Utafiti mdogo nilio ufanya juu ya chaguzi za viongozi na uelewa wa wanainchi juu ya haki zao za kikatiba zinavo takiwa kutekelezwa

Mathiasyusuph

Member
Jul 13, 2021
53
68
Ndugu zangu habalini za wakati huu, poleni na majukum ya kulijenga taifa.

Niende moja kwa moja ktk mada tajwa hapo juu
Watanzania wengi hususani wa vijijini hawana uelewa wa haki ya kuwawajibisha viongozi wao ktk maswara ya haki zao za kikatiba zinapo shindwa kutekelezwa na viongozi walio waweka madarakani.

Kwamfano: inakua vipi tz toka imepata uhuru mpaka sasa huduma za msingi kama vile Barbara, vituo vya afya, elimu na maji safi na salama viwe nivya kukosekana au hafifu na bado ikifika uchaguzi wanainchi wanasahau kuwawajisha hao viongozi?

Na wanasahau shida zao wanawachagua tena?na baada ya uchaguzi hao walio chaguliwa wanaondoka na kwenda kutunga sheria mbovu ambazo hazimnufaishi wanainchi wa kawaida bali ni faida kwao hao viongozi tuu!

Na baada ya miaka mitano wanaludi tena wapewe ligha na hao wanainchi badara ya kuwadhibu kikatiba wanawachagua tena.

Nilicho kigundua ni wanainchi wengi hususani wa vijijini hawana uelewa wa wajibu wao ktk maswara ya katiba inasema nini juu ya kuwaondoa hao viongozi walio shindwa kutekeleza kero za wanainchi.

Wengi wameridhika na hali iliopo tangu uhuru mpaka leo na linapo kuja swara ya hatima ya maisha yao hawana maamzi yenye tija kwao wao ni ndiyo tuu!!

Na ukiwambia tubadilishe hiki chama wanakwambia inaweza ikatokea vita au alie oa mama yako ndie baba yako, na hayo ndio majibu unayo yapata.
Nikachunguza zaidi nikaona chanzo cha haya yote ni ukosefu wa:
1: lishe bora kipindi cha utoto

2: Elimu ilichelewa kusambaa hususani vijijini.

3: umaskuni na ufukara vimekidhili ndani ya jamii nyingi.

4: udhubutu wa ujasiri haupo na uoga vimetamalaki ndani ya jamii nyingi.

Mwisho
Ili kuweza kung' oa hawa viongozi wasio jari masirahi ya wanainchi wa chini nilazima kuwepo uelewa wa katiba inasema mini na Mimi kama raia nina uchungu gani na haki zangu.

Asanteni sana. Ijumaa njema.
 
Tatizo kubwa zaidi ni kwenye muundo na namna ya usimamizi wa chaguzi,wateuliwa wa mtawala kuwa sehemu ya kumsimamia mteuzi kwenye kuhakikisha mteuzi anaendelea au laa,hakuna lugha nyingine ya kuiita zaidi ya rushwa,hivyo mtoa rushwa ana nafasi kubwa ya kupata upendeleo,na mteuzi haishii hapo pia ana dola na vyombo ambatano anavyoviamuru atakavyo kulingana na mamlaka na mkao wa katiba iliyopo,hivyo dawa ya yote ni Katiba mupya na sii vinginevyo.
 
Tatizo kubwa zaidi ni kwenye muundo na namna ya usimamizi wa chaguzi,wateuliwa wa mtawala kuwa sehemu ya kumsimamia mteuzi kwenye kuhakikisha mteuzi anaendelea au laa,hakuna lugha nyingine ya kuiita zaidi ya rushwa,hivyo mtoa rushwa ana nafasi kubwa ya kupata upendeleo,na mteuzi haishii hapo pia ana dola na vyombo ambatano anavyoviamuru atakavyo kulingana na mamlaka na mkao wa katiba iliyopo,hivyo dawa ya yote ni Katiba mupya na sii vinginevyo.
Sasa katiba mpya itapatikana vipi ilihali wanainchi niwaoga wa kuidai kwa nguvu na vitendo?
 
Back
Top Bottom