inayobaki nyuma, kwa hiyo wanazidi kuharibu mashua yao ya MPODO!

Utafiti wa Synovate na Redet ni mojawapo ya makombora ambayo ni mapya, yaliyoandaliwa na CCM, kujenga hoja (isiyo na msingi) kumvika JK joho lililotengenzwa kwa kioo, ambalo pindi atakapolivaa litapasuka LOTE! Matumizi ya pesa yasiyo na tija, kufanya utafiti usio na kichwa wala miguu, kupoteza muda na malengo! HAWAWEZI! Muda watapoteza, malengo yako pale pale. Wote tunajua, hawa ni wapiga debe wa mfalme JK, ambao hawana ubavu wa kusema, Mfalme yuko uchi, hajavaa nguo. Wataendelea kusema, Jamani mfalme amependeza na nguo yake yenye vito vingi vya almasi, rubi na dhahabu! Wapi! Mwambieni ukweli mfalme wenu; hajavaa nguo! Mnamdanganya, mnampotosha, kwa kutaka sifa kwake! Siku akiwagundua mtakiona cha mtema kuni!

-> Mwana wa Haki

UFISADI utatupwa nje tu! Wala tusibabaishwe na Synovate!
 
Matokeo hayo tuliyategemea na hakutakuwa na mabadililiko isipokuwa tu kwa watanzania kwenda kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Kwa kweli hawa watu wanatuabisha watafiti wa Tanzania. Huwezi fanya kitu cha kuangalia ni chama gani kinaandikwa na kutangazwa zaidi na vyombo vya habari, kisha akaita huo kuwa ni Utafiti!!! What a rubbish.... Alafu wakaja waandishi njaa wa gazeti la uhuru wakasema chama kilichoongoza kwa kuandikwa zaidi eti 'kina mvuto'!!!! Mbona watu wanapenda kujifanya wajinga?

Yes, CCM inaandikwa zaidi kwa sababu yapo ya kuandikwa; Mwenyekiti wao kaanguka jukwaani, wanachama wake wamesingiziwa sio raia, wanachama wake wanakihama chama, wanachama wake wanakamatwa na Takukuru kwa rushwa, wagombea wake wanabembeleza watu waende kwenye mikutano, makada wake wanapeleka watu mikutanoni kwa malori, mipasuko na makundi chungu nzima nk nk alafu unasema inaandikwa kwa sababu ina mvuto!!!

Mi naomba hao synovate waipublish report nzima (kwenye gazeti of coz kwa sababu hakuna journal itakayopokea takataka kama hiyo), ili tuone objectives, methodology na result zilizopatikana.... swine...
 
Kwa namba ya wapiga kura nchini na kama watatumia sample ya 1000 to 2000 nadhani haitakuwa na uwakilishi mzuri be it in favor of upinzani or tawala!

Labda kwenye report yao wataeleza sample ilikuw aya watu wangapi, maeneo walipofanyia utafiti, aina ya maswali etc. Itapendeza sana kama watatoa report yao live ili maswali yaweze kuulizwa
 
Nimesikia tetesi kwamba shirika la utafiti la Synovate limeipatia Chadema alama za ushindi 44% ikifuatiwa na CCM 41% lakini limeshauriwa lisiyatangaze hadharani badala yake liseme CCM inapendelewa kwa kutangazwa zaidi kwenye media. Nasema tena hizi ni tetesi tu kuna mwenye data kamili atujuvye.
 
Labda kwenye report yao wataeleza sample ilikuw aya watu wangapi, maeneo walipofanyia utafiti, aina ya maswali etc. Itapendeza sana kama watatoa report yao live ili maswali yaweze kuulizwa



Hii yote wadau wenzangu ni kwa sababu Tanzania tunalea vitu kama hivi. Inatakiwa Comrade Dr Slaa akishaapishwa, mara moja anatangaza tafiti zote zinazolenga kupotosha jamii zikome, tafiti zote zisizokuwa na malengo mazuri watarajie kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

kwa sababu, kama mtu amesoma na kufaulu katika fani yake haina maana kukiuka misingi ya kazi zake, eti kwa sababu ya pesa aka ana njaa.

Inabidi watu warejeshwe kwenye maadili ya kazi zao mara moja baada ya Mh. Rais D. Slaa kuapishwa. We don't need this kind of shit in 21st century. Tunataka facts hata aisyeenda shule akielezwa japo kidogo aelewe.
 
Back
Top Bottom